Chachu Ombara
JF-Expert Member
- Dec 11, 2012
- 6,042
- 10,787
Mmiliki wa shule ya Lucky Vincent Arusha na Makamu Mkuu wa shule hiyo, wamefikishwa Mahakamani, wanakabiliwa na makosa matano.
MMILIKI wa shule ya Lucky Vicent iliyopo Kwa Morombo jijini hapa,Inosent Simon Moshi na makamu wake, Longino Vicent Mkama wamefikishwa mahakamani na kusomewa mashtaka matano ya uvunjivu wa sheria za usalama barabarani na kusababisha vifo vya wanafunzi 32, walimu wawili na dereva mmoja.
Akisoma mashtaka hayo mbele ya hakimu, Desdery Kamugisha wa mahakama ya hakimu mkazi Arusha, mwendesha mashitaka wa serikali, Rose Sulle aliieleza mahakama hiyo kwamba, washtakiwa hao walitenda makosa hayo Mei 6, mwaka huu katika eneo la Kwa Morombo jijini Arusha.
Alieleza kuwa mshitakiwa wa kwanza ambaye ni mmiliki wa shule hiyo anakabiliwa na makosa manne huku shtaka la tano likiwahusu washtakiwa wote wawili.
Kuhusu ajali ya wanafunzi wa Lucky Vincent, soma AJALI Karatu: Coaster yaua wanafunzi na walimu wa Lucky Vincent (karibu wote)
=====
UPDATES:
Korti ya Arusha yawaachia huru mmiliki wa shule ya Lucky Vincent Innocent Mosha na Makamu Mkuu Logino Vicenti kwa dhamana ya Sh15m kila mmoja.

Mkurugenzi Lucky Vincent jela miaka 4 na miezi sita
Mkurugenzi wa shule ya Lucky Vincent ,Inosent Moshi ametiwa hatiani na mahakama ya hakimu mkazi Arusha kwa kutenda makosa manne ya usalama barabarani na kutakiwa kwenda jela miaka minne na miezi sita ama kulipa faini ya sh,milioni 1.5. Mwingine aliyekumbwa na adhabu ni mwalimu mkuu msaidizi wa...
www.jamiiforums.com