Mmarekani ahukumiwa kufungwa na kazi ngumu Korea Kaskazini

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,879
6,356
Raia wa Marekani amefungwa jela miaka 10 na kazi ngumu nchini Korea Kaskazini baada ya kupatikana na makosa ya kufanya ujasusi, shirika la habari la Uchina la Xinhua limeripoti.

Kim Dong-chul, raia wa Marekani aliyezaliwa Korea Kusini, alikamatwa mwezi Oktoba mwaka jana.

Kim aliwasilishwa kwa wanahabari mjini Pyongyang mwezi jana na akaoneshwa akikiri makosa, na kusema kwamba alilipwa na Korea Kusini kufanya ujasusi.

Mwezi Machi, mwanafunzi mwingine Mmarekani alifungwa jela miaka 15 kwa kujaribu kuiba bango la propaganda.

Alipatikana na makosa ya "uhalifu dhidi ya dola”.

Kim amefungwa jela katika kipindi ambacho uhusiano baina ya Korea Kaskazini na Umoja wa Mataifa, Marekani na nchi nyingine za Magharibi umedorora.

Majuzi, Pyongyang imefanya msururu wa majaribio ya kurusha makombora baada ya kufanyia majaribio bomu ya nyuklia mwezi Januari, majaribio yote yakivunja vikwazo zilivyowekwa na UN.

Pyongyang ilijaribu kurusha makombora mawili ya masafa ya wastani Alhamisi lakini yalilipuka na kuanguka baharini muda mfupi baada ya kurushwa.

Hatua hiyo ilipelekea kuitishwa kwa mkutano wa dharura wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.


Chanzo: BBC
 
Acha aadabishwe shenzi kabisa na ikiwezekana wampige kitanzi...haya mashoga njoeni mumtetee jamaa yenu anateswa na mapanki
 
huyo nae anapiga kelele tuu mwisho wa siku Wamarekani anawaachia amewahukumu raia wa USA kama saba ivi lakini woote wameachiwa kwa vipindi tofauti waliopo ndani ni yule pastor mcanada aliehukumiwa kifungo cha maisha jela na mwingine miaka 15...huyu nae atamtoa tuu
 
aliita waandishi wa habari mwenyewe na kusema alichokua anafanya miaka mingi...baadae wakamtia nguvuni na kupata hukumu ngoja tusubiri hii hadith itaishaje...
 
Back
Top Bottom