Mmemsikia Kikwete......?! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mmemsikia Kikwete......?!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Wa mmoja, Aug 7, 2009.

 1. Wa mmoja

  Wa mmoja Member

  #1
  Aug 7, 2009
  Joined: Aug 4, 2009
  Messages: 99
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mheshimiwa anasema Wizara ya Miundo Mbinu ikiwezekana ibadilishe sheria kwamba dereva atayesababisha ajali na kuua abiria anyang'anywe leseni,akatafute kazi nyngne ya kufanya!!!
  Jamani wana JF hii si inaweza ikaongeza majambazi nchini?
  Nyi mnaionaje hii kitu?
   
 2. b

  bnhai JF-Expert Member

  #2
  Aug 7, 2009
  Joined: Jul 12, 2009
  Messages: 2,207
  Likes Received: 1,373
  Trophy Points: 280
  kwani nchi zilizoendelea wanafanya nini? Watu wanakufa saana. Zichukuliwe hatua sasa. Vyuo binafsi vimeshindwa kusomesha madereva, labda serikali iboreshe VETA na watu wakasome huko. Suala la kunyang'anya leseni ni jema kabisa kuna watu wanaamka mayatima kwa sababu ya uzembe wa mtu mmoja, miundo mbinu inaharibiwa, watu wanapata ulemavu, insurance company zinafilisika. No way lazima kupambana na madereva na ikibidi wanyang'anywe leseni
   
  Last edited: Aug 7, 2009
 3. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #3
  Aug 7, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Na anayeingiza nchi kwenye mikataba mibovu inayoumiza mamilioni ya wananchi je afanywe nini, au amefanywa nini?

  Je kuna Dereva anaepanga kuua kwa kudhamiria?
  Lakini mambo ya kifisadi yote yanapangwa vizuuri mezani, watu wanabipiana wee, hadi wakubaliane dau! , je wao wafanyweje?

  Mi nakwambia, sheria hizi za jinai zinawalenga watu wadogo!

  Hiyo ndo jino kwa jino au tit for tat kwa watu wa hali ya chini!

  Shauri zenu, chekeni nae!
   
 4. Mponjoli

  Mponjoli JF-Expert Member

  #4
  Aug 7, 2009
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 668
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Kwani ukisikia kazi nyingine unadhani ni ujambazi tu? Watu wanaweza kwenda kufanya kazi nyingine nje ya ujambazi. Huyo anaeacha udereva anaenda kuwa jambazi ujue hata kabla hiyo kazi alikuwa anaifanya au alikuwa anataka kuifanya.

  Hatuwezi kuendelea kuvumilia watu wanaangamia kwa ajali kila kukicha. Madereva ni moja ya sababu za ajali na wadhibitiwe.
   
 5. M

  Magezi JF-Expert Member

  #5
  Aug 7, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Ni kweli ndugu yangu mbona watuhumiw wa richmond anawachekea tu? Kwa nini asiwanyang'anye leseni ya kazi (kuwafukuza kazi)? Niliwahi kutembelea Norway lakini cha ajabu wakati nasafiri kwenye basi dereva alikuwa ana hakikisha havuki speed 80km/hr na wala hatukuwa na askari ktk basi. Nilimuuliza nilipofika kwa nini hawezi kwenda zaidi ya speed hiyo akasema gharama atakayolipa akikamatwa ni kubwa bora achelewe njiani.

  Sisi hapa TZ tunachekesha tu eti utakuta traffic pollice wapo kwenye basi kumdhibiti dereva, huu ni ujinga!! weka sheria kwamba "over speedig faini yake ni US $ 500 na kunyang'anywa leseni" uone kama mtu atathubutu. Kwa sababu Norway kwa mwaka 2007, faini ilikuwa NOK 300 na kunyang'anywa leseni.
   
 6. Komamanga

  Komamanga JF-Expert Member

  #6
  Aug 7, 2009
  Joined: May 2, 2009
  Messages: 221
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33

  Mimi kwa mawazo yangu hii imekaa sawa ila sasa kusema kwamba wakafanye kazi nyingine ina maana wanakuwa hawanamashtaka ama hapa sijaelewa vilevile nafikiri kumyang'anya mtu leseni naona ni poa zaidi na kama ndio wataingia kwenye ujambazi basi polisi wafanye kazi yao.
   
 7. Kaka K

  Kaka K Senior Member

  #7
  Aug 7, 2009
  Joined: Feb 9, 2008
  Messages: 129
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hata ikiwezekana nani wa kusimamia hiyo sheria?....naamini kabisa sheria zilizopo zikisimamiwa kwa ukamilifu hii itapungua kwa silimia kubwa sana....

  mpaka siku siasa itakapo acha kuingilia kila jambo ndo tutaona maendeleo...vinginevyo kufa kama kawaida tu....kisha gov itatoa rambi rambi.
   
