"Mzoea vya kunyonga vya kuchinja Haviwezi". Hongera Halima Mdee na Makamanda wote kwa kugomea wito wa kienyejienyeji

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,467
113,581
Wanabodi,
JF ni mtandao wa jamii, moja ya faida kubwa ya mitandao ya kijamii zaidi ya kuhabarisha habari mbalimbali, ni kuelimishana, wale members wa mitandao ya kijamii wanaojua jambo fulani, na ambao sio wachoyo wa kuelimisha wengine, hujitolea muda wao mwingi wa thamani, kuwaelimisha wengine, na hiki ndicho mimi ninacho kifanya kwenye bandiko hili.

Hili ni bandiko elimishi kuhusu uendeshaji wa vyama vya Siasa nchini Tanzania, kuna vyama vinaendeshwa na viongozi kama miungu watu!, na kujiendeshea tuu hivyo vyama, jinsi wanavyotaka wao, kama mali zao, binafsi au biashara zao, jinsi wanavyo jisikia, wakijisikia kufukuza mwanachama fulani, hata kwa makosa ambayo sio ya msingi ya kustahili kufukuzwa,
wanaitana na kukaa kama a Kangaroo court na kufukuza wanachama kwa kuwavua uanachama kienyeji enyeji tuu kama kufukuza mbwa koko barazani kwako!.

Kufuatia kukithiri kwa tabia hii kwa baadhi ya vyama ikiwemo Chadema kufanya hivi bila kuhojiwa na yeyote, hatimaye sasa, tabia hii imeota mizizi na kuendana na msemo huu wa Kiswahili kuwa "Mzoea vya kunyonga, vya kuchinja haviwezi", yaani katika timua timua, Chadema imezoe vya kunyonga, jee vya kuchinja itaviweza?. Chadema ilizoea kuwanyonga wanachama wake kwa kuwafukuza kienyeji enyeji na kujinga jinga bila kufuata katiba yake ya Chadema iliyoweka, sheria, taratibu na kanuni za mamlaka za nidhamu ya kufukuza uanachama. Leo nimeisoma taarifa hii kwa faraja sana...
Walitakiwa kufika saa mbili asubuhi mbele ya kamati kuu ya CHADEMA Taifa, hadi saa tano asubuhi hawajafika ofisi za chama, makao makuu. Jeuri, kiburi, dharau. Kuna nguvu kubwa ya DOLA nyuma yao. Wangelifika mbele ya kamati kuu, wajieleze, nafikiri wameamua kuirahishia kazi CC.

Toka kwa mjumbe kamati kuu
Halima Mdee ni mwanamke shujaa, msomi na mwanasheria, anaijua katiba ya Chadema, anaijua haki yake na yeye kama Mwenyekiti wa Bawacha, anaijua mamlaka yake ya nidhamu, hivyo yeye Halima Mdee, amegomea kikao batili cha mamlaka ya nidhamu kilichoitishwa kiubatili kwa kienyeji enyeji ili kumchukulia hatua yeye na wabunge 19, ambao wote ni makamanda makomandoo shupavu na mashujaa wa kike wa Chadema, walio ipigania Chadema kwa machozi jasho na damu, baada ya kubaini chama chao kinafanya ujinga fulani, kugomea fursa fulani, hivyo Halima Mdee kama Mwenyekiti wa Bawacha, akamua kutanguliza mbele maslahi ya Taifa vs maslahi ya chama na kuwaongoza Wanawake wenzake kuchangamkia fursa.

Utangulizi: Haki ya Kujadili Mambo ya Chadema Kwa Mtu Ambaye Sii Mwanachama, Mfuasi, Mshabiki wa Chadema.
Sii wengi wanafahamu kuwa vyama vya siasa Tanzania, vyenye wabunge na madiwani, sio private parties za viongozi na wanachama pekee, bali ni public parties za umma kutokana na kulipwa ruzuku ya serikali ambayo ni kodi yako wewe na mimi, hivyo Mtanzania yoyote ambaye ni taxpayers, has the right to know it's public as well as its private conduct of it's leaders Kwa kuhoji jambo lolote kuhusu any public entity kwasababu inaendeshwa kwa kodi yake!. Hivyo nawaomba nyie manazi wa Chadema, mliotamalaki humu jf, kaeni mkijua mtoa mada ni mmoja wa wachangiaji wa fedha za kuiendeshea Chadema!, hivyo ana haki kuhoji jambo lolote kuhusu uendeshaji wa chama chochote, na ili msidhanie nimeikamia Chadema tuu, nimeisha wahi kusema mengi kuhusu CCM, nimesema mengi kuhusu CUF, nimesema kuhusu NCCR, ACT, etc.

