TANZIA Mmiliki wa hoteli ya kitalii ya Snowcrest, William Mollel afariki

Cannabis

JF-Expert Member
Jan 20, 2014
8,938
25,281
Arusha. Mfanyabiashara maarufu jijini Arusha ambaye pia ni mmiliki wa hoteli kadhaa za kitalii , ikiwepo Snow crest , William Mollel amefariki Dunia baada ya kuugua kwa muda mfupi.

Akizungumza na mwananchi Mpwa wa mfanyanyabiasha huyo,Lemburis Sirikwa amesema Mollel amefariki Jana.

"Ni kweli Mollel ambaye ni mtoto wa dada yangu amefariki Jana baada ya kuugua kwa muda mfupi na taratibu za mazishi zinaendelea"

Amesema Mollel ambaye alikuwa akifanya biashara kadhaa ikiwepo ya kuendesha hoteli za kitalii ameacha watoto watatu.

Mwenyekiti wa chama cha wafanyabiashara ,Viwanda na Kilimo(TCCIA) Mkoa Arusha Walter Maeda alieleza pia kusikitishwa na kifo cha mfanyabiashara huyo.

Mollel alinunuwa hoteli hiyo, mwaka 2014 kutoka kwa mfanyabiashara Wilfred Tarimo, hata hivyo aliingia katika mgogoro wa kushindwa kuendesha hoteli kwa ufanisini kutokana na kurithi madeni mengi ya wazabuni na wafanyakazi.
Kwa mara ya mwisho kuzungumza na mwananchi kabla ya kifo chake alisema alinunua hoteli hiyo kwa mkopo wa dola 8 milioni kutoka benki ya PTA na na standard chartered.

"Nilitegemea baada ya kupata mkopo wa kununua hoteli hii niifanye ya kimataifa na kuunganisha na mtandao wa hoteli kubwa duniani''alisema.
Kifo cha Mollel kimetokea takribani mwezi miwili tangu kifo Jacob Ombay mmiliki mwingine wa hoteli nane za kitalii.

Ombay alikuwa anamiliki hoteli za Bougainvillea safari lodge, country lodge karatu,Ngorongoro coffee lodge, lake Eyasi safari lodge,Sangaiwe tented lodge, Thorn tree camp,Hippo Traill camp.
Katibu mtendaji wa chama cha mawakala wa utalii nchini-(TATO) Sirili Akko amesema vifo vya wafanyabiashara hao ni pigo Kwa sekta ya Utalii.

Chanzo: Gazeti la Mwananchi
 
Arusha. Mfanyabiashara maarufu jijini Arusha ambaye pia ni mmiliki wa hoteli kadhaa za kitalii , ikiwepo Snow crest , William Mollel amefariki Dunia baada ya kuugua kwa muda mfupi....
Nani yuko salama?

Huenda tukaamka wakati tutakuwa tumechelewa sana.

Wangapi wanao uwezo wa kufika huko nje kwa matibabu?

Miradi miradi ilikuwa priority juu ya maisha?
 
Tahadhari ni mhimu😁
Kifo hakina tahadhari usijifariji zikifika zimefika hazijui ulikuwa na tahadhari hukuwa na tahadhari chenyewe kikija kimekuja.
Leo hii hata ukinywa sumu tuseme siku zilifika? Umejinyonga tuseme zilifika?
Lkn sawa zilifika mkuu
 
Kifo hakina tahadhari usijifariji zikifika zimefika hazijui ulikuwa na tahadhari hukuwa na tahadhari chenyewe kikija kimekuja.
Acha kupotosha watu hapa. Kifo hakina tahadhari? Nenda basi kakatishe barabara bila tahadhari hutakufa. Fanya zinaa bila tahadhari kwani huwezi kufa. Katisha maeneo yenye vibaka usiku bila tahadhari hamna neno.
 
Arusha. Mfanyabiashara maarufu jijini Arusha ambaye pia ni mmiliki wa hoteli kadhaa za kitalii , ikiwepo Snow crest , William Mollel amefariki Dunia baada ya kuugua kwa muda mfupi.

