Mlolongo wa Ajali za Barabarani Tanzania 2007-2011

Unajua viongozi wa Africa wanakasumba ya kudhania sababu wewe ni kiongozi then unaweza kuamua chochote. Hii sio kwenye barabara tuu, waulize bank kuu kasheshe wanayo ipata kutoka kwa hawa viongozi shwain, pesa hakuna wanaorder tuu kwa balali print more money, Barabara foleni, wanaorder viongozi wanunuliwe choppa na barabara funga leni moja ya kwenda.

Tukiadopt tabia ya kusue serikali na kusnach some money from their poket all this mess will end.
 
.... kali zaidi ni hapo walipotenga 10bn ili kuimarisha huo mpango wa bwana Lowassa,sijui kutoa pesa kiasi hicho kwa miradi kama hii wameangalia nini? au ndio so called MAAGIZO kutoka ofisi ya waziri mkuu....bado saaaaana wajomba!
 
...................Tukiadopt tabia ya kusue serikali na kusnach some money from their poket all this mess will end.

Good pont!............na tuwaelimishe wananchi kuhus haki zao barabarani.

Utaratibu wa njia tatu sio mbaya......................tatizo linalotusumbua, na ninapenda kurudia tena na tena ni Engineering, Education, Enforcement (i.e EEE).

uamuzi wa njia tatu kwa niuonavyo mimi pale Dar its unfinished engineering practice, education nafikir ilikuwa almost zero.....enforcement ndio kabisaa hata kusema sitaki
 
Huyo El Yeye Anajua Kutoa Amri Tu...hatumii Kichwa Hata Kidogo! Nakumbuka Aliamua Eti Wanafunzi Wa Chuo Cha Ardhi Warudishwe Nyumbani Mwaka Mzima Mnamo 1995! It Was So Crazy! Wakati Wanafunzi Walikuwa Na Madai Dhahiri Na Halali Kabisa. Ni Ubinafsi, Kuonyesha Umwamba, Hana Lolote.

El Kama Anataka Afanya Kitu Kimoja Cha Maana Tz Basi, Aamuru Barabara Zijengwe Tz, Ali Muradi Aanze Na Dar. Hivi Kwa Nini Ni Sisi Peke Yetu Hatuna Barabara Za Juu Ya Ardhi? Infrastructure Za Namna Hii Zinasaidia Sana Foleni, Na Ni Salama Pia Kwa Kutokuleta Ajali...maana Magari Yanayoenda Muelekeo Mmoja Yanachukua Njia Yake, Na Opposite Direction Yanachukua Mkondo Wake. Lowassa Anatakiwa Awe Na Mawazo Ya Maendeleo Kama Haya, In This Way, Hata Akidokoa Hapa Na Pale, Watanzania Tunaweza Kujiliwaza Kwamba Angalau Amefanya Kitu Cha Maana Kwenye Wakati Wake.

Tuna Ma-engineer Kibao Nchini, Lakini Hawatumiwi Kwa Manufaa Ya Nchi Kuleta Maendeleo....kila Siku Tu Tunaishia Kuziba Viraka Barabara Za Mwaka 1969...hivi Huu Uvivu Wa Viongozi Wetu Wa Kufikiri Utaisha Lini Haswa? Jamani Tan-road Ipewe Challenges Inayostahili!!! Viongozi Wetu...kama Mnasoma Jf, Please Do Your Homeworks. Kila Siku Mnaenda Nje Na Misafara Ya Jk Tu Akienda Vacation Nje Ya Nchi, Nyie Hamfunguki Macho Jamani? (pardon My Language, But I Think What Our Esteemed President - Jk Is Doing Is To Take A Series Of "good For Nothing" Vacations/honeymoon On Our Tax-payers Money!!!!).

Naona Niishie Hapa Kwa Leo ;-)!
 