 8. M

  Malyamungu JF-Expert Member

  #8
  Aug 7, 2009
  Joined: Jul 5, 2009
  Messages: 363
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hapa ni kuvifuta vyuo vya udereva na kuanzisha kitengo cha udereva ndani ya TANROADS kiwe na examiners wao waliobobea.

  Polisi isijihusishe na utoaji wa leseni bali leseni itolewe chini ya uangalizi mkubwa wa Mamlaka ya barabara ambao ni Tanroads. Kwa hiyo TANROADS iwe ni mamlaka moja yenye mtandao mkubwa kwani barabara zinajengwa na wao na ndo watakaoweza kujua thamani za ujenzi wa bara*2. Na leseni ziwe za kutambulika kwa komputer ziwe za kadi.

  Polisi tutakutana nao kwenye ukaguzi na kunyanganyana hizo leseni barabarani.

  Mheshimiwa JK kama tunaweza kugharamia vitambulisho vya taifa je ni hizo leseni ambazo kila mtu atalazimika kulipia ndiyo aipate??
   
 9. M

  MpendaTz JF-Expert Member

  #9
  Aug 7, 2009
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 1,579
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Huku ndiyo kufanya maamuzi ya juu juu yale yale ya uswahili. Kwanza inatakiwa kuangalia pande zote, sababu na uawezekano gani upo wa ku-monitor tabia za madereva wanapokuwa barabarani. 1. Kuna haja ya kuhakikisha kuwa watoa leseni wanazitoa baada ya kuridhika kuwa dereva amepata mafunzo ya kutosha na anapata leseni yenye uzito wake.
  2. Polisi wa barabarani wanatakiwa nao wawajibishwe kuwa wamechukua hatua gani za kuhakikisha madereva wanakuwa "monitored" ili kupunguza hizi ajali
  3. Ndipo adhabu kali iwekwe ikiambatana na kushitakiwa, kufungwa na kunyanganywa leseni ya kuendesha magari ya abiria. Aachiwe ya kuendesha tractor tu au lori kutegemeana na uamuzi wa mahakama.

  Lakini muhimu zaidi ya yote ni kuhakikisha kuwa wanapata mafunzo ya kutosha na motisha iwe ni kupanda kiwango na mishahara kutokana na takwimu ya miaka ya kazi na namba ya abiria-kms aliobeba na kutembea. Maamuzi ya juu juu hayatatui matatizo kwenye jamii. Hii inaonekana kama ni wazo lilitokea kwenye mazishi ya aliyekumbwa na mauti kwenye ajali.
   
 10. F

  Froida JF-Expert Member

  #10
  Aug 7, 2009
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Kasema kweli madereva wanajifanya wako juu ya sheria wanastaili kupewa adhabu kali sana nakumbuka hapa DSM pale mahakama ya kivukoni kulikuwa na hakimu ambaye yeye kila mwenye kosa la barabarani alimfunga mwezi mpaka mitatu mbona alipunguza sana ajali hapa dar
   
  Last edited: Aug 7, 2009
 11. Wa mmoja

  Wa mmoja Member

  #11
  Aug 7, 2009
  Joined: Aug 4, 2009
  Messages: 99
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tatizo lingine linakuja kwamba hawa hawa madereva nasikia huwa wanapewa allowance na maboss wao kama watalifikisha gari mapema na lifike salama...!This means that,dereva atashawishika kulikimbiza gari ili mradi afike mapema ili apate allowance.
  Sasa hii si inachangia kuongezeka kwa ajali?
   
 12. M

  Malyamungu JF-Expert Member

  #12
  Aug 7, 2009
  Joined: Jul 5, 2009
  Messages: 363
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nilitembelea Poland Warsaw, ni kwamba ukifanya kosa hasa la uendeshaji mmbovu ( over speed limit) ukapata ajali au kamera ikakupiga utakapokea barua kutoka posta, hukumu zilishatolewa na zilishaandikwa vitabuni wewe cha kufanya unatangulia magereza kwa kuhudhuria kifungo chako jela na jina lako tayari lilishakutangulia mwanangu.

  Kwa Australia, kwanza unajidhalilisha pili, unalipa faini ya dola kuanzia 200 hadi 1000 average.

  Huwa kuna matatu kwa wakati mmoja-unaporwa leseni, unalipa faini na unatumikia jela kwa muda wa mwaka mmoja na ukitoka haurhusiwi kuendesha gari ya aina yoyote ile baada ya kutoka jela kwa muda miezi sita hadi mwaka. Hata kama umeipata leseni ile na huwezi kuipata kwani you are rrecorded.

  Dereva wa basi wanaheshimika sana ni kazi nzuri mno wanavyosema, they are enjoying alot wanawapenda abiria wao, wanawasalimia wanapoingia kwenye basi mwanangu utafurahi.Wanamnyenyekea abiria aje tena asafiri kwa basi, asipande ndege au treni.

  Walahi bongo bus drivers ana wenge la kufa mtu, hasira matusi, anatukana duu! nimechoka!
   
 13. L

  Lukundo Member

  #13
  Aug 7, 2009
  Joined: Feb 19, 2009
  Messages: 61
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  jamani kwani ulaya wanafanya nini ukisababisha ajari mara tau. wanakunyanganya leseni ambayo ni ghali sana kuipata, uanrudi chuo kuisotea tena wakiwa na maanaa kuwa inawezekana ukawa hujafahamu baadhi ya sheria. hiyo itapunguza sana ajari. tusichanganye makosa, na kusema kwa sababu kosa fulani limetendeka basi menigine yote yatatuliwe kwa njia moja. sio kweli, yanayowezekana, kwa wakati tulionao tuyafanyie kazi leo, kama hili.
   
 14. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #14
  Aug 7, 2009
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,802
  Likes Received: 161
  Trophy Points: 160
  Ni wakati upi kauli za JK zilishawahi kutekelezwa? Hiyo ni funika kombe mwanaharamu apite... Kwani taztizo la ajali za barabarani ni Madereva tu? Haya mabasi mbona yana ratiba kabisa zimepangwa kwamba kutoka kituo "A" mpaka kituo "B" ni muda "t". Mona haya magari yote yamewekewa "stcikers" kwamba yanastahili kutembea barabarani?

  Hiyo kauli ni yale yale tu ya kila kukicha!
   
 15. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #15
  Aug 7, 2009
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Hapo ndipo huwa napata shida sana. Hiyo ni kauli ya rais wa nchi mwenye dhamani ya maisha ya watu karibia milioni 40? Wanaharakati wanasema namna hiyo; PM, mawaziri na viongozi wengine wa serikali nao hivyo hivyo. Hivi nani kwenye nchi hii anaweza kutoa kauli yenye uzito sawa na dhamani aliyopewa? Asipopatikana huyo tutaendelea kutwanga maji kwenye kinu!!

  Simple solution to complex issues! Utadhani kwamba hatujui wenzetu wanafanyaje? Tuna macho lakini hatuoni, tuna masikio lakini hatusikii..!! Sasa kwa nini tunafuja hela za umma bure kutembea huku na kule kama hatuwezi kujifunza kitu? Hii inanikumbusha katuni za "ZERO".
   
  Last edited: Aug 7, 2009
 16. B

  Bunsen Burner Member

  #16
  Aug 7, 2009
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 95
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Unajua factors za ajali ni nyingi tu including kuhakikisha enforcements za sheria barabarani kwa traffic police (sio kuchukua rushwa tu na kuachia walevi nk.), pia factors zingine ni kama road designs za bongo ambazo kwenye steep condition hazi allow extra climbing lanes for slow traffic kuwesha gari zingine ku overtake badala ya kuslow smooth movement of traffic, kama ambavyo huku Southern Africa barabara nyingi wanafanya na inasaidia sana kuepuka ajali za overtaking!
   
 17. The Native Son

  The Native Son Member

  #17
  Aug 7, 2009
  Joined: Jul 14, 2009
  Messages: 87
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 15

  Kuwanyang'anya leseni mimi sioni kama ni issue kubwa sana kwa dereva wa Tanzania. Sijui kama Bw JK amewahi kujiuliza hizo leseni wanazipataje maana kwa Tanzania asilimia kubwa unapata kwanza leseni alafu ndio unajifunza gari.
  Nionavyo mimi sasa, hata ukichukua leseni kwa kuwa mfumo wa ufuatiliaji hauko vizuri, dereva anaweza akapata leseni nyingine na kuendesha gari kama kawaida alafu leseni haindeshi gari kwa Tanzania, gari anaendesha mtu ndio maana utakuta miji kama Dar Es Salaam watu wengi wanaendesha magari bila lesini kitu ambacho ni tofauti na miji mikubwa ya nchi nyingine.
   
 18. Mopao Josee

  Mopao Josee JF-Expert Member

  #18
  Aug 7, 2009
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 280
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Na anayeingiza nchi kwenye mikataba mibovu inayoumiza mamilioni ya wananchi je afanywe nini, au amefanywa nini?

  Je kuna Dereva anaepanga kuua kwa kudhamiria?
  Lakini mambo ya kifisadi yote yanapangwa vizuuri mezani, watu wanabipiana wee, hadi wakubaliane dau! , je wao wafanyweje?

  BRAVO
  `nyani haoni kundule`
   
 19. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #19
  Aug 7, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  We have to understand that life is unreplaceable and/or irreparable, this must be fully settle in the minds of drivers. When you cause an accident which expires life, you must understand that the one you killed is a father or mother or uncle or etc of somebody, and this person may be is the pillar of the family. By killing such a person, you have killed and distroy the whole family, in its entirety. As such, the GOV must put into place traffic laws that will be harsh to reckless drivers and insurance companies that insured the driver/car.

  To my opinion, Mr. President is correct when he said whatever he said regarding drivers who are killers. Let them go and find another jobs, to wit.
   
Loading...