Mme wangu alinigeuza DISPLAY kwa hawara yake hotelini bila mimi kujua | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mme wangu alinigeuza DISPLAY kwa hawara yake hotelini bila mimi kujua

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by MBILIA, Oct 20, 2012.

 1. M

  MBILIA Member

  #1
  Oct 20, 2012
  Joined: Oct 13, 2012
  Messages: 33
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Baada ya sherehe iliyomhusu, mme wangu June 2012, alitoa ofa ya chakula cha jioni kwa familia na wageni wetu. Tulipofika pale hotelini tuliwakuta wadada wa2 wa kiafrika, (Ile ni hotel ya kichina). baada ya dk7 hivi wale watoto wakaondoka kwa miondoko iliyotufanya tucheke.

  juzi nimesaidiwa na wajuzi wa mambo ili niweze kumwona aliyeongea na mme wangu saa 5 za usiku na kisha kuahidiana kukutana airport. Yule binti akamwelekeza mwenye kunisaidia (kijana kwa kutumia simu ya kimapenzi, yule kijana alijifanya amewahi kumwana na alimpenda) kuwa yeye alikuwa darasani ktk chuo kimoja hivi. tukaenda huko. Nilichoka sana baada ya kumkumbuka dada huyu kuwa ndiye aliyekuwa hotelini na mwenziwe. kwani hata hapo chuoni walitoka wote wawili.

  Lililonisukuma kusema ni hili. inaniuma mme wangu kwa miaka 21 sasa (ondoa ya uchumba) amenigeuza DISPLAY
   
 2. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #2
  Oct 20, 2012
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,591
  Likes Received: 801
  Trophy Points: 280
  Unaonaje, ukimshtakia Mungu?
  Maana hapa zaidi ya kukuambia piga goti chini sioni kama kuna msaada mwingine wowote.

  Chochote uakachoamua you need God; remember you and God are the majority.
   
 3. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #3
  Oct 20, 2012
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,037
  Trophy Points: 280
  kuanzia hapo kwenye....'juzi nimesaidiwa...' umeniacha njia panda shosti.....sijakuelewa....
   
 4. TIQO

  TIQO JF-Expert Member

  #4
  Oct 20, 2012
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 13,832
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 0
  Hadithi ya kusadikika
   
 5. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #5
  Oct 20, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,874
  Likes Received: 6,228
  Trophy Points: 280
  na wewe mgeuze display
   
 6. happiness win

  happiness win JF-Expert Member

  #6
  Oct 20, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 2,478
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 0
  Hiyo ndiyo shida ya kumchunguza sana kuku. Inaonekana humuamini mumeo na unaelewa fika anaenda isivyo. Kitendo cha kutafuta mtu wa kukusaidia kuwaona wapenzi wa mumeo kinahitaji KIFUA. Ona sasa, unaanza kuhaha baaada ya kujua ukweli, huoni ni hatari kwako? utakufa kwa presha na kuwaacha wengine wanamfaidi.

  Sijasema usimchunguze mumeo, mchunguze kwa uwezo wako wa kuhimili matukio. Ungeweza kumuonya mumeo kwa ushahidi wa kumkuta akiongea na simu usiku, ila kumuwekea watu na kuwaona wabaya wako.... yatakata moyo! kuna wengine hufika hadi gesti kufumania na huishia hospitali mahututi presha juu!
   
 7. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #7
  Oct 20, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  display........???? hii mupya....bado double screen tu lol
   
 8. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #8
  Oct 20, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  mmmhh, pole.

  Hisia hazigawanyiki, lazima mtu atajikanganya tu mahali.
  Tafuta cha kukufanya uwe bize, kama hufanyi jitolee kazi za kanisani.

  Kuwa bize tu kwa sasa.
   
 9. Baba V

  Baba V JF-Expert Member

  #9
  Oct 20, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 19,507
  Likes Received: 170
  Trophy Points: 160
  au yeye amfanye keypad!, mzima wewe BADILI TABIA,mbona sijakuona huku makirikiri?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 10. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #10
  Oct 20, 2012
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,591
  Likes Received: 801
  Trophy Points: 280
  Kongosho, this is our famous Mke ya jaji; ushauri mlimpa wakuzidi tu. So nafikiri anahitaji kufanya maamuzi tu!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 11. Janjaweed

  Janjaweed JF-Expert Member

  #11
  Oct 20, 2012
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 9,531
  Likes Received: 884
  Trophy Points: 280
  I think Mbilia kinamna ni mtu aliyekuja kumchafua mtu na hakuna cha mume wala nini

  something fishy stinks here
   
 12. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #12
  Oct 20, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  namkumbuka sana.

  Ndio maana namshauri, kama hana kazi aanze kujitolea zile za kanisani, awe bize kwa muda kwanza wakati anatakari achukue maamuzi gani.

   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 13. nyumba kubwa

  nyumba kubwa JF-Expert Member

  #13
  Oct 20, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 10,280
  Likes Received: 1,720
  Trophy Points: 280
  Utakuta vimada kwa vimada wanachafuana...mke halali wa Mheshimiwa jaji kajituliza ndani...Si unajua tena mtu akijua buzi lake linakaribia kukata kamba; Ila ukweli lazima utakuwepo though anaye report kuwa wife anaweza asiwe wife ila yuko well informed kwa kuwa ni kimada.

  Pole Mbilia; kwa kuwa tunatumia fake IDs hapa ni ngumu kukuamini kama kweli wewe ni mke halali....maana tulishakushauri na hujatupa feedback unaleta uzi mwingine uso na kichwa wala miguu.
  Ukizingatuia kama ni kweli ulisema una miaka 50...muda wa kufuatilia upuuzi huu unapata wapi...wewe tulia kama hauko tayari kufanya maamuzi magumu.


  Unajua mwanaume mwenye vimada wngi ni rahisi wao kwa wao kugombana na mwingine kupozi kama wife; ili kuwalipua wenzie.

  Nina mfano wa mume wa rafiki yangu...aligombanisha vimada wakati mkewe masikini ya Mungu anaangalia tu picha inavyochezwa kwa kuwa ni mpole kupindukia.

   
 14. C

  CHUAKACHARA JF-Expert Member

  #14
  Oct 20, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 12,206
  Likes Received: 3,828
  Trophy Points: 280
  Mbilia, kama walivyoshauri wengine. Unatakiwa kuamua kati ya haya:
  1. Kama umezaa, kaa uwalee watoto wako. Mwone kama siyo mume wako, uko pale kwa vile una watoto na mchango wako katika matrimonial properties-hapo ni kwako. USIMPE UNYUMBA katu.
  2. Kubali fact kuwa mme wako ni mzinzi na mkusanyioe ushahidi wa kutosha dai talaka na mgawame mlicho nacho uanza maisha yako.

  Najua yote hayo ni magumu kutekeleza lakini inafika mahali unachagua moja katika mabaya. Kwa miaka 22 ya ndoa halafu anafanya upuuzi hatabadilika!
  Nilimshauri shemeji yangu alikuwa na hali kama ya kwako alichagua namba 1. She is happy now maana aliuzoeza moyo kuwa hana mume. mwanzoni ilikuwa tabu kidogo.
   
 15. Janjaweed

  Janjaweed JF-Expert Member

  #15
  Oct 20, 2012
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 9,531
  Likes Received: 884
  Trophy Points: 280
  Yes kabisa

  Hapa mtu kachezewa sasa inauma mzigo unatoa nanga, anahangaika sana kwasababu alipata access ya simu na kila mwanamke humo ndani anaamua kumchafua... THIS DOESNT HELP WOMEN!!! THEY SHOULD STAND UP AND FIGHT THESE BUGS IN THE SOCIETY

  ANAJIMALIZA, ANAWACHAFU WANAWAKE WENZAKE, IN THE NAME OF LOVE
   
 16. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #16
  Oct 20, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  We una akili sana
  huyu hataki kushauriwa
  yuko kutoa matangazo hapa..
  na si ajabu akapa kidumu hapa huko pm..
  sababu keshaanza kuwa maarufu pia
  ana enjoy u celeb wa jf i guess..
   
 17. M

  MBILIA Member

  #17
  Oct 20, 2012
  Joined: Oct 13, 2012
  Messages: 33
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nashukuru sana kwa michango yenu. Ijulikane kuwa mtu akimtaja mtu jua mtu huyo huko sahihi. Pia michango yenu yote ndiyo naifanyia kazi. Sikujua kuwa mabaraza ya upatanishi yanahitaji kwanza barua toka mwenyekiti wa mtaa, yote ni ushauri wenu mzuri sana.

  Ila si vibaya kuwajulisha wenye ndoa kuwa wajue kuwa wanaweza kugeuzwa display na wenzi wao wasio waaminifu. Na pia jambo hili linakuwa si jema. Kwa anaeniambia sina la kufanya, kwa taarifa nina miradi mingi mno ambayo naajili watu
  kufanya ili mimi nipate mda zaidi wa kujiendeleza na si kukaa ofisi tuuu, elimu yangu si kwa ajili ya kuajiliwa bali kuajiri.
  Miradi kama nyumba za kupangisha unataka nikawaangalie wapangaji?

  Pia hapa sipo kumchafua mtu, anyejihisi nimemchafua nasikitika kusema kajichafua mwenyewe. Ila dhambi usiitetee iseme kama waasemavyo wahubiri ili isifanywe tena.
   
 18. Chauro

  Chauro JF-Expert Member

  #18
  Oct 20, 2012
  Joined: Aug 20, 2010
  Messages: 2,969
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  dada wewe ni mke wa ndoa kweli?

   
 19. k

  kamusi JF-Expert Member

  #19
  Oct 20, 2012
  Joined: Aug 9, 2012
  Messages: 1,081
  Likes Received: 170
  Trophy Points: 160

  POLE mwaya, najua maumivu yake yakoje.. watu hawajui uchungu na maumivu ya kusalitiwa yakoje mpaka na wao yawakute japo mara moja ndio wataelewa..
  kaa chini na mume wako umueleze mwanzo mwisho..tumia busara, ongea kwa upole sana na wala usitumie ukali na lugha chafu..kama kwa sasa una hasira, basi subiri mpaka hasira zitakapopungua..ni vizuri maongezi hayo ukayafanya nje ya nyumbani kama hoteli hivi..ikibidi mlale hukohuko siku hiyo...
  mwambie kama yuko tayari kuendelea na ndoa basi amuache huyo binti..mpe masharti kadhaa ambayo unaona yanafaa...endelea kumfuatilia baada ya hapo ili kuona km amebadilika au la.

  kama akikubali basi msamehe mume wako, na muendelee kuishi kama mke na mume..wakati mwingine ni shetani tu mamangu, na visichana vya siku hizi huwa havisubiri kutongozwa bali vinajipitishapitisha kwa waume zetu, hasa wakiona kuna chochote(which is obvious)
  usimuache mume wako wa miaka 21, ni muda mrefu, mkalishe chini na muongee, muyamalize wenyewe..ninyi mumeshakuwa watu wazima...nawe kwa upande wako tazama madhaifu yako, inawezekana kuna kasoro 2-3 ambazo zimemboa akaamua kwenda nje..mwambie mumeo akueleze mapungufu yako ujirekebishe..

  Hayo ni majaribu tu ya maisha ya ndoa mamangu, usikate tamaa, amini nakwambia mkivuka kivuko hicho mtaishi maisha ya amani sana(km mumeo atajirekebisha)..kila mmoja kati yenu atakuwa makini na upande wake na kuangalia mapungufu yake na kujirekebisha..mara nyingi ndoa inakuwa imara sana baada ya misukosuko mikubwa kama hiyo..
   
 20. nyumba kubwa

  nyumba kubwa JF-Expert Member

  #20
  Oct 20, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 10,280
  Likes Received: 1,720
  Trophy Points: 280
  Tunaelewa ila ametushangaza kwa kuwa alishakuja na ma evidence ya kutosha humu...tumejua sasa anafanyia kazi...

  Sasa anarudi square one...kama alikuja humu na gia ya kuuliza talaka inadaiwaje...leo hii anafuatilia vibinti vya chuo...si ndo hata sie mabingwa wa kufuatilia waume zetu tunaanza ku doubt...mtu kama umeshamtoa kwenye mahesabu yako unamfuatilia wa nini tena???


  Labda aseme anataka kurudisha mapenzi ya mumewe tumpe ushauri mwingine...tatizo keshasema yeye hana shida na mume anataka process gani afuate kudai talaka...sasa leo hii anaenda tena kwa vibinti vya chuo kufuata nini na mume hamtaki tena?

  Au amegundua ushaidi alonao hauna mashiko ndio anaendelea kudunduliza ma evidence.


   
Loading...