Mmezoea vya kunyonga hamviwezi vya kuchinja. Hongera sana Halima Mdee na Makamanda wote kwa kugomea wito wa kienyejienyeji

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
121,665
2,000
Mkuu huyo jamaa humu kishajidharaulisha kuliko mwanachama yeyote aliyewahi kutokea hapa jamvini. Hawa ndiyo watu wanajiita wasomi lakini hawakuelimika hata chembe. Upuuzi wanaouandika ambao hauingii hata akilini unashangaza sana.


Kama Halima ni mwanasheria, alitakiwa kujua mwenye mamlaka ya kisheria ya kupeleka majina tume ya uchaguzi ni KM. Huu uzi unakuchoresha tu bro.
 

KISIWAGA

JF-Expert Member
Oct 22, 2015
4,158
2,000
Mkuu huyo jamaa humu kishajidharaulisha kuliko mwanachama yeyote aliyewahi kutokea hapa jamvini. Hawa ndiyo watu wanajiita wasomi lakini hawakuelimika hata chembe. Upuuzi wanaouandika ambao hauingii hata akilini unashangaza sana.
Huyu bwana tunachoweza kusema in kuwa kazeeka vibaya kama Lyatonga Mrema
 

vipik2

JF-Expert Member
Nov 24, 2011
2,513
2,000
Sasa aliyekuwa hawezi vya kuchinja kwa njia za kisheria ambazo Mungu amezileta na akakataza vya kunyonga ni nani?

Hebu niambie kati ya ccm na chadema juu ya msemo huo ni nani unamuhusu?

Uchaguzi mliuharibu kwasababu hamwezi vya kuchinja, mliuwa,kupora,kupora kura feki,kurq halali hamkuzihesabu. Wacha usengerema wako WA kinafiki wee kinaja.

Huyo kama aliwahi kusoma shule za boarding lazima waliharibu na matokeo yake ndio huko kubwabwaja
 

Samboko

JF-Expert Member
Oct 30, 2011
5,187
2,000
Kwa hili tukio lilivyochezwa kitoto na mfumo ingemchukua halima mdee miaka 100 kuitika wito wa kamati kuu...

Hua siamini kama kuna mtu na akili zake timamu anaamini lipo jambo limejificha hapa, hasa ukifikiri kwa kina kuhusu Nusrat kutolewa jela usiku.
 

mkulima gwakikolo

JF-Expert Member
Nov 22, 2014
1,193
2,000
Jambo la kwanza Chadema ilipaswa kwenda mahakamani kupinga Majina yaliyopelekwa na NEC na kujenga hoja ya kwamba kuna Udanganyifu uliofanyika.
Lengo ni kumpata mtu mmoja au wawili waliopeleka majina yale NEC.
Uchunguzi ungefanyika ili abainike aliyepeleka na kusaini yale majina.

Haiwezekani kuwa Wanawake 19 pamoja na aliyekua Gerezani wote walibeba barua na form zile kama Jeneza na kuzipeleka NEC.
Kama ni Mdee aliyepeleka awajibishwe peke yake na wengine wabaki kama Wabunge mana wameshaapishwa kuwawakilisha wananchi .

Chama kingeweza kikawatoa kwenye Nyadhafa zao zote na kuwakana kwa kutoshirikiana nao kwa namna yoyote lakini sio kuwavua uanachama.

Hakuna nchi yenye Demokrasia isiyokuwa na mgombea Binafsi.
Kuwaacha bila kuwafukuza kungemaanisha kwa vitendo kuwa Chadema ni Chama Cha Demokrasia na kinapigania Demokrasia ya kweli na Katiba mpya inayoruhusu mgombes binafsi.
Wangehojiwa kwa umakini bila kukurupuka kama Mnyika alivyofanya kuanza kuwakashifu na kuwafokea kwenye motandao kabla ya kuwasikiliza.
Baada ya kuhojiwa wangebaini nani hasa aliyefanya figisu zile na huyo angechukulwa hatua kali.
Wakina mama ndio watakaoijenga Chadema yenye Wanachama wenye kulipenda chama .
Mtoto akizaliwa akalelewa na mama anayeimba nyimbo za kukijenga chama na Demokrasia atakua na kuwa na imani na chaka hicho. Kuwatisha wanawake na kuwafukuza bila kujali mazuri waliyoyafanya ndani ya chama hicho ni kujenga Udikteta wa viongozi wanaojiona ni miungu watu.
Tunasema kila siku Mkuu wa nchi apunguziwe madaraka ili asiwe mungu mtu lakini cha ajabu tunajenga vyama vyenye kiungu watu huku wakiwa wanawatawala wanachama wao kwa kujenga hofu na kutaka waheshimiwe na kutukuzwa kwa gharama za kuwaumiza wengine.

