Mlolongo wa ajali za misafara ya Rais Kikwete - Nini kifanyike?

Una maana Rais wetu analindwa na majini ya Shekh Yahya, na sasa yanataka mlo wa damu ya binadamu? Watu wengine bana wanatuvunja mbavu kwani ni hadithi za kufikirika.

Mkuu siyo mimi niliyesema,muundaji wa hayo majini hayati Sheikh Yahya ndiye alilitangazia taifa kuwa amejitolea kuongeza ulinzi wa rais baada ya kuona wale vijana wa PSU wameshindwa kazi kwa kumuacha JK akipiga mieleka ya hapa na pale.
 
Mkuu siyo mimi niliyesema,muundaji wa hayo majini hayati Sheikh Yahya ndiye alilitangazia taifa kuwa amejitolea kuongeza ulinzi wa rais baada ya kuona wale vijana wa PSU wameshindwa kazi kwa kumuacha JK akipiga mieleka ya hapa na pale.

Cha msingi umetukumbusha yaliyokuwa yanaongelewa na hayati Sheikh Yahya kwamba atamwongezea Rais Kikwete ulinzi usioonekana.
 
Jamani, hapa tuacheni uCCM, uCDM, uSheikh Yahya na tuliangalie hili sual kwa uhalisia wake? Inakuwaje gari (liwe la yeyote lakini la Raisi ndio zaidi) linavuka tairi? Inakuwaje msafara wa raisi unaenda safari bila ya kuwa na mafuta ya ziada wanaenda kuweka mafuta kwenye vituo? Ni uzembe kama sio njama. Raisi kuwa anapanga safari ghafla isiwe sababu ya kutokea ajali hizi za kizembe. Hata dereva wa mtu binafsi ikiwa ameajiriwa kwa kazi hiyo wajibu wake ni kuhakikisha kuwa gari ipo salama muda wote.

Na kama tunaliacha hili katika mikono ya Mungu, Mungu si wa CCM, CDM wala wa Sheikh Yahya tu. Ikiwa kweli tunamwamini Mungu, iweje tena sisi kumtumia Mungu huyo huyo awaadhibu wengine? Ameshindwa kazi hadi kutaka msaada wetu?
 
Sio kawaida kwa gari kama hili kuchomoka tairi likiwa njiani - tena na brake disk kuachia kabisa! Wawe waangalifu sana kwani hapa ni ama uzembe ulifanyika katika ufungaji baada ya kubadilisha parts au ni hujuma tu. Inaonekana uswahili umeenea hadi kwenye usimamizi wa nyenzo za Ikulu.

Kwani si hukohuko kimara mwaka jana tairi lilichomoka?

RAIS2.JPG
 
Kwani ile helkopta ya kampeni kaipeleka wapi? Si aitumie!!!!!!!!!!!!

Tena atasaidia na kupunguza folen zisizo za lazima
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom