Mmea wa Mbuyu Unatakiwa Kuzalishwa Kwa Wingi- Wizara | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mmea wa Mbuyu Unatakiwa Kuzalishwa Kwa Wingi- Wizara

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Dec 11, 2009.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Dec 11, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  Mmea wa Mbuyu Unatakiwa Kuzalishwa Kwa Wingi- Wizara

  [​IMG]
  Tuesday, February 10, 2009 11:27 PM

  [​IMG]
  [​IMG]  MMEA wa zao la mbuyu unatakiwa kuzalishwa kwa wingi nchini kutokana na kugundulika kwa kutoa faida nyingi kwa binadamu na rasilimali ya nchiRai hiyo imetolewa hivi karibuni Bungeni Dodoma, na Wizara ya Maliasili na Utalii, kupitia Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Ezekiel Maige.

  Maige alisema kuwa mmea huo, umegundulika kuwa na faida nyingi sana katika maisha ya kila siku ya binadamu hasa watanzania.

  Alisema kutokana na kugundulika kwa faida nyingi kwenye zao hilo Serikali kupitia wizara ina mikakati ya kuongeza uzalishaji wa zao hilo ili kuweza kuongeza uchumi mzuriwa nchi na ni zao la biashara.

  Alizitaja faida zinazotokana na mmea huo, na kusema mbuyu unaweza kutoa mafuta ya kupikia, kujipaka, kulainisha ngozi na kuzifanya kucha zimeremete na kuwa ngumu.

  Vilevile amesema mmea huweza kutumika kama chakula kinachotoa Vitamini B, Vitamin A inayosaidia kuona macho kwa ufasaha, Vitamini C inayosaidia ukuaji wa fizi, meno, ngozi na misuli.

  Alisema kuwa katika tafiti zilizofanyika na wataalamu mbuyu unaweza kutumika kama dawa ya kutibu magonjwa kama vile kisukari, surua, ngozi, meno ,fizi, kuhara na magonjwa ya moyo.

  Na unga wa majani na matunda ya mmea huo hutumika kama kiungo cha kuongeza ladha kwenye chakula.

  Na matunda yake hutumika kutengenezea juisi nchini katika mikoa mingi nchini zaidi mikoa ya Singida, Dodoma na Shinyanga, na baadhi ya wananchi hutumia matunda hayo kujikwamua kiuchumi kwa kutengenezea biashara ya Icecream.

  Pia mbuyu hutoa nyuzinyuzi ambazo hutumika viwandani kutengeneza kamba, pia mti wenyewe wa mbuyu hutumika kutengeneza karatasi na boti za kuvulia samaki.

  Hivyo kwa kufuatia faida hizo Waziri Maige amesema Serikali inahimiza utunzaji wa mti huo kutokana na umuhimu wake kwa kuhifadhi mazingira.

  Na alisema kuwa wakala wa mbegu nchini wanafanya majaribio ya kuotesha mbegu za mti huo kwenye baadhi ya mikoa ambayo haina miti hiyo kuona kama itaweza kuzalishwa katika mashamba ya kilimo.
   
 2. Mtoto wa Kishua

  Mtoto wa Kishua JF-Expert Member

  #2
  Dec 11, 2009
  Joined: Oct 15, 2009
  Messages: 819
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 45
  Pamoja na Mwarobaini, vyote hivi vitakuwa ni zao muhimu sana kutoka Tanzania
   
 3. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #3
  Aug 27, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,135
  Likes Received: 6,628
  Trophy Points: 280
  Heshima mbele mkuu,
  Naomba faida za mafuta ya huu mmea wa mbuyu mkuu.

   
Loading...