Mmmh!....HII SASA IMEZIDI; YAANI HATA IKULU INATUMIA "@YAHOO.COM" ??!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mmmh!....HII SASA IMEZIDI; YAANI HATA IKULU INATUMIA "@YAHOO.COM" ??!!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Augustoons, Sep 4, 2008.

 1. Augustoons

  Augustoons JF-Expert Member

  #1
  Sep 4, 2008
  Joined: Oct 31, 2007
  Messages: 410
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Wakuu heshima mbele,
  Siku chache zilizopita kulikuwa na thread hapa ikijadili kuhusu mfuo wa mawasiliano wa ikulu na mtumizi ya website au barua pepe,suala hili pia lilipata kuibuliwa kule bungeni.Niliufatilia sana mjadala huu japo sikuweza kutoa maoni yoyote.Kwa hakika sasa nimethibitisha ubabaishaji wa kurugenzi ya mawasiliano pale.Nimeshtuka sana pale nilipoona press release ya serikali kabisa ikitumia anwani ya @yahoo.com. Hivi kweli are we serious?serkali inashindwaje kuwa na domain name ya barua pepe kama hiyo @ikulu.go.tz?

  Mimi kama mdau ambaye kwa kiasi fulani nimesoma mambo ya cyber crimes and law,moja ya vitu ambavyo hackers/scammers hutumia katika kuwadanganya watu ni hizi general public addresses like @gmail.com,@yahoo.com nk.na mara nyingi inashauriwa unapopokea tarifa inayoclaim kutoka ofisi fulani maalumuahalafu ofisi hiyo mawasiliano yake ni @yahoo.com au @gmail lazima uwe na mashaka kuhusu veracity yake.Nilipoingia katika website ya serikali leo,hiki ndicho nilichokutana nacho, na hii ni moja ya anwani niliyokutana nayo ikulumawasiliano@yahoo.com:
  DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

  UNITED REPUBLIC OF TANZANIA[
  /CENTER]


  Telephone: 255-22-2114512 , 2116898

  E-mail: ikulumawasiliano@yahoo.com

  press@ikulu.go.tz

  Fax: 255-22-2113425


  PRESIDENT’S OFFICE,

  THE STATE HOUSE,

  P.O. BOX 9120,

  DAR ES SALAAM.

  Tanzania.

  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


  Rais Jakaya Mrisho Kikwete wa Tanzania na Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika, amesema Marehemu Levy Mwanawasa wa Zambia ameishi na kuwatumikia wananchi wa Zambia kwa mapenzi, kujitolea, heshima na kwa dhati kubwa na wananchi wa Zambia wanaweza kumlipa hilo kwa kumuenzi katika matendo yake haya.  Rais Kikwete amewaambia waombolezaji katika viwanja vya bunge mjini Lusaka leo wakati wa Misa ya kumuombea Marehemu iliyohudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kimataifa, viongozi wa dini na wananchi kutoka sehemu mbalimbali nchini.  “Ameishi maisha yake na kuwatumikia watu wake kwa mapenzi, heshima na kwa ustaarabu, kitu mnachoweza kumrudishia ni kumuenzi, fuateni na tekelezeni yale aliyobakiza”.  Rais Kikwete ametoa salamu hizo kwa niaba ya viongozi wa Afrika watu wake na Tanzania ambapo amewaambia wananchi wa Zambia kuwa Mrehemu Mwanawasa alikuwa rafiki na mwenzake kama alivyokuwa kwa viongozi wengine katika ukanda huu na duniani kwa ujumla.  “Yeye na mimi tulipatana sana kama ilivyo kawaida kwa viongozi wa nchi mbili rafiki na majirani, siku zote tulikuwa tunawasiliana na kila mara kulipotokea jambo linalotuhusu sote tulishauriana na kwa kweli utamaduni huu ulikwenda vizuri kwa faida ya nchi zetu mbili” amesema na kumuelezea kuwa alikuwa kiongozi wa kutumainiwa na rafiki mkubwa kwa Watanzania, nchi jirani Afrika na dunia kwa ujumla na kwamba Tanzania na bara la Afrika limepoteza mtu muhimu”.  Rais Kikwete amesema viongozi na waombolezaji wamekuja kutoka karibu na mbali na Zambia kuja kuwafariji wa Zambia na kumshukuru Mungu kwa maisha na aliyomjalia Mwanawasa.

  Premi Kibanga,

  Lusaka, Zambia  03 September, 2008


  Are they serious au tuseme wamepitwa tu?(inadvertence)​
   
 2. D

  DAR si LAMU JF-Expert Member

  #2
  Sep 4, 2008
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 2,942
  Likes Received: 286
  Trophy Points: 180
 3. Kipunguni

  Kipunguni Senior Member

  #3
  Sep 5, 2008
  Joined: Jun 20, 2008
  Messages: 151
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Jamaa wa Ikulu wanadai kwamba hiyo ya yahoo inapatikana kirahisi wakati wowote na wakiwa mahali popote duniani.
   
 4. The Invincible

  The Invincible JF-Expert Member

  #4
  Sep 5, 2008
  Joined: May 6, 2006
  Messages: 4,722
  Likes Received: 1,212
  Trophy Points: 280
  Ikulu hawana website inayofanya kazi. Game theory amewalalamikia sana kwa hili.

  Kuna wakati ndugu Ansbert Ngurumo aliwahi kummwagia misifa kibao Salva Rweyemamu. Kwamba he is professional; na anaijua kazi yake. Sijui hasa alichomaanisha. Lakini kwa mwendo wa mambo mpaka sasa, hii kurugenzi ya mawasiliano Ikulu ni sifuri, tena yenye masikio.

  Anuani ya barua pepe ndiyo hiyo ya yahoo. Aibuuuu!
   
 5. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #5
  Sep 5, 2008
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,855
  Likes Received: 2,430
  Trophy Points: 280
  huyu ahsante uchafuzi...salva rweyemamu....ambaye mnasikia mkewe alikuwa amejilipua uk..kama mkimbizi wa rwanda[enzi jamaa akiwa rai......hajakamata channel]..hivi huyo mkeo ameshaukana ukimbizi na kurejelea uraia wa tanzania...nashangaa hata kama salva alifaulu vipi vetting ya usalama kwa kazi hii kubwa..anyway...

  ...serikali upande wa mwasiliano inatia aibu hata ile website ya maoni aliyoagiza pale maelezo haifanyi kazi..na tunaambiwa alijetengeneza ile website ameshalipwa milioni zaidi ya 200!!!!!

  tovuti ya serikali haiwi updated ..

  juzi nimeangalia international tender ya ku run uwanja wa taifa ....kutoka wizara ya habari,utamaduni na michezo..wizara ya hao maelezo........correspondence inaonyesha ukitaka maelekezo andika michezo@yahoo.com...nikasema du aibu...serikali inashindwa ku host.........haya!
   
 6. C

  Chuma JF-Expert Member

  #6
  Sep 5, 2008
  Joined: Dec 25, 2006
  Messages: 1,330
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Uliwauliza au Mbwembe zako?
   
 7. C

  Chuma JF-Expert Member

  #7
  Sep 5, 2008
  Joined: Dec 25, 2006
  Messages: 1,330
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  IT bado ipo nyuma sana hapa Home...lWazee wetu ukiwaambia unasoma Computer tu....wanafikiri wewe unasomea Ufundi/technician....Ukubwa wa IT wengi hawaujui...lkn inapofanya serikali inakuwa AIBU....mie naona hapa watu wa kwanza kulaumiwa ni TCRA....nafikiri kwa role yao wanatakiwa kuangalia kama kila wizara au idara ya serikali inaperfom...

  either kuna watu wazembe au mafisadi au whatever .......
   
 8. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #8
  Sep 5, 2008
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 864
  Trophy Points: 280
  Waache ushamba hawa,

  Kwani wanataka kusema kuwa ikulu.go.tz haipatikani sehemu nyingine duniani? Je wao wana mtandao wao peke yao unaopatikana wakiwa Tanzania tu? Mbona hawana server yao dedicated, badala yake domain ya ikulu.go.tz inatumia server za UK-Intelsat zilizoko Uingereza?
   
 9. S

  S. S. Phares JF-Expert Member

  #9
  Sep 5, 2008
  Joined: Nov 27, 2006
  Messages: 2,141
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0

  Duh...hivi huko Ikulu kuna watu wamesoma IT kweli??

  Mbona tunatia aibu namna hii.?
   
 10. Insurgent

  Insurgent JF-Expert Member

  #10
  Sep 5, 2008
  Joined: Jun 26, 2007
  Messages: 469
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Its a shame! There is no defence to this!!
  ERB wana IT Engineers wa kutosha wanaoweza kuisaidia ikulu katika kuweka/kuhost domain yao wenyewe.

  Wazi IT wa Ikulu hawako serious!
   
 11. M

  MpiganajiNambaMoja Member

  #11
  Sep 5, 2008
  Joined: Sep 20, 2007
  Messages: 69
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tatizo la Serikali yetu haijaichukulia IT kwa uzito unao stahili. Mimi ninavyojua katika taasisi kuna kuwa na IT Department ambayo ndo inashughulikia mambo yote ya Tekinolojia. Sasa mmeona ikulu wa IT department? Zunguka kwenye Wizara zote except fedha na utumishi hautakuta IT Department.

  Nchi nyingine kama Botswana na nchi za ulaya wana mtu/ofisi ya Chief Information Office or Chief Information Technology Officer ambaye kazi yake na majukumu yake ni kuratibu shughuli zote za IT serikalini.

  Hapa kwenu tunajiendea tu, kila mtu anafanya anavyojisikia hakuna utaratibu.

  Mara nyingi Non IT people wanaona IT kana ni internet tu (website na email). Hivyo kutoona haja ya kuwa na proper IT management kwenye taasisi zao.

  TCRA wao ni regulatory authority ya communication (Data communication), hivyo hawausiki na IT za maofisini au website. Kazi yao wanaifanya vizuri na hawastahili kulaumiwa kwa hili.
   
 12. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #12
  Sep 5, 2008
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Labda watu wa IT wakipewa visafari safari vya mikoani na Ughaibuni watachangamka.
  Unajua tena Bongo ukiwa na kazi kwenye ofisi yenye jina na huna visafari njaa.
  Lakini kikubwa ni kwamba Fungu la Internet Wamelibananga kwa kujenga vibanda na kununua Toyota Kitchen Part kwa wake zao.
   
 13. M

  Mwikimbi JF-Expert Member

  #13
  Sep 5, 2008
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,745
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  kuna tofauti kubwa kati ya wahitimu waliohitimu kuanzia 1993 and backwards, wakati ule computer tulisoma cobol, pascal, na ... kwenye madaftari, computer kama pale uclas zilikuwa mbili tu, university of dsm zilikuwa si zaidi ya 8 kwa wanafunzi wote hao

  sasa kama mtu alihitimu wakati huo na hataki kujua IT inavyokuwa na serikali bado inamweka nafasi nyeti kama ikulu kwa kuwa ni mwenzetu atatupamba ndo matokeo yake.

  mnadhani huyo salva angeweza kwenda pale ikulu bila baraka za fisadi lowasa? na huyo balile wa rai, anayeandika utumbo kila siku tunaambiwa masters yake alilipiwa ada na fisadi lowasa
   
 14. Pundit

  Pundit JF-Expert Member

  #14
  Sep 5, 2008
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 3,741
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Mimi nilipoisikia hii a while ago nilichoka.Vikampuni vidogo tu vinavyoelewa umuhimu wa image na privacy haviwezi kutoa business card yenye a yahoo email address, unaonekana tapeli usiyeweza kuwa hata na domain name/ SMTP server.

  Wakati wenzetu wanataka kuondoka kwenye ku route internet traffic zao Marekani, sisi tunatumia email ya Ikulu, sasa huku Bush akitumia "Patriot Act" na kuwabana watu wa Yahoo watoe nyeti zilizopo kwenye email ya Ikulu?

  Ona story hii kuhusu Yahoo China na privacy

  http://www.csmonitor.com/2006/0214/p01s04-usfp.html
   
 15. Kipunguni

  Kipunguni Senior Member

  #15
  Sep 5, 2008
  Joined: Jun 20, 2008
  Messages: 151
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Afisa mmoja wa Ikulu alinieleza hivyo.
   
 16. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #16
  Sep 5, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Kwanini watu wa JF tusijitolee kulipia Dedicated Server ya Ikulu kama mchango wetu?
   
 17. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #17
  Sep 5, 2008
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Jamani nitawamegea ninalolifahamu kuhusiana na mtandao wa Ikulu.

  Wakati P4 ilipoingia, mwenye kigoda alitaka iwe priority kuwa na website na communication center nzuri.

  Tatizo likaja pale Kallaghe alipoitisha mkutano wakakutana wajanja wakaunda kamati na tume, na tangu hapo imekuwa kasheshe.

  Muungwana on the otherhand, enjoyed the services of KikweteShein kutoka kwa Billy Mushi.

  Mvutano wa Ikulu website ni wa kisiasa na utendaji na kukosekana msukumo au utaalamu.

  Suggestion ilitolewa watafute independent parties, wafanye bid, kukaja mizengwe! kisha kukawa na vikao kibao, kutoka Ofisi ya Raisi, Usalama wa Taifa, Wizara za nchi, na utitiri mwingine ambao uko chini ya jina Ikulu, kila mtu akitaka atoe mawazo na mambo yake jinsi gani webite iendeshwe na idara na wizara gani ziwemo kwenye Ikulu.go.tz!