Kama Sio Chadema, Unahoji au Unajadili Mambo ya Vikao vya Ndani vya Chadema Kama Nani? na Maamuzi ya Ndani vya Chadema Vinakuhusu nini na Una Hoji ili Iweje?.
Hapa naomba kujitambulisha kama mwandishi wa habari wa kujitegemea. Fani ya uandishi nayo ina specializations, kama ilivyo ualimu, kuna waalimu wa somo la hesabu, Kiingereza, Sayansi, Jiografia etc, na kwenye Udakitari kuna madakitari wa meno, wafamasia, wapasuaji, madakitari wa watoto, kinamama etc, hivyo kwenye uandishi, kuna maripota, maproducers, ma presenters, news readers, wahojaji, yaani wafanya mahojiano, mimi nime specialize kwenye kufanya mahojiano, interviews na hivyo my area of specialization ni kuhoji tuu!. Kufuatia kazi yangu ni kuhoji tuu, nikikutana na jambo lolote ambalo sio la kawaida, kazi yangu ni kuhoji.

Katika pitia pitia zangu Katiba za vyama, kuna siku nikakutana na kitu cha ajabu sana kwenye Katiba ya Chadema, nilipohoji kuhusu hicho kitu, na jibu ninilojibiwa na uongozi wa juu wa Chadema, ndipo nikagundua kuwa kumbe kuna viongozi hadi wa ngazi za juu za vyama ni ama ni ma mbumbumbu kuhusu baadhi ya vipengele vya katiba za vyama vyao, au simply ni vilaza tuu ambao hawana muda kusoma katiba za vyama vyao!.

Tangu pale nikajikuta kila Chama kikifanya uamuzi wa ajabu ajabu kinyume cha utaratibu wa katiba zao, mimi huwa naibuka na kukemea kwa kuwasisitiza waheshimu katiba zao. Hoja ya viongozi wa juu wa Chadema, kuwa mbumbumbu kuhusu katiba zao, tembelea uzi huu... Tuhuma Hii: CHADEMA kendeshwa kwa Katiba "Fake" ikithibitishwa, CHADEMA inaweza kufutwa

Kwa Vile Kamati Kuu ya Chadema Imewaita Kina Halima Mdee ili Iwahoji, na Wamegomea Mwito, Naomba Kuwaletea Vifungu vya Mamlaka ya Nidhamu Kwa Mujibu wa Katiba ya Chadema.

6.5 Taratibu zifuatazo lazima zizingatiwe katika kuchukua hatua za kinidhamu:-
6.5.1 Kila tawi litaweka kumbukumbu/orodha ya wanachama wanaokoma kuwa wanachama Uongozi na Vikao vya Tawi. Kumbukumbu itaonyesha jina kamili la mwanachama katika rejista ya wanachama tarehe aliyokoma kuwa mwanachama wa Tawi na sababu za kukoma kuwa mwanachama.
6.5.2 Kwa mujibu wa Ibara 5.4.3 na 5.4.4 ya Katiba, mwanachama yeyote hatachukuliwa hatua za kinidhamu ama kuonywa ama kuachishwa ama kufukuzwa uanachama bila kwanza: (haya ni masherti ya vikao vya nidhamu)
(a) Kujulishwa makosa yake kwa maandishi na kutakiwa kutoa majibu ya maandishi katika muda usiopungua wiki mbili. (Mashitaka ni kwa maandishi na Majibu ni kwa maandishi na sio kuitana kienyeji enyeji)