Akizungumza na mwananchi Mpwa wa mfanyanyabiasha huyo,Lemburis Sirikwa amesema Mollel amefariki Jana.

"Ni kweli Mollel ambaye ni mtoto wa dada yangu amefariki Jana baada ya kuugua kwa muda mfupi na taratibu za mazishi zinaendelea"amesema

Amesema Mollel ambaye alikuwa akifanya biashara kadhaa ikiwepo ya kuendesha hoteli za kitalii ameacha watoto watatu.

Mwenyekiti wa chama cha wafanyabiashara ,Viwanda na Kilimo(TCCIA) Mkoa Arusha Walter Maeda alieleza pia kusikitishwa na kifo cha mfanyabiashara huyo.

Mollel alinunuwa hoteli hiyo, mwaka 2014 kutoka kwa mfanyabiashara Wilfred Tarimo, hata hivyo aliingia katika mgogoro wa kushindwa kuendesha hoteli kwa ufanisini kutokana na kurithi madeni mengi ya wazabuni na wafanyakazi.

Kwa mara ya mwisho kuzungumza na mwananchi kabla ya kifo chake alisema alinunua hoteli hiyo kwa mkopo wa dola 8 milioni kutoka benki ya PTA na na standard chartered.

"Nilitegemea baada ya kupata mkopo wa kununua hoteli hii niifanye ya kimataifa na kuunganisha na mtandao wa hoteli kubwa duniani''alisema.

Kifo cha Mollel kimetokea takribani mwezi miwili tangu kifo Jacob Ombay mmiliki mwingine wa hoteli nane za kitalii.

Ombay alikuwa anamiliki hoteli za Bougainvillea safari lodge, country lodge karatu,Ngorongoro coffee lodge, lake Eyasi safari lodge,Sangaiwe tented lodge, Thorn tree camp,Hippo Traill camp.

Katibu mtendaji wa chama cha mawakala wa utalii nchini-(TATO) Sirili Akko amesema vifo vya wafanyabiashara hao ni pigo Kwa sekta ya Utalii.
afariki-pic-data.jpg
 
Nani yuko salama?

Huenda tukaamka wakati tutakuwa tumechelewa sana.

Wangapi wanao uwezo wa kufika huko nje kwa matibabu?

Miradi miradi ilikuwa priority juu ya maisha?
Kabla ya miradi hapakuwepo na vifo, kufa ni sifa ya kiumbe chochote kilicho hai!
 
Kabla ya miradi hakukuwa wala Corona na vifo hivi vinavyoweza kuzuilika. Yasemekana hii ni habari mbaya sana kwenu:

RIP Mollel

Wito wangu kwa baadhi ya Wafuasi wa Chadema, haipendezi kuombeana vifo, sisi sote ni watanzania na wanaofariki ni Watanzania wenzetu yaani ndugu zetu, majirani na jamaa zetu

Hvyo si busara kila mara kupost taarifa zenye viasharia vya kushabikia vifo au kuombea vifo kwa Watanzania wenzetu,,, tukumbuke tu SISI SOTE NI NDUGU
 
Hizi ni nyakati za mashaka kila nafsi imejaa hofu na sintofahamu akili zetu zimegota. wanaopaswa kuchukua hatua wametuacha mithili ya kuku aliyekatwa kichwa, ni kama tupo kwenye gereza la waliohukumiwa vifo na kila mmoja ananyongwa kwa wakati wake.

Ni kweli yana mwisho lakini sijui huo mwisho tutabaki wangapi?

Tumaini letu ni Mungu pekee.
 
RIP Mollel

Wito wangu kwa baadhi ya Wafuasi wa Chadema, haipendezi kuombeana vifo, sisi sote ni watanzania na wanaofariki ni Watanzania wenzetu yaani ndugu zetu, majirani na jamaa zetu

Hvyo si busara kila mara kupost taarifa zenye viasharia vya kushabikia vifo au kuombea vifo kwa Watanzania wenzetu,,, tukumbuke tu SISI SOTE NI NDUGU
Siasa ndio imetufikisha hapa...siasa imefunga akili za watu....
 
Back
Top Bottom