Mloingia katikati ya jiji la Dar Es Salaam leo foleni mmeionaje!?

mtozatozo

JF-Expert Member
Sep 25, 2021
459
412
Kusema kweli tangu nimeanza kuishi katika jiji hili pendwa takriban miaka kumi na tano ilopita,sijaona foleni kubwa kama Jumatatu ya leo Novemba 29..kuanzia Posta,Kariakoo,Lugoda, Gerezani,hadi Kurasini.

Inafikia hatua hadi watembea kwa miguu wanakosa sehem ya kupita, hususan kipande cha kutoka gerezani hadi round about ya bendera tatu...kama umeingia mjini leo hebu tupe experience yako kwa foleni ya leo.
 
Nimekaa kwa foleni tangu saa 1 mpaka saa 8 mchana.Na sikuweza kuingia mjini kutoka kigamboni kupitia darajani.
 
Hameni sasa Dar mje mikoani.
Msing'ang'anie kukaa Dar huku mkiteseka kuvuta hewa chafu ya msongamano, moshi wa magari, viwanda, majenereta na mashine. Pia kuteswa na kelele kwa kwenda mbele. Unachosha mapafu na ubongo mwisho wa siku mnakufa mapema.
 
Money money

Back
Top Bottom