Mloganzila yakanusha juu ya taarifa za vifo vya wagonjwa

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,492
9,263
Hospitali ya taaluma na tiba (MAMC)Mloganzila iliyopo chini ya chuo kikuu cha afya na sayansi shirikishi (MUHAS) kimekanusha juu ya taarifa za kuwepo kwa vifo vya wagonjwa vinavyotokana na ukosefu wa huduma bora wakiwemo wale waliohamishiwa hapo kutoka Muhimbili.

DUUIC6JWsAAP1KU.jpg

ITV
 
Haya malalamiko yamekuwa mengi iundwe tume luyachunguza kama ni kweli
 
Imekuwa machinjio ya kimataifa, waunde tume kufatilia hilo.
Hao madaktari wanafunzi wanajifunzia kwa wagonjwa badala ya maiti km zamani.
 
Sio wanafunzi? ni madaktari wanafunzi?

Sent using Jamii Forums mobile app
Intern Doctors (Madaktari watarajali) sio wanafunzi. Hawa huwa wahitimu kutoka shule husika za tiba (medical schools). Huwa na leseni (Provisional Licences) za kutoa huduma za afya kutoka mabaraza husika ya kitaaluma.

Madaktari wanafunzi na au wanafunzi wa tiba (Medical Students) bado hawajahitimu, ndio hao ambao wapo kwenye shule za tiba (Medical Schools) wanaendelea kusoma. Usiwachanganye.

Hawa interns (Doctors, Nurses, Pharmacists, Laboratory Scientists, Physiotherapists, Radiologists, n.k.) wapo kwenye Hospitali zote za Rufaa za Kanda na baadhi ya Hospitali za Rufaa za Mkoa, hawapo Mloganzila pekee.
 
Imekuwa machinjio ya kimataifa, waunde tume kufatilia hilo.
Hao madaktari wanafunzi wanajifunzia kwa wagonjwa badala ya maiti km zamani.
Mkuu,

Wataalamu wa tiba za wanadamu hujifunza kupitia kwa wanadamu wanaowahudumia. Maiti huwa ni hatua ya mwanzoni kabisa wanaposoma somo la physiology na anatomy.

Theories nyingine hujifunza huko shuleni na baadae (mara nyingi kuanzia mwaka wa pili katikati au wa tatu) huanza kujifunzia kwa watu walio hai kwa kuanza na vitu vidogo kama kufuatilia maendeleo ya mgonjwa, kuchukua historia, tiba sahihi, n.k. Haya yote hufanyika chini ya uangalizi.

Baada ya kuhitimu, kwa mujibu wa sheria duniani kote, na kwa Tanzania, huhitaji kufanya kazi mwaka mmoja chini ya uangalizi, huku wakifanya kila kitu kama Wataalamu wa afya, na hivyo hupewa leseni.

Halafu ni mantiki ndogo kabisa, mtu anayehudumia mwanadamu aliye hai hapaswi kujifunzia kwa maiti pekee. Ni kitu ambacho hakiwezekani.

Let's be rational and fair.
 
Nashukuru kwa shule tosha, maana miye sikulipenda hilo somo kbs "maana miye nilisoma kitu kinaitwa unified science km uliwahi kusikia.
Ila ninachomaanisha hao madaktari wanafunzi wangekuwa chini ya uangalizi km ulivyosema mwanzo mwisho.
 
Kukanusha kuwepo vifo ni UONGO, hakuna hospitali wagonjwa hawafi duniani. Wangekanusha specifics, sio general kwamba HAKUNA VIFO. Kwani Mloganzira ni MBINGUNI?
 
Back
Top Bottom