Mlolongo wa ajali za misafara ya Rais Kikwete - Nini kifanyike? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mlolongo wa ajali za misafara ya Rais Kikwete - Nini kifanyike?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Candid Scope, May 7, 2012.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  May 7, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  [​IMG]
  Rais Jakaya Kikwete akiteremka kwenye gari lake eneo la Kimara Rombo,
  Dar es Salaam kumjulia hali Askari wa kikosi cha Usalama Barabarani
  Sajent Steven Laizer, baada ya kupata ajali akiongoza
  msafara wa Rais kuelekea kwenye msiba wa dereva wa Ikulu


  1. MSAFARA wa Rais Jakaya Kikwete jana ulipata ajali baada ya askari aliyekuwa akiuongoza kwa pikipiki kudondoka na kujeruhiwa katika eneo la Kimara, Dar es Salaam. Ajali hiyo ilitokea eneo la Kimara Rombo saa 4.30 asubuhi wakati Rais Kikwete alipokuwa akielekea Kimara Kilungule kwenye msiba wa Dereva wa Ikulu, Deokalyus Makwasinga aliyefariki dunia katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili baada ya kupata ajali mbaya ya gari katika eneo la Kimara-Korogwe, Msikitini usiku wa kuamkia Ijumaa.
  2. Tukio la kwanza lilitokea maeneo ya Kimara Mwisho wakati Rais alipokuwa akitokea Kimara-Bonyokwa katika alikokwenda kutembelea maeneo yaliyokuwa na matatizo ya maji kwa muda mrefu. Msafara huo ulilazimika kusimama ghafla kutokana na gari alilokuwa amepanda kuchomoka tairi la mbele.
  3. Katika tukio la pili, msafara wa Rais ulisimama ghafla eneo la bandarini karibu na eneo la Matangini baada ya gari alilokuwemo kuchomoka tari la nyuma wakati akitokea Keko Toroli.
  4. Januari 2010, msafara wa Rais Kikwete ulipata ajali mkoani Shinyanga wakati gari la polisi lililokuwa likiuongoza kuacha njia na kupinduka na kujeruhi askari. Walioshuhudia ajali hiyo walisema waliliona gari hilo likiyumba na baadaye kuacha njia na kupinduka kando ya barabara iendayo Meatu. Katika ajali hiyo iliyotokea katika Kijiji cha Nyikoboko wakati msafara wa Rais ukitokea Kisese alikokuwa amekwenda kuzindua Mto Simiyu unaounganisha Wilaya za Bariadi na Meatu, askari sita walijeruhiwa.
  5. Mei, 2010, magari aliyokuwa amepanda Rais Kikwete akiwa katika ziara yake ya siku mbili Dar es Salaam yalipata hitilafu baada ya magari hayo kuchomoka matairi katika maeneo tofuati yakiwa safarini.
  6. Kuna ajali iliyotokea msafara wa Salma Kikwete barabara ya Segerea kama sijakosea iligharibu uhai wa mtu.
   
 2. s

  sikiolakufa JF-Expert Member

  #2
  May 7, 2012
  Joined: Feb 1, 2010
  Messages: 411
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mara nyingi riders( waendesha pikipiki za msafara) hujisababishia ajali kwanini huwa wanailaza zigzag pikipiki huku wakiwa kasi kubwa? Wakati sumaye alikwa waziri mkuu rider alinusurika kufa pale brake point bado wanaendelea kuzilaza pikipiki...sisi tufanyeje sasa?
   
 3. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #3
  May 7, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 444
  Trophy Points: 180
  Sheikh Yahya anawaita taratibu! Akisikia njaa anaita damu za the gambaz fasta unashangaa ajali hiyoooooooo!!!!
   
 4. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #4
  May 7, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Kasi ya msafari ni kitu hatari zaidi. Sioni sababu ya kwenda kasi kiasi hicho. Mbona jana Kikwete alisubiri dakika kadhaa ilipotokea ajali hakikutokea kitu kibaya? Kasi ile wanaogopa nini kama si mtindo tu wa maisha na woga?
   
 5. M

  Mkwe21 JF-Expert Member

  #5
  May 7, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 1,856
  Likes Received: 498
  Trophy Points: 180
  Kuchamba Kwingi!! - Wanatakiwa Wajue Safety Kwanza!!
   
