Mmiliki Palm Beach adai kumiliki kihalali eneo lake

mams

JF-Expert Member
Jul 19, 2009
614
30
Mmiliki wa eneo linalodaiwa kuwa la wazi Palm Beach, amekanusha kuvamia eneo hilo. Mmiliki huyo, Taher Muccadam, amesema anamiliki kiwanja hicho kihalali kwa mujibu wa taratibu za kisheria.
Muccadam aliwaambia waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam kuwa Mahakama Kuu, Kitengo cha Ardhi, iliamuru arejeshewe umiliki wake baada ya kufanya makubaliano ya nje ya mahakama kati yake na Manispaa ya Ilala.
“Baada ya kesi kukaa muda mrefu mahakamani, nilitumia uzalendo wangu bila kudai fidia ambayo nilistahili kulipwa dola milioni sita za Marekani kuanzia mwaka 2004 kesi ilipofunguliwa hadi mwaka jana tupofanya makubaliano ambapo mahakama iliamuru nirejeshewe eneo langu” alisema.
Alisema mbali na kusamehe fidia pia alipunguza sehemu ya eneo lake na kupisha barabara na kituo cha daladala.
Alisema kitendo cha Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo, Patrick Rutabanzibwa, kulishikia `bango' suala hilo na kusahau utawala wa sheria, ni kwenda kinyume na amri ya mahakama ambayo ni chombo huru.
Aidha, alisema kiongozi huyo kuingilia uhuru wa mahakama ni sawa na kurudisha nyuma mafanikio na maendeleo ya nchi kwa kudharau sheria za nchi na katiba.


CHANZO: NIPASHE 02/12/2010
 
0 Reactions
Reply
Top Bottom