Hizo njia tatu ni balaa kabisa kila siku zinasababisha ajali. Hao Tanroads wangefanya mipango ya muda mrefu kupanua barabara za kuingia mjini kadiri inavyowezekana kwa sababu nafikiri kuna baadhi ya sehemu haziwezi kupanuliwa kutokana ma majengo.
Kuna hawa watu wanaitwa SUMATRA, hawa mimi naona ni kitengo kimewekwa tu kwa ajili ya ulaji. Hakuna wanachofanya zaidi ya bosi wao mmoja kuonekana tu kwenye TV kila mara na kofia la pama anachofanya hata sijui nini. Kama kweli leo hii SUMATRA wakiamua na wana uwezo huo kupiga marufuku vipanya vyote viishie ubungo kwa vinavyotoka mbezi na kimara, vya kutoka tegeta, bunju kunduchi viishie mwenge, vinavyotoka mtoni, mbagala viishie temeke na vinavyotoka gongo la mboto, vingunguti viishie buguruni (na hii iwe kwa kuanzia baadaye vizidi kusogezwa nje ya mji taratibu)na waruhusu mabasi yenye ukubwa wa kuanzia dcm/coaster kuingia mjini. Nafikiri hili likifanyika hata leo hii foleni zitapunguwa sana asubuhi wakati wa kuingia mjini na jioni wakati wa kutoka mjini. Kwa sababu baadhi ya watu wakiwa na uhakika na "public transport" watapaki "private car" zao.

Kuna foleni nyingine inayokera sana hii ipo mjini kuanzia muda wa saa 4 asubuhi mpaka saa saa nane hivi. Hii ni folleni hakuna anayeizungumzia. Lakini hii foleni mimi naiita ya kijinga kabisa na inasababishwa na hawa wahusika wanaotoa vibali vya ujenzi. Na hii inasababishwa na kutokuwepo na "parking" za magari mjini. Hivi city wanashindwa kabisa kuweka sheria ndogo tu kuwa kila jengo hususani la ghorofa linalojengwa ni lazima liwe na "floor" moja au mbili za "parking" ndani yake.
 
Huyu dereva wa lori si inatakiwa akabiliwe na kosa la kuua (sio kuua bila kukusudia)? Maana kama alijua gari ina matatizo ya brakes na bado akalipeleka barabarani, basi Tanzania tuna hatari kubwa mno.

Watu 15 wafa katika ajali Mbeya

*Yumo askofu wa Wasabato


Brandy Nelson na Hawa Mathias, Mbeya


WATU 15 wamefariki dunia na wengine 13 kujeruhiwa akiwamo Askofu Mkuu wa kanisa Wasabato Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, William Mtani baada ya lori kuligonga kwa nyuma basi dogo la abiria Toyota Hiace maarufu kama kipanya katika eneo la Kinyala Wilaya ya Mbozi, mkoani Mbeya.


Waliokufa katika ajali hiyo na majina yao kutambuliwa ni pamoja na Katibu wa kanisa hilo la Wasabato Golden Mwangwilima, kondakta wa Kipanya, Friday Siwakwi (23) mkazi wa Mwanjelwa jijini Mbeya, Salome Mgala mkazi wa Ihumwe jijini Mbeya, Atupakisye Sege, Salum Ramadhani, Frank Mwasege, Hussein Amani, Elizabeth Mwakalukwa, John Poles, Andrwe Mwalukama na wengine wanne bado majina yao hayajatambulika.


Waliojeruhiwa katika ajali hiyo ni pamoja na Veronika George, Lucy Ndenga, Upendo Isaya, Amani Mwasanga, Hezron Masawe, Amani Salehe ambao wote wamelazwa katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mbeya na dereva wa Hiace, Remijo John (41) ambaye amelazwa katika Hospitali teule ya Ifisi iliyopo Mbalizi nje kidogo ya Jiji la Mbeya na hali zao zinaendelea vizuri.


Akielezea tukio hilo dereva wa Lori, Elipamphrey Samky mkazi wa jijini Dar es Salaam alisema ajali hiyo ilitokea saa 12:00 juzi baada ya kushindwa kufunga breki kutokana na gari hilo kuwa na matatizo ya breki wakati mbele yake kulikuwa na basi la abiria lililokuwa linaingia barabarani kutoka kituoni.


�Baada ya kuona Hiace inaingia barabarani na gari yangu ilikuwa na tatizo la breki nilipoonyesha ishara ya hatari kwa kuwasha taa ya kuwa gari yangu haiwezi kusimama, lakini dereva wa Hiace aliendelea kuingia barabarani ndipo nilipomgonga kwa nyuma,�alisema.


