Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 48,691
- 149,912
Huyu mzee ni Raisi Mstaafu na ni mwana CCM lakini ni kiongozi pekee ambae ni nadra sana leo hii kusikia wapinzani wakimsema vibaya, kumkejeli, kumdhihaki au kumponda katika majukwaa ya kisiasa.Mzee huyu alishiriki uzinduzi wa kampeni za CCM,ameendelea kupewa mialiko mbalimbali na kote huko huwa anaongea/anahutubia lakini katika platform zote hizo sijawahi kumsikia akikejeli,kutukana wala kubeza wapinzani.
Kwa miaka ya hivi karibuni,niambieni ni lini mmewahi kuwasikia wapinzani wakimkejeli huyu mzee?Ni lini mzee huyu amewahi kuandikwa vibaya mitandaoni?Ni lini mmewahi kuwasikia wanaharakati mbalimbali wakimyooshea kidole mzee huyu?Hamjiulizi ni kwanini?Sababu kubwa ni kwasababu anajua aongee nini,wakati gani,mahali gani na zaidi ahaheshimu wadhifa alionao kama Raisi Mstaafu wa nchi hii.
Viongozi wote wastaafu wanapaswa kuiga kutoka kwa mzee Mwinyi na hata wao watapendwa na wataheshimiwa karibu na kila mtu.Simanishi kama viongozi wengine hawapendwi na kuheshimiwa,lakini naamini mzee huyu amekuwa kipenzi cha watu wengi zaidi wakiwemo wapinzani ndio maana huwezi sikia hata wapinzani wakimtaja mzee huyu majukwaani kwa mabaya.
Leo hii sidhani kama kuna mtu anaweza kutamka mzee huyu ashitakiwe kwa makosa aliyoyafanya akiwa madarakani.
Huyu mzee ni icon wa kuheshimu human dignity bila kujali wadhifa aliokuwa nao baada ya kustaafu.
Mzee wa watu hana makuu na anaheshimu kila rai wa nchi.Ni mzee huyu aliewahi pigwa kibao lakini ni mzee huyu nasikia alitaka aliemipiga kibao asamehewe!Kiongozi gani leo hii angekuwa tayari kusamehe mtu aliempiga kofi tena hadharani?
Mzee Mwinyi mungu akupe maisha marefu maana umekuwa raisi mstaafu wa wote bila kujali itikadi zetu.Ubarikiwe sana.
NB:
Hii mada ni ushahidi kuwa comprehension ni janga lingine kubwa kwa wabongo.Mada hii inamuongelea mzee Mwinyi kama raisi mstaafu na si wakati alipokuwa madarakani lakini watu wanajadili kwa kumtazama wakati alipokuwa madarakani!
Kumbe huwa tunafeli mitihani sio kwasababu inaandikwa kingereza,bali ni kwasabubu ni wabovu katika Reading Comprehension.