Mmarekani Anatarajiwa Kuishi Miaka 75, Mtanzania Miaka 52

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,319
33,125
2893930.jpg

Sunday, August 23, 2009 7:08 PM
Kwa mujibu wa data za umoja wa mataifa, mtoto anayezaliwa na kuishi Tanzania anategemewa kuishi miaka 52 kabla hajafariki wakati mtoto anayezaliwa na kuishi Marekani anategemewa kuishi sio chini ya miaka 75. Kwa mujibu wa data zilizotolewa na serikali ya Marekani, wastani wa matarajio ya umri wa kuishi (Life expectancy) wa Mmarekani umeongezeka kufikia miaka 77.9.

Pamoja na ongezeko hilo wanawake bado wanaonekana kuwa na maisha marefu zaidi ya wanaume wakiwazidi wanaume kwa miaka mitano, taarifa iliyotolewa na kituo cha kupambana na kuzuia magonjwa cha Marekani (CDC) ilisema.

Idadi ya vifo nchini Marekani imepungua hadi kufikia vifo vya watu 760 kwa mwaka katika kila watu 100,000.

Katika kipindi cha miaka 10, wastani wa matarajio ya umri wa kuishi nchini Marekani umeongezeka kutoka miaka 76.5 mwaka 1997 hadi miaka 77.9 mwaka 2007.

Mtoto wa kiume anayezaliwa na kuishi nchini Marekani anatarajiwa kuishi na kufikia miaka 75 wakati watoto wa kike wanatarajiwa kufika umri wa miaka 80 ilisema taarifa ya CDC na kuongeza kuwa kwa mara ya kwanza wastani wa matarajio ya umri wa kuishi wa Mmarekani mweusi umefikia miaka 70.

Kwa ujumla watu 2,423,995 walifariki mwaka 2007 nchini Marekani huku asilimia 48.5 ya vifo hivyo ilitokana na magonjwa ya moyo na kansa. Watu 11,061 walifariki kutokana na ugonjwa wa ukimwi.

Kwa mujibu wa data za umoja wa Mataifa, wastani wa matarajio ya umri wa kuishi wa Mtanzania ni miaka 52.5.

Wanaume wa Tanzania wanatarajiwa kuishi miaka 51 wakati wanawake wanatarajiwa kuishi mpaka miaka 54.

Magonjwa ya malaria, ukimwi na kifua kikuu ndiyo yanayochangia vifo vingi nchini Tanzania na nchi nyingi za bara la Afrika.
http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsId=2893930&&Cat=2
 
Back
Top Bottom