Alisema magari yote mawawili yalikuwa yanatokea barabara ya Tunduma ambapo yeye alikuwa amepakia matofari aliyoyatoa wilayani Mbozi kuyapeleka eneo la Kwa Mama John, jijini Mbeya ndipo alipokutana na ajali hiyo katika eneo hilo.


Naye dereva wa kipanya, Remijo John akiwa katika Hospitali teule ya Ifisi alisema anachokumbuka ni kishindo tu na baada ya kupata fahamu aliona kuna lori ambalo limeanguka lakini alikuwa hajui kama ndilo lililomgonga mpaka alipoambiwa na watu waliompeleka hospitalini hapo.


Alipohojiwa kama aliliona lori hilo nyuma yake alisema hakuliona kwani yeye alikuwa anatoka katika kituo kupakia na kushusha abiria akiingia barabarani kuendelea na safari ndipo ghafla alisikia kishindo mara kapoteza fahamu na baadaye alipopata fahamu akaona lori lililoliganga basi lake.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Suleiman Kova alisema baada ya lori hilo kuigonga Hiace liliseleleka umbali wa meta 350 na kuanguka upande wa pili wa barabara umbali wa mita 20 wakati Hiace ilipogongwa iliburuzwa umbali meta 50 na baadaye likarushwa pembene mwa barabara.


Kova alisema waliokufa papo hapo katika ajali hiyo ni saba na wanne walifia njiani walipokuwa wakipelekwa hospitalini watatu walifariki jana usiku walipokuwa hospitalini wanapatiwa matibabu na mmoja amefariki dunia leo asubuhi katika hospitali ya Rufaa Mbeya.


Muuguzi wa zamu aliyejulikana kwa jina moja la Zambi alisema kuwa majeruhi hao wanaendelea vizuri lakini hawataweza kuruhusiwa kwa sasa.


Mkoa wa Mbeya umekuwa na matukio kadhaa ya ajali ndani ya mwaka huu wa 2007 na kwambva mpaka sasa jumla ya ajali tano na kusababisha vifo vya watu wengi. Novemba 8, mwaka huu lori aina ya Scania liliparamia nyumba na kusababisha vifo vya watu watatu.


Naye Gasper Andrew, anaripoti kutoka Singida wanafunzi wawili wa Shule ya Msingi ya Kasasida iliyoko Kijiji cha Kisasida katika Halmashauri ya Manispaa ya Singida, wamefariki dunia na abiria wengine 17 wamejeruhiwa vibaya baada ya gari hilo kushindwa kupanda mlima wa Kisasida kiasha kuacha barabara na kupinduka.


Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Celina Kaluba alisema ajali hiyo imetokea juzi jioni saa 12.00 jioni wakati abiria hao ambao wengi wao ni wafanyabiashara waliokuwa wanatokea mnadani.


Aliwataja wanafunzi hao waliofariki kwenye ajali hiyo kuwa ni Swaa Ally (13) na Juma Hamisi (13) na wote ni wanafunzi wa darasa la tano.


Kamanda Kaluba, alisema chanzo cha ajali hiyo ni gari hilo kukosa breki hivyo kumfanya dereva kushindwa kulimudu na hivyo kupinduka.
 
Mungu wangu.Watanzania tutaisha kwa ajali za kiholela namna hii.Mungu azilaze roho za marehemu pema peponi na majeruhi nawaombea wapone haraka
 
Tunatoa Pole kwa watanzania wote na hasa ndugu wa marehemu katika msiba huu, tuwakumbushe madereve kuwa makini wawapo barabarani na kufuata sheria za barabarani. Pia ni vyema madereva wakapata mafunzo sahihi yatakayoendana na kutahiniwa ili kujua viwango vya madereva. Polisi wa barabarani ni muhimu kufanya ukaguzi wa mara kwa mara kubaini viwango vya madereva.
 
Tufanyeje Watanzania ili ajali hizi zipungue? kila siku nikitazama taarifa ya habari ajali,viongozi wetu nao wanapata ajali,ingawa wanasema eti kwa watu wa chini ajali zinasababishwa na mwendo kasi,je? na wao wanatumia mwendo huo ndio maana ajali zinaongezeka? wemeleta speed govenor haikusaidia sasa itafuata nini ili tusimalizike wanyonge?
 
