Mmiliki wa gari aliyopata ajali marehemu Sharo Millionea ajitokeza na kusema haidai chochote familia

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,780
MMILIKI WA GARI ALIYOPATA AJALI MAREHEMU SHARO MILLIONEA AJITOKEZA na KUSEMA HAIDAI CHOCHOTE FAMILIA YA MAREHEMU

015.JPG

MMILIKI wa gari ambalo lilikuwa likiendeshwa na msanii maarufu nchini, Hussein Ramadhan ‘Sharo Milionea' na kupata nalo ajali iliyosababisha kifo chake huko Muheza, Tanga, Mohammed Ismaili maarufu kwa jina la Mudi Suma, ameibuka na kueleza uhusiano wake na marehemu, huku akisema amekubali hasara.Akizungumza kwa simu kutoka Muheza jana Suma alisema hana mpango wa kudai fidia au kupeleka malalamiko yoyote kwa ndugu wa marehemu kwa kuwa; "Kilichotokea ni kazi ya Mungu." "Siwezi kudai hata kidogo hivyo ni vitu vya kupita tu.

Marehemu alikuwa ni zaidi ya ndugu yangu, gari ni kitu kidogo sana katika uhusiano tuliokuwa nao," alisema Suma na kuongeza kwamba hata Marehemu Sharo Milionea naye alikuwa amemwachia mali zake kadhaa ikiwamo gari. "Siyo gari tu alilokuwa ameniachia. Kuna mikataba yake ya kazi, Bajaji yake na funguo za chumbani kwake. Nasubiri kukabidhi vitu hivyo baada ya kukaa na ndugu zake. Vitu viko kwenye mikono salama," alisema.

Kuhusu gari lake lililopata ajali, Suma alisema lilikuwa na bima ndogo, lakini anapanga kwenda TRA atakaporejea Dar es Salaam kufuatilia baadhi ya mambo.

"Kabla ya kuondoka bima ile kubwa ilikuwa imekwisha kwa hiyo nikaamua kuikatia bima ndogo. Nitakapofika kesho (leo) Dar es Salaam, nategemea kwenda ofisi za bima kuzungumza nao," alisema Suma. Alipoulizwa kama kuna mtu mwingine atakayeathirika kutokana na gari hilo kuharibika katika ajali mbali na yeye, alijibu: "Hakuna tofauti na mimi mwenyewe na familia yangu."

Kabla ya ajali.
Suma alieleza kuwa kabla ya kuanza safiri yake, Sharo Milionea alifika nyumbani kwake mchana na kumweleza kuwa afya yake haikuwa nzuri. "Kabla ya kuondoka aliniambia kuwa hajielewi elewi na kifua kilikuwa kinambana. Nikamshauri asiondoke peke yake, atafute mtu wa kuondoka naye ambaye atamsaidia kuendesha gari njiani," alisema Suma na kuongeza:

"Tulianza kuwapigia simu jamaa zetu wanne wa kusafiri naye lakini kila tuliyemwambia hakuwa tayari. Ilikuwa ni changamoto mpaka ilipofika saa 10:45 hivi jioni, akaamua kuondoka peke yake. Wakati anatoa gari getini kwangu, nikamwambia, basi jaribu kuwa mwangalifu sana, maana alikuwa kweli anasumbuliwa na kifua. Tukakubaliana kwamba atakaporudi aende hospitali kucheki afya yake."

Kuhusu uhusiano wake na marehemu, Suma alisema: "Mimi ni mfanyabiashara na yeye alikuwa msanii, lakini ilitokea tukawa marafiki sana mpaka ikafikia wakati nikaona kuwa ni ndugu yangu. Nilimwamini nikamtambua kama sehemu ya familia."

Alisema marehemu alikuwa akitumia gari hilo kila alipolihitaji na safari ya kwenda nalo Tanga kwa wazazi wake ilikuwa ni ya tatu."Siyo mara ya kwanza kuitumia gari lile, nilikuwa nimemwamini sana. Safari ya kwanza alichukua na kusafiri nalo mwenyewe, halafu safari ya pili ikafuata na hii ilikuwa safari ya tatu," alisema Suma.

Eneo la ajali wakimbia makazi Baadhi ya wakazi wa Kijiji cha Songa Kibaoni mahala ambako Sharo Milionea alipatia ajali, wamezikimbia nyumba zao baada ya Mkuu wa Wilaya ya Muheza, Subira Mgalu kutoa siku moja kwa waliopora mali za marehemu huyo kuzisalimisha mara moja.