Jengeni Chama Chenye dira tofauti kabisa na CCM.

Tujiiulize wote, hivi wale akina mama walipewa nafasi ya kukaa kama jumuiya na kutoa maoni yao kisha kuamua kidemokrasia kwa kupiga kura ya kukubali au kukataa kupeleka majina ya Viti maalumu Bungeni!?
Jibu ni hapana!
Wanawake wale walikua wanalazimishwa kukubaliana na matakwa ya wanaume ambao hawana hizo nafasi na haziwahusu.
Ni nafasi kwa ajili ya wanawake ili kujenga jamii yenye akina mama jasiri watakaowalea watoto wetu na kuondoa mfumo dume unaowafanya wanawake wawe kama bidhaa ya kuwatumiwa na wanaume wenye madaraka.

Tuwape ruhusa hao akina mama wakate rufaa ndani ya chama kisha waondolewe nyadhifa zao lakini wasifukuzwe.
Historia itashindwa kutofutosha kati ya utendaji wa serikali ya CCM katika maamuzi na utendaji wa viongozi wa Chadema katika maamuzi.

Kama utendaji wa na maamuzi yasiyojali kanuni za kutoa haki yanayofanywa na mwenyekiti Mbowe ni muhimu na wapambe wake wanayafurahiya na kuyasifia basi hata Mwenyekiti wa CCM na Rais wa nchi anafanya vizuri bila kujali Uhuru wa kujieleza,kusikilizwa,kutendewa kwa utu na kuheshimu haki za watu katika ujenzi wa nchi.

Haramu iwe ni haramu bila kujali ikefanywa na nani?

Cha ajabu Mbowe na Mnyika wakifanya Ubabe wanatukuzwa na kushangiliwa na kuitwa mwamba lakini Magufuli akitoa maamuzi magumu anatukanwa na kutangazwa dunia nzima kuwa ni dikteta na mbabe.
Tujiulize tunafanya nini na tunataka nini?
Yote maswali yako hayana mana mpaka pale utazingatia katiba inasema nini kuhusu vitimaalum,mimi nashindwa kuelewa mtu msomi anaweka paragraph nyingi akiongelea upuuzi Bila rejea ya misingi ya katiba ya nchi,vyama husika nk.yaani niwe msomi nikubali na kutetea upuuzi uliofanyika kwa Akina Mdee?ntakua nmesoma mwezini ama wapi??

Sent from my SM-G920F using JamiiForums mobile app
 

trachomatis

JF-Expert Member
Jun 7, 2011
3,752
2,000
Ndiyo hapo Sasa... Bora uwe na misimamo yako,ila usijionyeshe wazi uko upande mmoja... Sasa nchi yetu itakuwa inachekesha,waandishi wanatakiwa watunze kumbukumbu hizi za era ambayo katiba haikuwahi kuonekana ipo. Wabunge wanafutwa uanachama,bado wanaendelea na ubunge, mf. Mwambe wa Ndanda. Mtu kutolewa rumande jioni ili awahi shughuli ya kuapishwa bungeni kesho yake... Na mengine kibao...!
Yote maswali yako hayana mana mpaka pale utazingatia katiba inasema nini kuhusu vitimaalum,mimi nashindwa kuelewa mtu msomi anaweka paragraph nyingi akiongelea upuuzi Bila rejea ya misingi ya katiba ya nchi,vyama husika nk.yaani niwe msomi nikubali na kutetea upuuzi uliofanyika kwa Akina Mdee?ntakua nmesoma mwezini ama wapi??