(b) Kupewa nafasi ya kujitetea mbele ya kikao kinachohusika.
(c) Mwanachama atajulishwa kwa maandishi uamuzi wa kikao mnamo wiki mbili baada ya kusikilizwa.
(d) Kamati Kuu inaweza kuchukua hatua za dharura bila kuzingatia utaratibu wa kifungu (a) na (b) hapo juu kama itaona maslahi ya Chama kwa ujumla yanaweza kuathiriwa ( kwenye issue ya kina Halima Mdee, kulikuwa na uharaka huu?.) isipokuwa mwachama au kiongozi anayelalamikiwa atalazimika kuitwa kwenye kikao husika.
6.5.3 Mtu yeyote aliyepoteza uanachama wake kwa mujibu wa Ibara ya 5.4 ya Katiba atapoteza haki zake zote za uanachama na hatarudishiwa ada, zawadi au ruzuku yeyote aliyokwishaitoa kabla ya kupoteza uanachama wake.
6.5.4 Mwanachama aliyepewa adhabu na kikao kimoja cha kikatiba atakuwa na haki ya kukata rufani kwa kikao cha ngazi ya juu ya kile kilichompa adhabu.
6.5.5 Mwanachama aliyewahi kuachishwa ama kufukuzwa uanachama anaweza kuomba kurejea kwa maandishi kupitia ngazi iliyomfukuza akieleza sababu za kutaka kurejea. Maombi yake yatachunguzwa kwenye ngazi hiyo na kutolewa maamuzi na vikao vya ngazi moja ya juu inayofuata. Aliyesimamishwa au kufukuzwa na Kamati Kuu ataweza tu kurejeshwa na Baraza Kuu. Watakaofukuzwa na Mkutano Mkuu hawatakuwa na chombo kingine chochote kitakachotengua uamuzi huo.
6.5.6 Kiongozi yeyote hatachukuliwa hatua za kinidhamu bila kwanza kupewa mashitaka kwa maandishi na mamlaka husika na kupewa nafasi ya kujibu mashitaka kwa maandishi.
6.5.7 Kiongozi mhusika, zaidi ya utetezi wa maandishi, atapewa nafasi ya kujieleza bayana mbele ya kikao cha mamlaka ya nidhamu.
6.5.8 Kiongozi aliyeadhibiwa atapewa taarifa ya misingi ya maamuzi ya mamlaka ya nidhamu ili kumwezesha kuamua kukata rufani au
6.5.9 Mwadhibiwa atakayeamua kukata rufani atatakiwa kufanya hivyo katika muda wa siku thelathini baada ya kuarifiwa uamuzi wa adhabu.
6.5.10 Baada ya kutoa uamuzi kikao husika kinalazimika kuandaa taarifa kamili ya mwenendo wa shauri na kuwasilisha ngazi ya juu. Taarifa hiyo lazima ifike katika muda wa siku kumi na nne baada ya kikao cha maamuzi.

Sasa kwa mujibu wa katiba ya CHADEMA, ili kumvua mtu uanachama kuna mlolongo wa kanuni na taratibu za kufuatwa kama nilivyo zianisha hapo juu, jee zilifuatwa?
  • Kwa nini CC ya Chadema, inawaita watu kihuni huni tuu, bila kuandaa hati ya mashtaka kwa maandishi yenye tuhuma zote ambazo mtuhumiwa anakabiliwa nazo. Jee hati hizi za mashitaka kimaandishi ziliandaliwa?.
  • Hati hiyo ya mashitaki kimaandishi inatakiwa ikabidhiwa kwa mtuhumiwa kwa "despatch" ili kuthibitisha imemfikia. Je, hili lilifanyika? Nimesikia kuna watu waliitwa kwa simu, je huu ndio utaratibu kwa jambo zito kama hili?
  • Mtuhumiwa atatakiwa kuzijibu tuhuma za mashitaka hayo ndani ya kipindi cha siku 14 tangu tarehe aliyopokea barua ile ili apate muda wa kutosha kutafakari, je hili litafanyika?
  • Baada ya majibu ya hati ile ya mashitaka kurejeshwa, ndipo mamlaka ya nidhamu ingepaswa kuitisha kikao rasmi kwa mujibu wa katiba na kumwalika mtuhumiwa kwa barua ili kuwapa nafasi ya kujieleza na kumsikiliza kabla ya kufikia maamuzi!. Jee this time Chadema itafuata taratibu?
Halima na genge lake they are very right, kugomea wito huo wa kienyeji wa kufika mbele ya Kangaroo court iitwayo CC ya Chadema ambapo CC hiyo inapokaa kama a Kangaroo court, kazi yake huwa ni moja tuu, kuchinja bila kueleleza Kibla!. Ukichinja bila kuelekeza Kibla, kunahesabika ni kunyonga. Chadema ilizoea kufanya mambo kienyeji, leo imekutana na kisiki cha mpingo!.