Kwa hisani ya Habari na Matukio Blog
 
MKATA KIU

JF-Expert Member
Nov 22, 2010
2,348
3,229
Yes that's brotherhood, gari ya sharo millionea ni Toyota Opa ambayo wa safari za kijijini haifai as ipo chini sana...

So as brothers mnasaidiana as anakwenda kwa mama na mazaga zaga kama una gari ya juu huitumiii unamwachia jamaa apande nayo as vijijini barabara sio nzuri kwa gari za chini...

hata ningekuwa mimi hapo Gari huwez liwaza ni kitu kidogo sana as ukilinganisha na kumpoteza rafiki yako mnaependana..

I real miss you sharo millionea especially kila nikilisikia neno meeen
 
Kiranga

Platinum Member
Jan 29, 2009
60,394
74,458
Debonair.

Mara nyingine paranoia ninayoona kwa wenzetu wa nchi zilizoendelea inalipa. Mtu akiwa na kiugonjwa kidogo tu anaweza kuahirisha safari.
 
Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
90,740
104,888
Debonair.

Mara nyingine paranoia ninayoona kwa wenzetu wa nchi zilizoendelea inalipa. Mtu akiwa na kiugonjwa kidogo tu anaweza kuahirisha safari.

The thing is, if it's your day it's your day! Unaweza kweli kuahirisha na ukafia nyumbani vilevile.
 
Kiranga

Platinum Member
Jan 29, 2009
60,394
74,458
The thing is, if it's your day it's your day! Unaweza kweli kuahirisha na ukafia nyumbani vilevile.

The whole "your day" philosophy is full of predestination, like life is predetermined and everyone has an appointed day, that is fixed.

While the truth seem to be more like everything is flexible. Take good care of yourself and you icrease the chance of a good, long life.

Jump in front of a moving train and you make today your day, not that it will stop certain individuals from saying that that was your day anyway.

Bottom line, this "your day" philosophy is rather religious and irresponsibly so might I add.

Too passive and may encourage recklessness.

Mwisho watu watasema hamna haja ya kufunga mkanda, if it's your day it's your day. Hamna haja ya kuvaa mpira, if it's your day utaupata hata kwa kinyozi.

You see what I mean?

In any case, whether "your day" theory is right or wrong. I would feel comfortable dying after exhausting and taking care of all the possible causes of death that are practically exhaustible, knowing that death was not easily preventable, than dying because I stubbornly wanted to drive while sick, or just couldn't be bothered to buckle up.
 
Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
90,740
104,888
The whole "your day" philosophy is full of predestination, like life is predetermined and everyone has an appointed day, that is fixed.

While the truth seem to be more like everything is flexible. Take good care of yourself and you icrease the chance of a good, long life.

Jump in front of a moving train and you make today your day, not that it will stop certain individuals from saying that that was your day anyway.

Bottom line, this "your day" philosophy is rather religious and irresponsibly so might I add.

Too passive and may encourage recklessness.

Mwisho watu watasema hamna haja ya kufunga mkanda, if it's your day it's your day. Hamna haja ya kuvaa mpira, if it's your day utaupata hata kwa kinyozi.

You see what I mean?

I see what you mean but at the end of the day we are all going to die and (perhaps) besides those on death row, none of us know exactly when and how we gonna die.

Lakini hiyo haina maana kwamba watu waache kuwa waangalifu katika maisha yao.
 
Money Stunna

JF-Expert Member
Aug 9, 2011
13,054
6,202
mungu akubariki mkuu wewe kweli ulikuwa rafik wa sharo,mungu atakuongezea zaidi na zaidi,kama magari yapo mengi sana utapata zaidi,maombi yangu yapo kwako
 
Job K

JF-Expert Member
Oct 4, 2010
9,321
7,082
Hivi hii bima ndogo kazi yake nini sasa kama hakuna compensation yoyote

Wa-TZ bwana kila kitu kimjinimjini tu! Unakata bima ndogo ili iweje? Hiyo imekula kwake! Eti baada ya ajali ndo ukazungumze nao? Watakuelewa saa ngapi? Jamani tubadili mtazamo wetu (by Fifi).
 
Jodoki Kalimilo

JF-Expert Member
Feb 12, 2012
10,935
8,190
hapa naona itakua ni "third party only" (TPO) ambayo ina-cover hasara kama itampata mtu wa tatu au kitu kama vile nyumba etc.