Sent from my SM-G920F using JamiiForums mobile app
 

MWALLA

JF-Expert Member
Dec 12, 2006
16,245
2,000
Mkuu huyo jamaa humu kishajidharaulisha kuliko mwanachama yeyote aliyewahi kutokea hapa jamvini. Hawa ndiyo watu wanajiita wasomi lakini hawakuelimika hata chembe. Upuuzi wanaouandika ambao hauingii hata akilini unashangaza sana.
kadri siku zinavoyoyoma huyu dogo Pascal Mayalla naona kuna fyuzi kwenye oblangata yake zinapoteza ushirikiano na kichwa.
kaka yake MEKO alimwambia MAYALA ni njaa kali kwa lugha ya kisukuma.
 

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
121,665
2,000
Halafu cha ajabu hajistukii tu kwamba dharau dhidi yake kutokana na upuuzi anaouandika ili kutafuta teuzi inazidi kuongezeka badala yake ndiyo anazidi kupost pumba zake.
kadri siku zinavoyoyoma huyu dogo Pascal Mayalla naona kuna fyuzi kwenye oblangata yake zinapoteza ushirikiano na kichwa.
kaka yake MEKO alimwambia MAYALA ni njaa kali kwa lugha ya kisukuma.
 

MWALLA

JF-Expert Member
Dec 12, 2006
16,245
2,000
Halafu cha ajabu hajistukii tu kwamba dharau dhidi yake kutokana na upuuzi anaouandika ili kutafuta teuzi inazidi kuongezeka badala yake ndiyo anazidi kupost pumba zake.
Kwakweli mkuu huyu kijana Pascal Mayalla haitaji hata kuombewa tumuache tu kakake aendelee kumtosa
mzee msekwa kaweka wazi hapa sasa sijui watapinduaje akili kubwa za chadema
 

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
39,384
2,000
Swali moja rahisi sana kwako Paskali. CHADEMA ikifa, Watanzania na taifa kwa ujumla tutapata hasara gani? Unaamini NI LAZIMA CHADEMA iendelee kuwepo (exist)?

Maelezo yote hayo marefu sana uliyotoa na ambayo umekuwa ukiyatoa zaidi ya mwaka kuhusu CHADEMA, yanadhihirisha kuwa kwa mazingira ya kisiasa tuliyo nayo Tanzania, HAIWEZEKANI tuwe na mfumo wa demokrasia ya vyama vingi vya siasa nchini ambao ni BONA FIDE GENUINE.

Halafu, VERY CURIOUSLY, siioni juhudi yako ya dhati kuwaasa wenye dhamana ya kutengeneza mazingira sahihi ya demokrasia ya vyama vingi Tanzania ili kuwezesha vyama kama CHADEMA kuwepo na kufanya shughuli zake kwa ufanisi. Hapo ungeeleweka badala ya kupania kwa makala kadhaa zilizojaa jazba nyingi kutaka CHADEMA IWEPO na ikubaliane na dola tu hata katika mazingira hatarishi kiasi gani!

WHAT’S YOUR REAL MOTIVE?
Mkuu Drifter, kwanza asante kwa mchango wako, very objective, kiukweli tangu nimepandisha uzi huu, wewe ndio mtu wa kwanza kunielewa, kwasababu, kiukweli kabisa, hii jf ya sasa, tuna watu wachache sana, wenye kuweza kusoma bandiko na kisha kujiuliza what is the motive behind.

Chama cha Mapinduzi ni chama cha ukweli na haki, kiliasisiwa na Mwalimu Nyerere, mpenda haki na mtenda haki. Baada ya Mwalimu, CCM ilipitia mageuzi na kuishiwa kuhodhiwa na wenye fedha, hivyo kuzalisha kada kubwa ya makada wa CCM ambao ni makada maslahi, na kwenye uchaguzi, wanakuwa wako tayari kutumia mbinu zozote kushinda uchaguzi. JPM alipoingia, amekuja kuibadili CCM kuirudisha ile CCM ya Nyerere. Sasa ndani ya makada wa CCM, kuna makada wa aina mbili, kuna "CCM Die Hard", hawa ndio wanaotaka kuhakikisha CCM inaupondaponda upinzani na kushinda kwa asilimia 99.9% kwa kutumia mbinu zozote.