Chadema sasa lazima ijifunze kufanya mambo kwa kufuata katiba yake, sheria, taratibu na kanuni!, kufanya mambo kwa kienyeji enyeji kwa mtindo wa zimamoto, sasa basi!

Hongera sana Kamanda Mhe. Halima Mdee na makamanda wako makomandoo wa kike kumi na kenda, kwa kuifunza heshima, adabu, na nidhamu Chadema ili sasa ijifunze kufuata katiba ya chama chenu cha Chadema.

Paskali
 
Kwani wamefanya kosa gani mpaka waitwe kamatiii kuuuu?? Yaaaniii wabunge ambao wanajipanga kutupia nondo Kali, bungeniii, huku halima mdee akiwa mwenyeki wa KUB, na esta amosi bulaya akiwa mnadhimu mkuu wa KUB. Sasa wanaitwa wapi tena hao wabunge wa JMT? Waliokosa ubunge jipangeni 2025.
 
Halima Mdee amesema hadharani kuwa wamepata baraka za Chama chini ya uongozi wa Mbowe. Lakini, Mbowe hajatoka hadharani kukanusha hilo. Kwahiyo, simple logic ni kuwa Mbowe anaunga mkono wabunge hawa kuapishwa.

Mengine yanayoendelea ni kuwalaghai tu wanaharakati. Ni sawa na kumuahidi mtoto peremende ili aache kulia.
 
Huna lolote njaa tu inakusumbua,siyo wewe uliyeenda kuomba kuchaguliwa na chama chako wakuchague umtoe huyo unayemsifia hapa kigezo uwezo wa kuleta maendeleo hana na bado hukupata hata kura tano?

Leo upo hapa unamsifia kwamba anajitambua,miaka yote unaandika humu kusifia kwanini huonekani?inawezekana mamlaka zinakujua kwamba wewe ni snitch na unayumbishwa na njaa that's why hupewi kitengo ukatulia.
 
Mayalla! Unapogoma kwenda kazini kwa sababu ya kuwaogopa wafanyakazi wenzako ni kwamba umeacha kazi na si vinginevyo. Unampaje hongera anayejitoa uanachama! Kisa, anawaogopa wanachama wenzake, tulia tafakari.

Sijawahi kukushambulia na mara zote husema wakusikilize ili wakujue, lakini kwa hili umekosea ungewashauri waende au watoe ushahidi polisi au kwingineko wanakoona watalindwa.
 
Halima Mdee amesema hadharani kuwa wamepata baraka za Chama chini ya uongozi wa Mbowe. Lakini, Mbowe hajatoka hadharani kukanusha hilo. Kwahiyo, simple logic ni kuwa Mbowe anaunga mkono wabunge hawa kuapishwa.

Mengine yanayoendelea ni kuwalaghai tu wanaharakati. Ni sawa na kumuahidi mtoto peremende ili aache kulia.
Wangeenda na kuiambia CC kuwa Mbowe amewaruhusu ili CC imtake Mbowe ajieleze. Mayalla, hilo la kufukuzwa uanachama wewe umeambiwa na CC? Au na watuhumiwa?
 
Naona umeamua kujivua akili kabisa, aliyekwambia wanaenda kufukuzwa ni nani? Wale waliitwa kuhojiwa sio kuvuliwa uanachama, pili kwanini huoji kupatikana kwao kama kulifuata taratibu zote za kichama ila unahoji wao kuitwa tu? Hivi ukiwa CCM lazima kutetea kitu hata kama sio cha haki? Unanajisi taasisi zile zote ulizopitia kielimu.
 
Back
Top Bottom