Nimekupata mkuu ila huwa nashangaa huu utaratibu wa mtu akigongwa watu wanamalizana kwa kulipana kama indicator na vitu vingine wakati mashirika ya bima ndio kazi yake
 
Jodoki Kalimilo

JF-Expert Member
Feb 12, 2012
10,935
8,190
The thing is, if it's your day it's your day! Unaweza kweli kuahirisha na ukafia nyumbani vilevile.

Hizi kauli ni za kutiana moyo pindi matatizo yanapotupata na ni njia moja wapo ya kuonyesha kwamba kila mtu ana siku yake ya kufa na aina yake ya kifo (kiimani), lakini kwa upande mwingine huwa najiuliza mbona maeneo mengine duniani ambayo wanatii sheria na mamlaka mbalimbali za serikali huwa wanazuia mambo mengi ambayo huku kwetu huwa ni kawaida kutokea, nadhani tufuate tu kanuni mbalimbali za usalama hata kama if it's your day it's your day! maana huku kwetu maambukizi ya ngwengwe juu, ajali juu zingine zinazuilika though watz wengi tunajifariji ajali haina kinga alafu tunajifanya tunazijua dini kuliko waliozileta na kusema siku zake zimefika
 
Wi-Fi

JF-Expert Member
Aug 30, 2011
2,089
1,359
Nimekupata mkuu ila huwa nashangaa huu utaratibu wa mtu akigongwa watu wanamalizana kwa kulipana kama indicator na vitu vingine wakati mashirika ya bima ndio kazi yake

ni kweli kabisa, watu wengi wanakosa elimu ya bima ndio maana makampuni ya bima yanapata profit kubwa sana.
 
georgeallen

JF-Expert Member
Jun 3, 2011
3,780
1,250
ni kweli kabisa, watu wengi wanakosa elimu ya bima ndio maana makampuni ya bima yanapata profit kubwa sana.
mchakato wa kulipwa bima kwa vitu vidogo dogo ni kero. isitoshe kwenye bima kuna kitu inaitwa deductable na hasa kwenye madhara madogo madogo, hailipi kufuatilia kulipwa na bima.
 
Jodoki Kalimilo

JF-Expert Member
Feb 12, 2012
10,935
8,190
ni kweli kabisa, watu wengi wanakosa elimu ya bima ndio maana makampuni ya bima yanapata profit kubwa sana.

Alafu bima wala sio kubwa mfano kama bima ya nyumba au ajali unakuta ni 0.25% (sina uhakika sana lakini zinakuwa around hiyo figure) kitu ambacho unakuta nyumba ya 70 million unaweza lipa bima kama laki kwa mwaka lakini unakuta watu tunapata majanga kama kimbunga n.k tunabaki kuomba serikali wakati kazi ya serikali ni kuratibu shughuli mbalimbali though kwa upande mwingine ina jukumu la kuelimisha wananchi wake kujikinga na majanga. Nina imani tukizitumia hizi taasisi za bima kikamilifu hata gharama zingeshuka
 
Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
90,740
104,888
Hizi kauli ni za kutiana moyo pindi matatizo yanapotupata na ni njia moja wapo ya kuonyesha kwamba kila mtu ana siku yake ya kufa na aina yake ya kifo (kiimani), lakini kwa upande mwingine huwa najiuliza mbona maeneo mengine duniani ambayo wanatii sheria na mamlaka mbalimbali za serikali huwa wanazuia mambo mengi ambayo huku kwetu huwa ni kawaida kutokea, nadhani tufuate tu kanuni mbalimbali za usalama hata kama if it's your day it's your day! maana huku kwetu maambukizi ya ngwengwe juu, ajali juu zingine zinazuilika though watz wengi tunajifariji ajali haina kinga alafu tunajifanya tunazijua dini kuliko waliozileta na kusema siku zake zimefika

Hata huko kwingine nako wanakufa tena sana tu licha ya kutii sheria (ingawa si wote wanaotii sheria) na ndiyo maana kuna idioms kama "accidents will happen".

Kwa hiyo kama siku yako ya kufa imefika jua utakufa tu.

Death is no respecter of persons.
 
Thomas Odera

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
661
135
Pole kwa kufiwa na rafiki yako kipenzi na pia Mungu akujalie kwa kuwa na moyo wa huruma na utu
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

1 Reactions
Reply
Top Bottom