Spika Ndugai awashukia wasomi nchini, asema anajua watamshambulia katika mitandao

mshale21

JF-Expert Member
Apr 8, 2021
2,050
4,903
Spika wa Bunge Job Ndugai amesema anakerwa na kada nne ambazo zinatukuza usomi wao mbele ya Watanzania wasiopenda kujikweza.

Amezitaja kada hizo ni wahasibu, wahandisi, mawakili na madaktari wa kusomea ambao amesema kila mtu anataka kuanza na kutukuza kisomo chake wakati si lazima iwe hivyo.

Spika Ndugai ametoa kauli hiyo leo, Jumatano, Septemba 1, 2021 bungeni katika kipindi cha mjadala wa hoja za wabunge kuhusu muswada wa mabadiliko ya sheria mbalimbali uliowasilishwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Profesa Adelardus Kilangi.

Amesema anajua atashambuliwa na mawakili mitandaoni lakini anataka kujua iwapo hawaoni aibu kujiita ni wasomi wakati nchi ina wasomi wengine.

“Najua watanishambulia katika mitandao, ..ah lakini huo ndiyo ukweli nani asiyekuwa msomi katika nchi hii, au wengine hawajasoma, kwani hamuoni aibu fulani hivi kujiita wasomi wakati kuna wengine katika nchi hii wamesoma,” amehoji Ndugai.

Spika amesema; “kuna wakati nitahitaji mnishauri kuhusu hili la wanasheria kujiita wakili msomi, huu ni utaratibu fulani ulioanzishwa na wenzetu Waingereza wa kutukuza baadhi ya kada,’’

Ndugai amezitaja kada nne zinazompa shida na anawashangaa kuona wakitukuzwa kuliko wengine licha ya wengi kuwa ni wasomi.

Kada hizo ni wahasibu, wahandisi, mawakili na madaktari wa kusomea ambao amesema kila mtu anataka kuanza na kutukuza kisomo chake wakati siyo lazima iwe hivyo.

Kuhusu mawakili amehoji kama wakibaki na neno la wakili watapungukiwa kitu gani huku akiweka wazi kuwa neno msomi linawaongezea kitu gani kwa Watanzania wasiopenda kujikweza katika mambo mengine.

Kwa kada alizozitaja Spika, mawakili hujiita wakili msomi, wahasibu hupenda kuanza na neno CPA, wahandisi hutumia neno la ‘Engineer’ na waliosoma shahada za uzamivu (PhD) majina yao huanza na neno Dk

spikapic.jpg
 
Jamaa sijui Ana akili gani. Alichukia Assad kuitwa Prof akadai huko nje mtu anaitwa jinale bila Ilo la usomi.

Ana wivu Sana. Aliumia manager wa tarura kulipwa kuliko mkurugenzi.

Yeye anajua kusoma kuwa mhandisi unajenga daraja ama ghorofa watu wanaishi halianguki, ama daktari anakupasua anakutoa figo yako anaweka nyingine anadhani kuwa ni sawa kusoma socialogy, ama community development.

Haya udaktari wa kusomea anajua mtu ameusotea miaka mingapi, amehaso kinouma Sana.

Ila huyu jamaa hajui mziki uliopo wa hizo fani.

Hiyo CPA inamuumiza kichwa atakuwa ameshindwa kuipata.

Ngoja nigugo elimu yake niione alisomea Nini.

Yaani mpaka ameshindwa kazi iliyompeleka huko.

So anaumia dkt. Tulia kumzidi so anataka alingane naye.

Yaani binadamu anaonekana anaumia Sana na nonsenses
 
Spika wa Bunge Job Ndugai amesema anakerwa na kada nne ambazo zinatukuza usomi wao mbele ya Watanzania wasiopenda kujikweza.

Wahandisi wamefanya nini tena?
 
Ukisikia kudemka ndio huko, wao wanavyoitanaga waheshimiwa anajisikiaje? Au naibu speaker anapokuwa akiitwa Dr na yeye speaker hajafikia heshima hiyo kwani anajisikiaga vipi atuambie kwanza?

Nasema mimi nina wasiwasi na chanjo aliyochanjwa huyu kiumbe. Kuna miili mingine inakataa chanjo asiwe akawa naye ni muhanga wa hilitutaona vituko vingi sana hapa nchini.

Madhara ya kuchanjwa kwa pupa
 
Jamaa sijui Ana akili gani. Alichukia Assad kuitwa Prof akadai huko nje mtu anaitwa jinale bila Ilo la usomi.

Ana wivu Sana. Aliumia manager wa tarura kulipwa kuliko mkurugenzi.

Yeye anajua kusoma kuwa mhandisi unajenga daraja ama ghorofa watu wanaishi halianguki, ama daktari anakupasua anakutoa figo yako anaweka nyingine anadhani kuwa ni sawa kusoma socialogy, ama community development.

Haya udaktari wa kusomea anajua mtu ameusotea miaka mingapi, amehaso kinouma Sana.

Ila huyu jamaa hajui mziki uliopo wa hizo fani.

Hiyo CPA inamuumiza kichwa atakuwa ameshindwa kuipata.

Ngoja nigugo elimu yake niione alisomea Nini.

Yaani mpaka ameshindwa kazi iliyompeleka huko.

So anaumia dkt. Tulia kumzidi so anataka alingane naye.

Yaani binadamu anaonekana anaumia Sana na nonsenses
Pata juice upumzike mkuu, acha kuumiza akili yako kwa kile kimeo Cha Dodoma! Kinamind vitu vya kijinga, eti neno wakili msomi linamuumiza. Kimeo kweli.
 
Eti wasomi kujikweza? Mbona yeye na Wabunge wenzake wanajikweza kwa kujiita "Waheshimiwa"?

Hivi kila Mtanzania hapaswi kuwa "mheshimiwa"? Kwamba kuna kundi dogo linaloheshimiwa na wengi ambao ndiyo wapiga kura wasioheshimiwa??

Ndugai wewe ni mnafiki kabisa.
Ubunge ni heshima kwa wabunge na ipo duniani kote.

Ila hakupaswa kusema mambo alosema ndani ya bunge, alipaswa kuzungumzia kwenye baa sehemu kama Mahomanyika Nzuguni.
 
Yaani icho kinamkera speaker mpaka anakiongea bungeni? Natamani kujua yeye alisomea nini.

Tusidanganyane, degree na vyuo havina thamani sawa kwenye soko la ajira na ata perception ya jamii.

Btw umegundua fani zote alizozitaja unahitaji leseni kupractice legally baada ya kupata degree yako.
 
Mbona hujahoji wabunge, ukiwemo wewe, bila kutanguliza neno 'mheshimiwa' hapakaliki? Unajua ni muda gani unapotea kwa kurudia hilo neno kila atajwapo yeyote alie mbunge? Ni muda gani unapotea isomwapo budget au hotuba yoyote bungeni ambamo mstari kulikosa neno 'mheshimiwa' ni aghalabu? Kuna taaluma nne mama hapa dunia: Waalimu, wahandisi, tabibu.

nawe malizia moja iliobaki. Sio wanapenda kujiita hivyo, jamii inazaliwa inawakuta.
 
Back
Top Bottom