5 Tanesco workers die in Mbeya road smash

2007-11-15 10:08:33
By Pendo Fundisha, PST, Mbeya


Five Tanzania Electric Supply Company (Tanesco) employees died yesterday when their vehicle rammed into a lorry parked at the roadside at Chimala in Mbarali District, Mbeya Region.

The crash, which left four other people critically injured, occurred a mere two days after 15 people died and 16 were hurt in a similar road accident in the region.

Mbeya Regional Police Commander Suleiman Kova confirmed the incident, saying it occurred at around 7:15 am as the workers drove to Chimala Township to fix broken high-tension electric poles.

Survivors gave the name of the driver of the Tanesco vehicle, with registration number SU 33510, as Moses Mwaisaka.

They said he was trying to avoid crashing into the parked lorry when he discovered that two speeding passenger buses were behind him.

�Our driver tried to stop but the vehicle veered and hit the back of the lorry and overturned, killing five people on the spot,� explained acting Mbeya regional Tanesco manager Method Byabato.

He identified the deceased as Atson Limbo, Vatus Nchimbi, Mama Mwakanyamale and two other people only as Komba and Hussein.

The survivors are Odilia Milinga and three other casual labourers whose names could not be established immediately.

The bodies are preserved at the Chimala Mission Hospital, where the injured survivors are undergoing treatment.

SOURCE: Guardian
 
Duh kaazi kwelikweli, pole nyingi kwa familia za marehemu, walioumia nawaombea nafuu ya haraka.
 
Mudhihir JKN inter toka Lindi.jpg

Mudhihir wodini.jpg

Mudhihir atoka wodini.jpg


Mudhihir%2BPage-1.jpg

Mh na Mkono PACHA

Ajali iliyotokea siku kadhaa nyuma kwa Mh.mudhihir wadaku wanasema kumbe haikuwa ajali bali kitu kingine tofauti na wakuu wakachagua kusema ajali ili kuficha siri hiyo ya aibu…..wadaku wanahoji vipi dereva wa gari hilo asijulikane hali yake wala kutangazwa alipo???!!!!na vipi kuhusu hilo gari hata kuonekana limekuaje baada ya Mh.kukatwa hadi mkono???!! na vipi sura ya mtu aliepata ajali kubwa kiasi hicho asiwe hata na jeraha dogo tu usoni?????!!!!!
Wadau wa JF mwenye nyeti naomba aziwasilishe tupate ukweli huu.
 
Ajali iliyotokea siku kadhaa nyuma kwa Mh.mudhihir wadaku wanasema kumbe haikuwa ajali bali kitu kingine tofauti na wakuu wakachagua kusema ajali ili kuficha siri hiyo ya aibu…..wadaku wanahoji vipi dereva wa gari hilo asijulikane hali yake wala kutangazwa alipo???!!!!na vipi kuhusu hilo gari hata kuonekana limekuaje baada ya Mh.kukatwa hadi mkono???!! na vipi sura ya mtu aliepata ajali kubwa kiasi hicho asiwe hata na jeraha dogo tu usoni?????!!!!!
Wadau wa JF mwenye nyeti naomba aziwasilishe tupate ukweli huu.

Mhh! Interesting! Share with us the conspiracy theories!
 
Nimesikia hiyo mkuu ,kuwa alikutwa na mke wa mtu ,jamaa akamwambia achague mmoja mmkono au kinyume na maadili aingiliwe basi mheshimiwa akakubali akatwe mkono! Ni maneno ya huku uswahilini kwetu ,i got no proof on that!
 
Ila wanakijiji wenzangu, naona kama hapo kweli kuna utata kidogo. Ingawa wanasema kwamba gari alikuwa analiendesha mwenyewe. Macho yetu
 
kweli hata mimi nafikiri hata picha moja jamani ya gari lililopata ajali ya mheshimiwa, wala picha baada ya ajari!!!! very interesting
 
Hata mie nmesikia fununu toka huko Lindi kuwa kuna jamaa alikuwa anahisi MHESHIMIWA anatembea na mke wake, basi akaweka mtego, na ukanasa. Yanayofuata ni hivyo hivyo alivyoeleza mwanablog ENDAKU, wafikiri kuinama ni rahisi?. Tumaini langu siku ya kurejea bungeni yote yaweza kuwekwa wazi na WAPINZANI!!!! Inshalah
 
Back
Top Bottom