 6. Wingu

  Wingu JF-Expert Member

  #6
  May 7, 2012
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 4,326
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Apande mabasi tunayopanda sisi aone kama mpaka 2015 hajawa mkono mmoja,mguu mmoja,jicho moja na kalio moja.
   
 7. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #7
  May 7, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 444
  Trophy Points: 180
  Mkuu tatizo siyo kasi peke yake, kwa kuwa tangia enzi ya nyerere walikuwa wanaendesha hivyo!
  Mi nadhani hii kauli ya CHADEMA kutokulipiza kisasi kwa wauaji wa CCM ndiyo sababu. CHADEMA walisema wao wamewachinja watu wetu, lakini sisi hatutalipiza kisasi, tunawaachia Mungu atafanya!

  Sisi tuna Mungu
  Wao wana Pesa
   
 8. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #8
  May 7, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Damu za wahanga wetu zinawamaliza
   
 9. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #9
  May 7, 2012
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 159
  Trophy Points: 160
  Kwani si hukohuko kimara mwaka jana tairi lilichomoka?

  [​IMG]
   
 10. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #10
  May 7, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160

  Inawezekana misafara ya Mkulu haipangwi katika takwimu zake sahihi hivyo vyombo huwa havijaandaliwa ipasavyo. Kuna dalili kama za kushtukiza vile.

  Inaelekea akiwa pale Ikulu panawasha akikaa hivyo anaamua kuinuka ghafla na kupanga safari zisizotarajiwa na matokeo ndo hayo. Ni fikra zangu binafsi.
   
 11. Mr.Professional

  Mr.Professional JF-Expert Member

  #11
  May 7, 2012
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 1,602
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  yeye mwenyewe hana umakini na watu wanaoangalia ulinzi wake hawako makini kinachobaki ni kudra za Mungu tu
   
 12. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #12
  May 7, 2012
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,648
  Likes Received: 4,753
  Trophy Points: 280
  Ukiona hivyo ujue yale majini aliyowekewa na Shekh Yahya hajapata msosi siku nyiingi sasa yanabeep, yasipopigiwa yatafanya balaa siku si nyingi.
   
 13. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #13
  May 8, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Una maana Rais wetu analindwa na majini ya Shekh Yahya, na sasa yanataka mlo wa damu ya binadamu? Watu wengine bana wanatuvunja mbavu kwani ni hadithi za kufikirika.
   
 14. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #14
  May 8, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Ajali ni kawaida, Mungu akishapanga huwezi kukwepa.
   
 15. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #15
  May 8, 2012
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,315
  Likes Received: 5,608
  Trophy Points: 280
  Wapunguze speed zao ambazo sizo za lazima wanakimbiaa sanaa......wanaogopa nini?au wanakambia nini??
   
 16. Nzowa Godat

  Nzowa Godat JF-Expert Member

  #16
  May 8, 2012
  Joined: Jun 15, 2011
  Messages: 2,630
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Ajali hazipangwi na Yehova, zinasababishwa na:- uzembe, kukosa uangalifu/recklessness, matatizo ya kiufundi, hali ya hewa, mwendo kasi, and other physical conditions.
   
 17. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #17
  May 8, 2012
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,856
  Likes Received: 2,432
  Trophy Points: 280
  Umesahau kituko cha moshi ..magari Yake yote yalizimika baada ya kuwekwa mafuta mabovu...kwenye vituo vya uchochoroni vya mafuta......ililetaa tafrani Kali walinzi wake wakiohofia kuna tukio lilipangwa kumbe uzembe tu
   
 18. k

  kasimba123 JF-Expert Member

  #18
  May 8, 2012
  Joined: Apr 18, 2010
  Messages: 1,318
  Likes Received: 188
  Trophy Points: 160
  Shehe yahaya alisema atampatia ulinzi uliojificha usiooneka na yeye na ikulu yake hawakukanusha kwa hiyo unganisha dots
   
 19. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #19
  May 8, 2012
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,648
  Likes Received: 4,753
  Trophy Points: 280
  Labda mungu wa CCM, lakini Mungu muumba wa mbingu na nchi hapangi ajali.
   
 20. MD25

  MD25 JF-Expert Member

  #20
  May 8, 2012
  Joined: Jan 28, 2012
  Messages: 3,078
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Mungu atuondolee huu udhia mapema iwezekanavyo... Mungu tunakuomba usikie maombi yetu..
   
Loading...