Tupo sisi makada "Modern CCM" ambao kutokana na good track ya kazi nzuri ya JPM, CCM innashinda kwa mshindi mzuri safi na clear victory, kushinda kwa haki bila kufanya figisu figisu zozote.

Kwa vile Bunge letu ni Bunge la vyama vingi, mimi naamini kuna baadhi ya wana CCM very genuine, hakupenda kuona baadhi ya wapinzani wakishindwa akiwemo mtu kama Zitto!. Lakini kutokana na wapinzani kukataliwa na wananchi, ili Bunge lichangamke, zile kamati 2 za oversight committee, PAC na LAAC, lazima ziongozwe na wabunge wa upinzania ambao ni vichwa vya ukweli, kwenye hao wabunge wote sijaona watu wa kalibre hiyo ndio maana kila siku, tunamuomba Mwenyekiti wetu, JPM, katika zile nafasi zake 10, awateua wapinzani 4, Zitto, JJ Mnyika, Mbatia na kale kabinti Queen Sendiga.

Ili CCM itawale vizuri inahitaji Upinzani makini, ndio maana kila uchao, naibalasa Chadema humu na ACT Zanzibar, waache ujinga wa kususa. Ili kusasa kwa akili ni kususa kama kwa kususa huko utaachieve something, lakini kususa tuu for the sake of kususa, huku you won't achieve anything huu ni ujinga!.

Karibu tena.
P
 

MWALLA

JF-Expert Member
Dec 12, 2006
16,245
2,000
Mkuu Drifter, kwanza asante kwa mchango wako, very objective, kiukweli tangu nimepandisha uzi huu, wewe ndio mtu wa kwanza kunielewa, kwasababu, kiukweli kabisa, hii jf ya sasa, tuna watu wachache sana, wenye kuweza kusoma bandiko na kisha kujiuliza what is the motive behind.

Chama cha Mapinduzi ni chama cha ukweli na haki, kiliasisiwa na Mwalimu Nyerere, mpenda haki na mtenda haki. Baada ya Mwalimu, CCM ilipitia mageuzi na kuishiwa kuhodhiwa na wenye fedha, hivyo kuzalisha kada kubwa ya makada wa CCM ambao ni makada maslahi, na kwenye uchaguzi, wanakuwa wako tayari kutumia mbinu zozote kushinda uchaguzi. JPM alipoingia, amekuja kuibadili CCM kuirudisha ile CCM ya Nyerere. Sasa ndani ya makada wa CCM, kuna makada wa aina mbili, kuna "CCM Die Hard", hawa ndio wanaotaka kuhakikisha CCM inaupondaponda upinzani na kushinda kwa asilimia 99.9% kwa kutumia mbinu zozote.

Tupo sisi makada "Modern CCM" ambao kutokana na good track ya kazi nzuri ya JPM, CCM innashinda kwa mshindi mzuri safi na clear victory, kushinda kwa haki bila kufanya figisu figisu zozote.

Kwa vile Bunge letu ni Bunge la vyama vingi, mimi naamini kuna baadhi ya wana CCM very genuine, hakupenda kuona baadhi ya wapinzani wakishindwa akiwemo mtu kama Zitto!. Lakini kutokana na wapinzani kukataliwa na wananchi, ili Bunge lichangamke, zile kamati 2 za oversight committee, PAC na LAAC, lazima ziongozwe na wabunge wa upinzania ambao ni vichwa vya ukweli, kwenye hao wabunge wote sijaona watu wa kalibre hiyo ndio maana kila siku, tunamuomba Mwenyekiti wetu, JPM, katika zile nafasi zake 10, awateua wapinzani 4, Zitto, JJ Mnyika, Mbatia na kale kabinti Queen Sendiga.

Ili CCM itawale vizuri inahitaji Upinzani makini, ndio maana kila uchao, naibalasa Chadema humu na ACT Zanzibar, waache ujinga wa kususa. Ili kusasa kwa akili ni kususa kama kwa kususa huko utaachieve something, lakini kususa tuu for the sake of kususa, huku you won't achieve anything huu ni ujinga!.

Karibu tena.
P
Ngoa nipime ubongo wako leo kama umikaa sawia... utaongea kitu hapa..

....nduGEY.. Anasema ALIVUTA (cha arusha) ili mungu amsaidie
 

lungw

JF-Expert Member
Jun 13, 2016
207
250
Wanabodi,
Hili ni bandiko elimishi kuhusu uendeshaji wa vyama vya Siasa nchini Tanzania, kuna vyama vinaendeshwa na viongozi kama mungu watu, na kujiendesha tuu hivyo vyama, wanavyotaka wao, kama mali yao, wakijisikia kufukuza mwanachama, hata kwa makosa ambayo sio ya msingi, wanaitana na kukaa kama Kangaroo court na kufukuza wanachama kwa kuwavua uanachama kienyeji enyeji tuu. Kufuatia kukithiri kwa tabia hii Chadema kufanya hivi bila kuhojiwa na yeyote, hatimaye sasa, tabia hii imeota mizizi na kuendana na msemo huu wa Kiswahili kuwa "Mzoea vya kunyonga, vya kuchinja haviwezi"! Chadema ilizoea kuwanyonga wanachama wake kwa kuwafukuza kienyeji enyeji na kujinga jinga, nimeisoma taarifa hii kwa faraja.

Halima Mdee ni mwanamke shujaa, msomi na mwanasheria, anaijua katiba ya Chadema, hivyo amegomea kikao kilichoitishwa kienyeji enyeji ili kumchukulia hatua yeye na wabunge 19, makandaa mashujaa wa kike wa Chadema, waliamua kutanguliza mbele maslahi ya Taifa vs maslahi ya chama.

Utangulizi: Haki ya Kujadili Mambo ya Chadema Kwa Mtu Ambaye Sii Mwanachama, Mfuasi, Mshabiki wa Chadema.
Sii wengi wanafahamu kuwa vyama vya siasa Tanzania, vyenye wabunge na madiwani, sio private parties za wanachama na viongozi, ni public parties za umma kutokana na kulipwa ruzuku ya serikali ambayo ni kodi yako wewe na mimi, hivyo Mtanzania yoyote ambaye ni taxpayers, has the right kuhoji jambo lolote kuhusu any public entity kwasababu inaendeshwa kwa kodi yake!. Hivyo nawaomba nyie manazi wa Chadema, mliotamalaki humu jf, kaeni mkijua mtoa mada ni mmoja wa wachangiaji wa fedha za kuiendeshea Chadema!, hivyo ana haki kuhoji jambo lolote kuhusu uendeshaji wa chama chochote, na ilimsidhanie nimeikamia Chadema tuu, nimeisha wahi kusema mengi kuhusu CCM, nimesema mengi kuhusu CUF, nimesema kuhusu NCCR, ACT, etc.

Kama Sio Chadema, Unahoji au Unajadili Mambo ya Vikao vya Ndani vya Chadema na Maamuzi ya Chadema ili Iweje?.
Hapa naomba kujitambulisha kama mwandishi wa habari wa kujitegemea. Fani ya uandishi nayo ina specializations, kama ilivyo ualimu, kuna waalimu wa somo la hesabu, Kiingereza, Sayansi, Jiografia etc, na kwenye Udakitari kuna madakitari wa meno, wafamasia, wapasuaji, madakitari wa watoto, kinamama etc, hivyo kwenye uandishi, kuna maripota, maproducers, ma presenters, news readers, wahojaji, yaani wafanya mahojiano, mimi nime specialize kwenye kufanya mahojiano, hivyo my area of specialization ni kuhoji tuu!. Kufuatia kazi yangu ni kuhoji tuu, nikikutana na jambo lolote ambalo sio la kawaida, kazi yangu ni kuhoji. Katika pitia pitia zangu Katiba za vyama, kuna siku nikakutana na kitu cha ajabu kwenye Katiba ya Chadema, nilipohoji kuhusu hicho kitu, na jibu ninilojibiwa na uongozi wa juu wa Chadema, ndipo nikagundua kuwa kumbe kuna viongozi hadi wa ngazi za juu za vyama ni ma mbumbumbu kuhusu baadhi ya vipengele vya katiba za vyama vyao, tangu pale nikajikuta kila Chama kikifanya uamuzi wa ajabu ajabu kinyume cha utaratibu wa katiba zao, mimi huwa naibuka na kukemea kwa kuwasisitiza waheshimu katiba zao. Hoja ya viongozi wa juu wa Chadema, kuwa mbumbumbu kuhusu katiba zao, tembelea uzi huu...https://www.jamiiforums.com/threads/tuhuma-hii-chadema-kendeshwa-kwa-katiba-fake-ikithibitishwa-chadema-inaweza-kufutwa.543947/