  So as of today, almost 3 years, Ikulu as entity is still devided on the whole website issue! It is not about money, but failure to undestand the whole website concept na wamekutana wajanja wengi!
   
 18. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #18
  Sep 5, 2008
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Rev,
  Yaani naamini hata Shy pamoja na u-controversy wake bado angeweza kuwasaidia katika hili - wamlishe kiapo tu cha kutunza siri za serikali na kumpa budget ya 30million tshs, am sure he'll handle that! Tatizo lao kama unavyo point ni upuuzi wa kutaka 10% katika kila aina ya project hapa Tanzania. They totally forget kuwa kuna pahala katika ulimwengu wa sasa commissions hazina upenyo. Inatia aibu kwa kweli, hata mimi hapa ninatumia SteveD(at)Jamiiforums.com, sembuse civil servants kwenye idara maalum serikalini, particularly Ikulu!!

  Hao unaosema "wajanja wengi" ni more or less kuwa ni "wapuuzi" machoni pa watu wenye kujali maendeleo ya nchi yao, haswa pale kipimo hicho kinapolinganishwa na strategic nature and necessity ya Ikulu kujiendeshea vitu kama email servers wenyewe.


  Mkjj,

  Hii ni changamoto kubwa. Lakini ningeikubali tu kama kweli kufanya hivyo kungelitokana na umasikini wa kupindukia kiasi kwamba Serikali yetu isihimu kulipia mail server. Ukumbuke kuwa kuna bajeti imetengwa na kutumika katika hili tayari. Wahusika katika hili swala wamekosa mwelekeo na malengo. It's a 3 weeks project. Kitu ambacho kinaweza kumudiwa na kikampuni kidogo tu, IKULU inashindwa kukimudu. Sorry for harsh words, lakini hii haina neno jingine bali ni "upumbavu!"


  Pundit,
  Hilo la ku-route internet traffic nchi nyingi za Africa bado zinasumbuka nalo, and i can forgive them since it's an infrastructural expensive feat. Lakini hili la webmail server... no no no; nothing short of outright disgrace. Kumbuka Hotmail/Yahoo gateways si kwamba ziko America tu, bali some are situated within Africa na kwingineko ambako Tanzania inaweza kuwa ina mambo fulani ambayo inasimama against nchi hiyo, hivyo inaweza ku-access correspondence kama hizo at will wakiamua.

  Unajua nini... mara nyingi tunaongea kwa kukosoa hapa JF, lakini lengo letu tuliowengi si kukosoa tu, bali kupata solution za matatizo yetu hapa nchini. It's simply an instinctual tone we use when writing. Itakuwa jambo la busara kweli kama wahusika katika idara za serikali watajiandikisha hapa na kuestablish mawasiliano ili wale wenye kuweza kusaidia walau kwa kutoa mawazo tuweze kufanya hivyo. It won't cost an arm and a leg to set a secure mail server for Ikulu.

  SteveD.
   
 19. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #19
  Sep 5, 2008
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Hamna lolote mimi hii namrushia the failed guy JK maana alituahidi kwenye kampeni kwamba kutakuwa na E-Govt. Aulizwe iko wapi so far?????????? Hv mnajua viongozi wetu walio wengi wanaona hiyo yahoo wala haina noma na ok wht else tanzania iko juu kiteknolojia bwana!!!!!!!!!!, Well acha hiyo kuna vitengo kibao pale mlimani vinatumia hizo yahoo, hotmail, gmail etc. ni kichefuchefu..........

  Hivyo basi mimi nawashaurini ndugu zangu tusiwashangae bali tuwaambie kwamba that is not proper I am more than 90% sure hawaoni walakuhisi au kujua implication ya hiyo domain.....
   
 20. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #20
  Sep 5, 2008
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Hamna lolote mimi hii namrushia the failed guy JK maana alituahidi kwenye kampeni kwamba kutakuwa na E-Govt. Aulizwe iko wapi so far?????????? Hv mnajua viongozi wetu walio wengi wanaona hiyo yahoo wala haina noma na ok wht else tanzania iko juu kiteknolojia bwana!!!!!!!!!!, Well acha hiyo kuna vitengo kibao pale mlimani vinatumia hizo yahoo, hotmail, gmail etc. ni kichefuchefu..........

  Hivyo basi mimi nawashaurini ndugu zangu tusiwashangae bali tuwaambie kwamba that is not proper I am more than 90% sure hawaoni wala kuhisi au kujua implication ya hiyo domain.....
   
Loading...