Mmemsikia Rais anajuta kuwa Rais!

Hii sasa ni mara ya pili. Mara ya pili kuambiwa au kusikia kuwa Mhe. Rais anajuta kugombea na kuchaguliwa kuwa Rais. Mara ya kwanza watanzania waliambiwa na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam,Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo.

Ilikuwa kanisani,kanisa katoliki la Mtakatifu Petro. Kardinali Pengo alisema kuwa alizungumza na Rais Magufuli kwa njia ya simu akiwa Chato,Geita. Pamoja na mambo mengine,Rais akajuta kuwa Rais. Wakati Kardinali Pengo akifichua hilo,Rais Magufuli alikuwemo kanisani humo kuhudhuria ibada ya misa takatifu.

Mara ya pili ya kujuta ni jana. Mhe. Rais,alipokuwa akihutubia kilele cha Mei Mosi,alitamka na kusikika kuwa anajuta kuwa Rais. This is very serious. Inajulikana kuwa asingejuta kama angekuwa amejiandaa na kuutaka Urais. Asingejuta kama angeamua kugombea Urais kwa hiyari yake.

Ni muda wa kuwaambia watanzania,nani alimlazimisha Rais kugombea? Ni kwa malengo gani? Ili kutojuta zaidi,namshauri Rais kutogombea Urais mwaka 2020!

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
usipotoshe..ni kazi ngumu kwa mtu mwenye kukitendea haki cheo cha rais. alisema anakipata jasho linamtoka kwa kazi ngumu. kwa aliyetaka kwenda kufanya biashara kwake ingekua utukufu tu na kupiga dili. licha ya kukataliwa mtafuta utukufu ikulu bado anatoa machozi kulilia ikulu wakati mtumishi wa watu jasho inamtoka.
 
John Joseph Pombe Magufuli hakutaka wala hakuwazia kuwa Rais wa Jamhuriya Muungano wa Tanzania. Wiki ya Mwisho ya May 2015 kama sijakuosea alienda kukagua Maendeleo ya Daraja la Kigamboni akasema anataka liishe na lizinduliwe na Dr. Jakaya ili asije Rais mwingine akajifanya yeye ndie kalijenga!!!!

Siku Dr. JAKAYA akimtambulisha Rasmi kuwa Mgombea wa Chama July 12, 2015 Dodoma anasema yeye( Jakaya) ndie aliemwambia JPM akachukue form za Urais nae Magufuli akamuuliza atatosha? JK akamwambia kachukue kutosha au kutokutosha kwako itajulikana Dodoma. Dr. Magufuli hakujiandaa kuwa Rais ni jambo la wazi na hilo linaweza kuwa jambo litakalomsaidia kufanya vizuri, ukijiandaa unakuwa na Makundi mengi sana yanayokusaidia yakitegemea fadhila, makundi hayo yamemsumbua sana JK.
Kula like yangu mkuu..
 
Ukitaka uone nchi hii kuongoza sio kazi kuwa kama Kikwete, kiguu Na njia nchi za mbali.

Ukipewa tariifa haina haja ya kuifuatilia wewe ni kukubaliana tu.

Mtumishi akilalamikiwa kwa ufisadi unamhamishia mkoa mwingine.

Wanaopiga wapige tu ila wasijulikane.
 
Kuna siku nilihoji tamko la Rais kuwa hakujiandaa kuwa Rais! Watu walinizomea sana! Sasa leo ametoa tena kauli ya kushangaza kuwa anajuta kuutaka Urais...!

Hivi hili halina uhusiano na kauli kuwa hakujiandaa kwa majukumu haya... Kwa maneno yake "alikuwa anabeep! :-

Nyie watu mnashangaza sana, Hivi sifa ya kuwa Rais ni kujiandaa au kufaa?
Halafu mnashindwa hata kurecall kauli za Baba wa taifa, hata yeye aliona urais ni mzigo mkubwa sana hasa kwa watu waaminifu, na aliwahi kusema "watu waaminifu hawakimbilii ikulu .... ukiona mtu anakimbilia na fedha anatumia, ni wa kuogopa kama ukoma ..." JPM ni mwaminifu kwa nchi yake, kwa nini asione/ asijute kuongoza watu wenye akili za kupiga dill tu na sio kuhudumia watu? au nawe ni mpigaji nini?
 
Mbona Mwalimu Nyerere aliwai sema Urais ni mzigo mzito, je na yeye alikua hajajiandaa kua Rais..
tena alisema kwa yeyote mwenye mapenzi mema na nchi na raia wake hawezi kukimbilia ikulu...shida zote za wtz anaziona ni zake...sasa lowasa anahonga pesa ili aende kwenye matatizo!
 
Lazima ajute, nchi imeoza, hakutegemea TZ inayonuka kama alivyoikuta;
MUNGU amlinde tu, hakuna lingine.
 
Wacha kujaza saver za watu...zinagharamiwa ujue!
Kwa sababu anafanya kazi lakini kwa MAFISADI wengine ingekuwa kazi raisi sana. FISADI KAMA LOWASSA INSINGEMPA SHIDA KAZI HII YA URAISI HATA KIDOGO. EE MUNGU WA REHEMA MLINDE MJA WAKO NA UMPE AMANI YA KWELI ITOKAYO KWAKO.
 
Magufuli, wakati unaendelea kuondoa "majipu" -(silipendi neno hilo), shift your emphasis, weka mifumo ikusaidie kuiweka nchi sawa. Unajuta kuwa rais kwa vile hakuna mifumo. Na mifumo ni katiba ya Warioba and the like. Kwa style hii utachoka sana kwa sababu "PEOPLE SPEAK AT PEOPLE NOT TO PEOPLE" , maana hata hao wateule wako, kwa hakika hujui undani wao! Kwa mifumo mizuri ya utawala utaujua undani wao na hawatakuhangaisha
hataki kuwa overshadowed na wasaidizi wake,anataka asifiwe yeye tu!
 
Kwa sababu anafanya kazi lakini kwa MAFISADI wengine ingekuwa kazi raisi sana. FISADI KAMA LOWASSA INSINGEMPA SHIDA KAZI HII YA URAISI HATA KIDOGO. EE MUNGU WA REHEMA MLINDE MJA WAKO NA UMPE AMANI YA KWELI ITOKAYO KWAKO.
Fallacious arguments.
 
Ni Bora amekiri kuliko kukaa kimya Jambo la msingi ni kuwa na washauri wazuri na akipewa ushauri ajiridhishe kabla ya kuufanyia kazi, Amwombe Mwenyezi Mungu amwongoze vyema katika majukumu yake.
 
Kuna siku nilihoji tamko la Rais kuwa hakujiandaa kuwa Rais! Watu walinizomea sana! Sasa leo ametoa tena kauli ya kushangaza kuwa anajuta kuutaka Urais...!

Hivi hili halina uhusiano na kauli kuwa hakujiandaa kwa majukumu haya... Kwa maneno yake "alikuwa anabeep! :-
Hakuna tatizo mara nyingi sana katika maisha hutokea,, unafikiri unaweza kuota huko kukoje? Kuna Tajiri mmoja aliwahi nambia najuta kuwa tajiri, unaweza ukadhani anatamania kila jambo lina faida zake na hasara zake, Ukizingatia Raisi huyu alikuja na moyo tofauti na mfumo uliopo. Mfumo ulikuwa unatoa nafasi ya kujijenga mwenyewe yeye kaja na mfumo anotaka ajenge na za wengine na uweke uwajibikaji, usawa, apunguze gap la walionacho na wasio nacho hapo hapo anatamani tuwe kama china kwa miezi michache aliyokaa. Ana waza vitu vikubwa zaidi kuliko muda uliopo, kila sehemu kumevurugika hajui aweke priority ipi na ipi kwanza labda italeta nafuu.
 
Back
Top Bottom