Kwa Vile Kamati Kuu ya Chadema Imewaita Kina Halima Mdee ili Iwahoji, na Wamegomea Mwito, Naomba Kuwaletea Vifungu vya Mamlaka ya Nidhamu Kwa Mujibu wa Katiba ya Chadema.


6.5 Taratibu zifuatazo lazima zizingatiwe katika kuchukua hatua za kinidhamu:-
6.5.1 Kila tawi litaweka kumbukumbu/orodha ya wanachama wanaokoma kuwa wanachama Uongozi na Vikao vya Tawi. Kumbukumbu itaonyesha jina kamili la mwanachama katika rejista ya wanachama tarehe aliyokoma kuwa mwanachama wa Tawi na sababu za kukoma kuwa mwanachama.
6.5.2 Kwa mujibu wa Ibara 5.4.3 na 5.4.4 ya Katiba, mwanachama yeyote hatachukuliwa hatua za kinidhamu ama kuonywa ama kuachishwa ama kufukuzwa uanachama bila kwanza:
(a) Kujulishwa makosa yake kwa maandishi na kutakiwa kutoa majibu katika muda usiopungua wiki mbili.
(b) Kupewa nafasi ya kujitetea mbele ya kikao kinachohusika.
(c) Mwanachama atajulishwa kwa maandishi uamuzi wa kikao mnamo wiki mbili baada ya kusikilizwa.
(d) Kamati Kuu inaweza kuchukua hatua za dharura bila kuzingatia utaratibu wa kifungu (a) na (b) hapo juu kama itaona maslahi ya Chama kwa ujumla yanaweza kuathiriwa isipokuwa mwachama au kiongozi anayelalamikiwa atalazimika kuitwa kwenye kikao husika.
6.5.3 Mtu yeyote aliyepoteza uanachama wake kwa mujibu wa Ibara ya 5.4 ya Katiba atapoteza haki zake zote za uanachama na hatarudishiwa ada, zawadi au ruzuku yeyote aliyokwishaitoa kabla ya kupoteza uanachama wake.
6.5.4 Mwanachama aliyepewa adhabu na kikao kimoja cha kikatiba atakuwa na haki ya kukata rufani kwa kikao cha ngazi ya juu ya kile kilichompa adhabu.
6.5.5 Mwanachama aliyewahi kuachishwa ama kufukuzwa uanachama anaweza kuomba kurejea kwa maandishi kupitia ngazi iliyomfukuza akieleza sababu za kutaka kurejea. Maombi yake yatachunguzwa kwenye ngazi hiyo na kutolewa maamuzi na vikao vya ngazi moja ya juu inayofuata. Aliyesimamishwa au kufukuzwa na Kamati Kuu ataweza tu kurejeshwa na Baraza Kuu. Watakaofukuzwa na Mkutano Mkuu hawatakuwa na chombo kingine chochote kitakachotengua uamuzi huo.
6.5.6 Kiongozi yeyote hatachukuliwa hatua za kinidhamu bila kwanza kupewa mashitaka kwa maandishi na mamlaka husika na kupewa nafasi ya kujibu mashitaka kwa maandishi.
6.5.7 Kiongozi mhusika, zaidi ya utetezi wa maandishi, atapewa nafasi ya kujieleza bayana mbele ya kikao cha mamlaka ya nidhamu.
6.5.8 Kiongozi aliyeadhibiwa atapewa taarifa ya misingi ya maamuzi ya mamlaka ya nidhamu ili kumwezesha kuamua kukata rufani au
6.5.9 Mwadhibiwa atakayeamua kukata rufani atatakiwa kufanya hivyo katika muda wa siku thelathini baada ya kuarifiwa uamuzi wa adhabu.
6.5.10 Baada ya kutoa uamuzi kikao husika kinalazimika kuandaa taarifa kamili ya mwenendo wa shauri na kuwasilisha ngazi ya juu. Taarifa hiyo lazima ifike katika muda wa siku kumi na nne baada ya kikao cha maamuzi.

