Mmiliki wa Lake Priting auwawa kikatili jijini Mwanza

rweyy

JF-Expert Member
Aug 5, 2011
229
146
Mmiliki wa kiwanda cha karatasi Lake Priting maarufu kwa jina la mama Chande kauwawa na watu wanaosemekana majambazi jana jioni muda wa saa kumi nyumbani kwake maeneo ya Kauma. Majambazi walimuua na kuacha wamemfungia chumbani kwake, alikuwa hakiishi peke yake.

Mmoja wa wafanyakazi wake anasema bosi wake huyo hakuonekana kuanzia sa tisa unusu ilipofika saa 12 jioni ambapo sio kawaida alianza kupiga simu ikiita bila kujibiwa ilipo fika saa 2 usiku aliripoti polisi. Baada ya polisi kufika ndio walipo amua kuvunja mlango na kukuta marehemu kauwawa huku akiwa katobolewa macho na kuvunjwa mkono. Marehemu alikuwa hakiishi palepale kiwandani kwake kiwanda kikiwa chini yeye golofani.

R.I.P Mama chande
 
Japo amelazimishwa kutangulia mbele za haki, tunamuombea Mungu ampokee na kumsamehe makosa yake. RIP mama chande.
 
Duh! Ni dhahiri kabisa hilo tukio ni la njama kwa namna moja ama nyingine!
Mwanza sasa kunatisha kwa mauaji ya kikatili juzi tu RPC hivyo hivyo na tena hili Mmmmhh!

Lala kwa Amani yake Bwana wetu Mama Chande!
 
njama za kibiashara
polisi hapa wana kazi rahisi sana kuwadaka washindani wake
na kuangalia emai au sms communication within two weeks watajua nani mhusika
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom