Mmasai Ang'oa Toto la Kizungu, Wazazi Wamtenga | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mmasai Ang'oa Toto la Kizungu, Wazazi Wamtenga

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Felixonfellix, Apr 29, 2010.

 1. Felixonfellix

  Felixonfellix JF-Expert Member

  #1
  Apr 29, 2010
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 1,680
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  [​IMG]
  Binti wa Kiingereza Colette Armand kulia akiwa na mume wake mtarajiwa Meitkini
  Binti wa Kiingereza ambaye kutokana na utajiri mkubwa wa baba yake, alizoea maisha ya kifahari akisafiri nchi mbalimbali duniani, ameangukia kwenye penzi la kijana wa kimasai nchini Kenya na kuamua kuolewa naye na kusababisha wazazi wake waamue kumtenga kupinga uamuzi wake huo.Binti wa Kiingereza Colette Armand mwenye umri wa miaka 24 alizoea kuishi maisha ya kifahari akisafiri nchi mbali mbali na kukaa kwenye hoteli za kifahari.

  Hata siku moja hakuwahi kufikiria kwamba siku moja angeangukia kwenye penzi la kijana wa kimasai anayeishi porini ambako hakuna umeme wala maji.

  Baba yake Colette ni mfanyabiashara mkubwa na mkurugenzi wa kampuni moja kubwa ya madini ya nchini Uingereza wakati mama yake ni nesi katika hospitali moja nchini humo.

  Mkasa wa mapenzi wa Colette ulianza miaka mitatu iliyopita wakati Colette alipoacha masomo yake ya chuo kikuu jijini Paris, Ufaransa na kuamua kuja Afrika kufanya kazi za kujitolea kwenye mashirika ya hisani.

  Colette bila ya kumwambia mtu mwingine yeyote zaidi ya mama yake, ndani ya wiki moja aliacha shule na kufunga safari hadi Nairobi, Kenya kufanya kazi ya kujitolea kwenye taasisi ya watoto yatima.

  Colette alitokea kupendwa kwenye taasisi hiyo ya yatima kutokana na jinsi alivyokuwa akijitolea kwa moyo wote kuwasaidia watoto yatima.

  Colette alijipatia umaarufu wa ghafla baada ya mtoto wa miaka tisa aliyejulikana kwa jina la Mumbe ambaye hakuwahi kuongea hata siku moja kabla ya kuwasili kwa Colette, alipotamka neno la kwanza kumwita Colette "Mama".

  Colette alijipatia umaarufu mkubwa kutokana na tukio hilo akihesabika kama mtu mwenye miujiza.

  Umaarufu huo ulipelekea chifu wa kimasai Kehmini kukitembelea kituo hicho cha yatima na kumpa mwaliko Colette wa kuitembelea jamii ya wamasai.

  "Nilipofika nilionyeshwa kibanda ambacho kilikuwa hakina hata mlango, kulikuwa hakuna umeme wala maji", alisema Colette.

  "Usiku sikulala kabisa nikihofia nyoka wataingia ndani na kunigonga, nilikuwa nikisiliza sauti toka kila kona kuhakikisha niko salama", aliongeza Colette.

  "Maji ya kuoga nayo yalikuwa ya tabu nilishindwa kuoga kwenye mto kwa kuhofia mamba. Niliamua kuchota maji na kisha kuyachemsha kabla ya kuoga".

  "Hata hivyo nilitokea kupenda maisha ya kimasai, wanaume wakiondoka asubuhi kwenda kuwinda wakiacha wanawake wakilea watoto, jioni tulikusanyika pembeni ya moto na kupiga stori", alisema Colette.

  Ulikuwa ni wakati huo ndipo Colette alipoangukia kwenye penzi motomoto na kijana wa kimasai Meitkini mwenye umri wa miaka 23.

  Colette alimaliza miezi akiishi kwenye boma la wamasai mpaka mwaka 2008 yalipotokea machafuko ya kisiasa nchini Kenya ambapo alishauriwa na maafisa wa umoja wa mataifa arudi kwao kwakuwa maisha yake yatakuwa hatarini kutokana na rangi yake.

  Colette alikata shauri atumie muda huo kurudi Uingereza kumalizia masomo yake ingawa kutokana na mapenzi aliyo nayo ilikuwa vigumu kwake kuishi mbali na Meitkini.

  Colette alirudi Uingereza na kumalizia masomo yake akiwataarifu pia wazazi wake na ndugu zake uamuzi wake wa kuolewa na mmasai na kuishi kwenye boma la wamasai.

  Colette hakueleweka katika familia yake na wazazi wake waliliona suala hilo kama skendo na kuamua kutotaka kulizungumzia kabisa.

  Colette ingawa hivi sasa ametengwa na wazazi wake bado ameshikilia msimamo wake wa kuolewa na Meitkini na yupo kwenye hatua ya mwisho ya kumalizia maandalizi ya harusi itakayofanyika siku chache zijazo.

  Kuhusiana na suala la mumewe kuongeza mke mwingine kama jadi ya wanaume wa kimasai ilivyo, Colette anasema kuwa yeye hatajali kuwa mke mwenza ingawa anaamini Meitkini hafikirii kuongeza mke mwingine zaidi yake.
   
 2. MIUNDOMBINU

  MIUNDOMBINU JF-Expert Member

  #2
  Apr 29, 2010
  Joined: Apr 14, 2010
  Messages: 452
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  Mapenzi haya chagui Dini, kabila,wala Mali.Mwenye kupenda haoni ingawa Macho anayo...kumpenda yule bibi msinilaumu penzi la fukara jama halina thamani mbele ya watu.....ehhhhhhhhhhee
   
 3. StaffordKibona

  StaffordKibona JF-Expert Member

  #3
  Apr 29, 2010
  Joined: Apr 21, 2008
  Messages: 671
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Mapenzi haichagui kabila
  Muzungu Muchaina huoana
  japanizi mwafrika vile vile
   
 4. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #4
  Apr 29, 2010
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Safi sana. Tatizo la familia nyingi maarufu hasa kwa mali/utajiri huwa wanalazimisha watoto wao kuolewa/oa ndani ya circle yao na mwishowe ndoa hazidumu! Acha mwanao achague mwenzi wake ili mradi wote wana maadili mema.
   
 5. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #5
  Apr 29, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  safi sana ...mapenzi ya kweli ni kutoka moyoni
   
 6. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #6
  Apr 29, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  aaaah mjukuu wangu umenikumbusha mambo yangu hayooooo miaka ileeeee....dah
   
 7. L

  LadySwa Member

  #7
  Apr 29, 2010
  Joined: Jan 25, 2009
  Messages: 77
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  wale mliosema dada zetu wakibongo wanaolewa na wazungu kwa ajili ya njaa......mshindwe........
  Tatizo lenu kila kitu mnatoa madomo kizuri kibaya hiyo imepitwa na wakati.
   
 8. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #8
  Apr 29, 2010
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Hapo mmasai ni full kujiexpress
  Si n'chezo kudadadadeki.
   
Loading...