Sasa kwa mujibu wa katiba ya CHADEMA, ili kumvua mtu uanachama kuna mlolongo wa kanuni na taratibu za kufuatwa kama nilivyo zianisha hapo juu, jee zilifuatwa?
  • Kwa nini CC ya Chadema, inawaita watu kihuni huni tuu, bila kuandaa hati ya mashtaka kwa maandishi yenye tuhuma zote ambazo mtuhumiwa anakabiliwa nazo. Jee hati hizi za mashitaka kimaandishi ziliandaliwa?.
  • Hati hiyo ya mashitaki kimaandishi inatakiwa ikabidhiwa kwa mtuhumiwa kwa "despatch" ili kuthibitisha imemfikia. Je, hili lilifanyika? Nimesikia kuna watu waliitwa kwa simu, je huu ndio utaratibu kwa jambo zito kama hili?
  • Mtuhumiwa atatakiwa kuzijibu tuhuma za mashitaka hayo ndani ya kipindi cha siku 14 tangu tarehe aliyopokea barua ile ili apate muda wa kutosha kutafakari, je hili litafanyika?
  • Baada ya majibu ya hati ile ya mashitaka kurejeshwa, ndipo mamlaka ya nidhamu ingepaswa kuitisha kikao rasmi kwa mujibu wa katiba na kumwalika mtuhumiwa kwa barua ili kuwapa nafasi ya kujieleza na kumsikiliza kabla ya kufikia maamuzi!. Jee this time Chadema itafuata taratibu?
Halima na genge lake they are very right, Chadema ilizoea kufanya mambo kienyeji, leo imekutana na kisiki cha mpingo!
Chadema sasa lazima ijifunze kufanya mambo kwa kufuata katiba yake, sheria, taratibu na kanuni!, kufanya mambo kwa kienyeji enyeji kwa mtindo wa zimamoto, sasa basi!

Hongera sana Kamanda Mhe. Halima Mdee na makamanda makomandoo wa kike kwa kuifunza nidhamu chama chenu cha Chadema.

Paskali
Update:
Mkuu mode, bila kuingilia uhuru na mamlaka yako wewe mode ku edit bandiko lolote na heading yoyote, ila heading inapotumia tamathali za semi, methali au nahau, neno hilo linapaswa kuwa vile vile lilivyo kwa sababu tamathali za semi, zinatumia vina, ukibadili kitu, vina havizami!. Mode hapaswi kulibadili!. Nimetumia neno
"Mzoea vya kunyonga, vya kuchinja haviwezi", hivi ndivyo neno rasmi lilivyo, ni tofauti na neno ulilotumia wewe.
Naomba neno rasmi lirudishwe!.
P

6.5.2 d imejibu swali lako na waliitwa wakadharau kamati kuu hayo mengine njaa tu zinakusumbua
 

lungw

JF-Expert Member
Jun 13, 2016
207
250
Chadema wakubali yaishe. Walishiriki uchaguzi ili wapate kura .Wamepata wabunge 20.Si haba wawape ushirikiano wawashe moto bungeni. Waendelee kujenga chama. Na waongee hoja bungeni. Maana huku nje wakiongea wanaitwa wachochezi.
Kwenda kwao bungeni Kuna halalisha uchaguzi kua ulikua poa na wataendelea kupokea hiyo misaada yao Bora tusiwe na wawakilishi bungeni lakini na mabeberu yawanyime misaada ili aikiri iwakae vizur
 

lungw

JF-Expert Member
Jun 13, 2016
207
250
Mbowe anajua misimamo ya akina Lissu lakini pia bila ruzuku ataendesha vipi chama? Hao wapiga kelele wanachangia nguvu tu sio pesa! He is playing very smart.
Chadema inawanachama hai milioni 6 ikiweka utaratibu mzuri kila mwezi mwanachama achangie elfu 1000 inatosha kabisa kuendesha chama
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom