Mme wangu, njoo tuanze kujenga familia.

blessedme

Member
Nov 23, 2018
37
125
FINAL UPDATE.
Nimeelemewa, nawashukuru sana kwa kuchukua mda wenu na kusoma bandiko langu.
PM zimekuwa nyingi mnoooo, nashindwa hata nianzie wapi, I didn't see this coming at all. Nilijua zitakuwa chache.
Ambao mlichelewa ona bandiko poleni sana, ila kwa sasa sipokei PM nyingine tena.
Nimeireport hii thread ifutwe, ikifutwa sawa, isipofutwa sawa. Ila mi sina uhitaji nayo tena. Nawapenda ovyo.
 

Tunzo

JF-Expert Member
Feb 1, 2013
3,720
2,000
Kila laheri, ila hizo sifa na huo umri, nikifikiria na wanaume wa jf mmh sisemi mabaya ila kuolewa hapo unaweza ufike 33yrs bado utakuja kuomba uchumba humu.
 

jurist

JF-Expert Member
Dec 15, 2013
278
500
Habari za weekend wanajukwaa.
Toka jumatatu nimekuwa nikijiuliza ni siku gani na mda gani nitaweza kuanzisha hii thread, lengo langu lilikuwa niianzishe siku ambayo watu wengi watapata nafasi ya kuipitia. Na leo nikaona ndo itakuwa siku sahihi.
Nimeamua kutumia id hii, well sio mpya sana ila ni ngeni ili niruhusu nafasi ya kujielezea, kujibu maswali kama nitaulizwa na kuwa huru.
Kiukweli mi ni member mzoefu humu ndani, nawajua members wengi. Kupitia JF nimepata marafiki mbali mbali, na nimeweza kukua kifikra.

SASA TURUDI KATIKA TITLE
Nimefikiria saaana, na kwa umakini sana, nikiwa na akili timamu kabisa nikaamua kuwa nahitaji kuolewa na mtu wa JF. Nitawapa sababu zifuatazo.
Humu JF ni sehemu ambayo tunadiriki kuwa wawazi, mtu akiwa JF seriously lazima awe na uelewa sio kwenye mambo ya nchi ila hata kwenye mahusiano najua atakuwa anajitambua.
Sio kwamba huku niliko hakuna wanaume, ila niliotoka nao naona hawana vitu ninavovihitaji in a man so unfortunately huwa naishia kuachana nao. Wengine wamediriki kunambia fani ulosomea tutaishia kushindwana (like seriously??) So naamini Mme wangu yupo hapa.
MIMI NI NANI
Mimi ni binti wa miaka 27, dini yangu ni mkiristo RC, ni wakili, well mi ni mrefu kiasi, mweusi kiasi, mchangamfu sana sana sana, huwezi kuwa bored tukiwa tunaongea, msafi, najua kupenda. Sijisifii ila kiukweli hakuna ex wangu ambaye atapinga, ninajali sana shida yako naichukulia kama yangu, sina shida ya ela ndogo ndogo, bado nina wazazi na ni last born katika familia ya watoto watatu. Najua kupika, na najitegemea kimaisha. Nipo Dar.

SIFA ZA MTU NINAYEMHITAJI.
Kama nilivosema hapo juu, sio kwamba huku mtaani sitongozwi ninatongozwa saaana tu. Sema sijaona mtu mwenye sifa ninazohitaji. Mtu ninayemhitaji inabidi awe na sifa zifuatazo.
1. Asiwe na wivu kabisaaa, hiki kwangu ni cha muhimu maana asilimia kubwa ya watu wa field yangu ni wanaume. Sitaki mtu wa kunisakama na kunifanya minute kusomea sheria.
2. Awe na elimu. Kwakweli ambao hamjasoma naomba mnisamehe, hata kama una hela kama hujasoma utakuwa msumbufu mno. Ni bora uwe na elimu atleast ya degree.
3. Asiwe mtu alosomea ualimu au mass communication. Nyie watu ni walalamishi naomba mnisamehe.
4. Awe na kipato, sio lazima kikubwa ila atleast aweze kujihudumia na kuihudumia familia yake( tukiwa na watoto) mi sina shida ya hela, so asiumize kichwa kuhusu mimi.
5. Awe mrefu, hapa nasisitiza. Sio habari za joti kuwa kila mtu ni mrefu inategemea na ulosimama nae, kwangu mimi awe mrefu. Atleast futi 5.8 na kuendelea. Wanaume wafupi mna hasira za karibu siwawezi.
6. Swala la usafi sio tatizo, ni kazi yangu kumhudumia Mme wangu we njoo ila ujue kuoga. Nitakubadili maana naamini katika kubadilika.
7. Apende style mbali mbali za fashion, maana nitakuwa namvalisha, namfanya anukie nampendezesha hadi balaa. Hii sio tatizo kubwa, cha msingi awe tayari kubadilika.
8. Asiwe bahili, mi napenda kujali, kununua vizawadi, kudekezwa, yaani Asiwe mshamba. Siku nyingine tunatoka out. Yaani hivo.
9.AJUE KIINGEREZA, natia msisitizo.
10. Naomba anizidi umri hata miaka mitatu, nitatoa maelezo hapa, mimi nina IQ kubwa, nahofia akiwa ndogo nitakuwa namoverdose mtoto wa watu.
11. Awe tayari kubadilika katika kuwaza maisha, mi nitamsaidia kumshauri na tutakuwa na biashara nyingi tu.
12. Hapa naomba msinifikirie vibaya ila naogopa mtu mwenye majukumu mengi ya kifamilia, sijui una ndugu 20 wanakutegemea sitaweza, mimi sina mtu anayenitegemea so akiwa na wategemezi naomba wasiwe kijiji.
13. Napenda zaidi akiwa mtu wa dar ila wa mkoani uwe na uhakika wa kuniona kila baadae ya wiki 2.
14. Asiwe mwembamba jamani, na asiwe mnene sana, asiwe mweusiiiiii wala mweupe.
15. Asiwe mwanasheria.

SIFA ATAZOPATA.
Mapenzi kama yoote. Mi ni full package kwenye kudekezwa, kudekesha, kupenda, mapenzi baba mda wote utapata, heshima nipo, ushauri nipo, yaani utakuwa mtu mwenye bahati kuwa na mimi. Na nipo tayari kutoka JF akinikataza.

NOTE.
Sio kila anayetafuta Mme au mke humu yupo desperate, wakati mwingine tunajaribu kwenda extra miles kupata wale tunaowataka. Mme wangu nakuhitaji, nakuombea kila siku, njoo uwaone wakwe zako na mimi niwaone wakwe, mawifi na mashemeji zangu. Nakupenda sana. Kwayeyote aliye interested karibu PM, ila uwe tayari kuulizwa maswali, maana napenda tuwe marafiki kabla hatujaingia katika mahusiano.
Kama nilivosema nawajua sana wavulana wa humu, ukija kichwa kichwa ntakutukana. Kingine nina tako la wastani.Sent using Jamii Forums mobile app
No. 15 imekukosesha bahati mama

#ESQUIRE
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom