Mlituahidi SGR Dar - Moro kuwa tayari toka Novemba mwaka jana 2019, hadi leo ni visingizio tu, mara mvua, mahandaki, mara madaraja, blah blah, blah!

Kwa hatua ilipo, itatuchukua miaka 20 kuifikisha Kigoma. Huyu anaeomba ridhaa amalizie miradi aliyoianzisha maana yake tutavunja katiba kumpa ridhaa ya miaka 20 ili afanikishe hayo.

akiwa anakabidhiwa mradi 2024 na mkandarasi ili auzindue,utakuwa unaadika "abiria wa sgr moro-dar walalamika bei kuwa juu 8000,tofauti na nauli ya mabasi 7500"
 
Tuliambiwa kwamba awamu ya kwanza ya SGR Dar es Salaam kwenda Morogoro, kupitia Pugu, Soga, Ruvu, na Ngerengere ujenzi wake ungekamilika mwaka jana November 2019.

Mkasema ooh, kuna handaki karibu na Morogoro inabidi lichimbwe limechelewasha kazi (yaani kama vile hamkujua kuwa kutakuwa na hilo handaki kwenye SGR), kisha mkasema mvua kubwa zimenyesha zimeondoa madaraja. February mwaka huu 2020 mkaahidi kipande cha Dar - Moro kingekamilika April 2020, na majaribio kufanyika kwa miezi mitatu hadi July/August 2020, na kufikia October 2020 tungekuwa tunasafiri kwa treni ya SGR kati ya Morogoro na Dar es Salaam.

Sasa imekuwaje tena, au safari hii kiangazi kimekuwa kikali kimechelewasha SGR? Blah blah za kisiasa nyingi hadi kwenye SGR. Hebu semeni ukweli basi, lini awamu ya kwanza ya SGR itaanza kutumika? Haya mambo ya kukurupuka na miradi mikubwa mingi kwa wakati mmoja matokeo ndio haya.

Source: Tanzania’s standard gauge railway (SGR) to undergo formal testing
Kawia ufike. Mambo mazuri hayataki haraka.
 
Na wewe lazima umeanza kuvuta bangi ya Chato kama wengine. Watu wakisema tusukazie maendeleo ya vitu haina maana hawataki vitu. Tukikuambia usiendekeze ngono haina maana usizae. Mna matatizo ya akili nyie, ndio maana mnadhani upinzani unapinga kila kitu.
Sasa na nyie muwe mnaeleweka sio mnakuwa kama sigara kali, haileweki iwashiwe wapi juu au chini
 
Back
Top Bottom