Mlituahidi SGR Dar - Moro kuwa tayari toka Novemba mwaka jana 2019, hadi leo ni visingizio tu, mara mvua, mahandaki, mara madaraja, blah blah, blah!

Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
9,143
2,000
Tuliambiwa kwamba awamu ya kwanza ya SGR Dar es Salaam kwenda Morogoro, kupitia Pugu, Soga, Ruvu, na Ngerengere ujenzi wake ungekamilika mwaka jana November 2019.

Mkasema ooh, kuna handaki karibu na Morogoro inabidi lichimbwe limechelewasha kazi (yaani kama vile hamkujua kuwa kutakuwa na hilo handaki kwenye SGR), kisha mkasema mvua kubwa zimenyesha zimeondoa madaraja. February mwaka huu 2020 mkaahidi kipande cha Dar - Moro kingekamilika April 2020, na majaribio kufanyika kwa miezi mitatu hadi July/August 2020, na kufikia October 2020 tungekuwa tunasafiri kwa treni ya SGR kati ya Morogoro na Dar es Salaam.

Sasa imekuwaje tena, au safari hii kiangazi kimekuwa kikali kimechelewasha SGR? Blah blah za kisiasa nyingi hadi kwenye SGR. Hebu semeni ukweli basi, lini awamu ya kwanza ya SGR itaanza kutumika? Haya mambo ya kukurupuka na miradi mikubwa mingi kwa wakati mmoja matokeo ndio haya.

Source: Tanzania’s standard gauge railway (SGR) to undergo formal testing
 
Tate Mkuu

JF-Expert Member
Jan 24, 2019
4,645
2,000
Bado kuna ile Stiglers Gorge! Nayo sijui itakamilika lini? Bora tungeanza na kimoja kwanza baada ya kingine mpaka vyote vikamilike kwa utaratibu ambao hautaathiri watu/sekta nyingine kama ilivyo sasa.

Kinyume na hapo, basi Watumishi wa Umma tutaendelea kuumia na kudhulumiwa haki zetu kwa miaka mingine mitano ijayo. Maana sisi ndiyo punching bag la kwanza kabisa la magufuli.
 
Na kibano zaidi kinakuja Mkuu!
 
MUSHEKY

JF-Expert Member
May 9, 2014
2,021
2,000
Tuliambiwa kwamba awamu ya kwanza ya SGR Dar es Salaam kwenda Morogoro, kupitia Pugu, Soga, Ruvu, na Ngerengere ujenzi wake ungekamilika mwaka jana November 2019.

Mkasema ooh, kuna handaki karibu na Morogoro inabidi lichimbwe limechelewasha kazi (yaani kama vile hamkujua kuwa kutakuwa na hilo handaki kwenye SGR), kisha mkasema mvua kubwa zimenyesha zimeondoa madaraja. February mwaka huu 2020 mkaahidi kipande cha Dar - Moro kingekamilika April 2020, na majaribio kufanyika kwa miezi mitatu hadi July/August 2020, na kufikia October 2020 tungekuwa tunasafiri kwa treni ya SGR kati ya Morogoro na Dar es Salaam.

Sasa imekuwaje tena, au safari hii kiangazi kimekuwa kikali kimechelewasha SGR? Blah blah za kisiasa nyingi hadi kwenye SGR. Hebu semeni ukweli basi, lini awamu ya kwanza ya SGR itaanza kutumika? Haya mambo ya kukurupuka na miradi mikubwa mingi kwa wakati mmoja matokeo ndio haya.

Source: Tanzania’s standard gauge railway (SGR) to undergo formal testing
Yani bora corona kuliko upinzani!!

Mwanzoni mliipinga SGR hamuitaki ni matumizi mabaya ya pesa

Leo unakuja na mada ya kulialia eti SGR inacheleweshwa

Cha msingi nyie endeleeni tu na mambo yenu mengine haya ya kwetu tuachieni
 
dist111

JF-Expert Member
Nov 29, 2012
3,316
2,000
Soon treni ya ukweli itaingia, na test trip zitaanza kabla ya uchaguzi.

Wameanza na ubungo nategemea SGR ianze soon kabla ya uchaguzi
 
fazili

JF-Expert Member
Jun 10, 2011
7,226
2,000
Bora corona kuliko CCM...X3
Mkuu, sikupingi ila naomba ufafanue kuhusu mvua, maana mie najua mvua hutokana na mzunguko wa maji yatokayo chini kwenda juu.
Nachopinga kwenye hiyo kauli yako ni kuwa maji yaliyopo juu yapo katika mfumo wa mvuke, kwa tafsiri ya bible haiko hivyo.

Bible inasema maji haijazungumzia mfumo wa maji kama unavyoweka wewe.

Ukiendana na tafsiri hiyo utaona kuwa mfumo wa maji yaliyopo juu ya mbingu na chini ya mbingu ni ule ule.
Yani bora corona kuliko upinzani!!

Mwanzoni mliipinga SGR hamuitaki ni matumizi mabaya ya pesa

Leo unakuja na mada ya kulialia eti SGR inacheleweshwa

Cha msingi nyie endeleeni tu na mambo yenu mengine haya ya kwetu tuachieni
SGR ipo mbioni
Ufipa mnataka kujua maendeleo ya vitu na nyinyi mnahubiri maendeleo ya watu
Soon treni ya ukweli itaingia, na test trip zitaanza kabla ya uchaguzi.

Wameanza na ubungo nategemea SGR ianze soon kabla ya uchaguzi
 
Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
9,143
2,000
Yani bora corona kuliko upinzani!!

Mwanzoni mliipinga SGR hamuitaki ni matumizi mabaya ya pesa

Leo unakuja na mada ya kulialia eti SGR inacheleweshwa

Cha msingi nyie endeleeni tu na mambo yenu mengine haya ya kwetu tuachieni
Kwanza mie sio mpinzani. Pili hiyo sio SGR yenu kwa kuwa inajengwa na fedha za Watanzania. Au siku hizi hamjengi tena na fedha za ndani mnapewa fedha toka Chato?
 
Nyumisi

JF-Expert Member
Nov 10, 2010
4,001
2,000
Kilichotakiwa ni kufanya marekebisho makubwa kwenye maeneo korofi kwenye reli iliyopo. Hii ingesaidia kusave pesa nyingi sana kwa ajili ya maendeleo ya watu ikiwemo maji, afya, barabara, elimu, ajira mpya na kuboresha maslahi ya watumishi. Wajanja wakaja na single ya sgr, stiglaz, ndege za cash huku gas ya mtwara na makaa ya mawe ya kiwira vikiwekwa kapuni.....nchi ngumu sana hii.
 
Azizi J Hamad

JF-Expert Member
Sep 20, 2020
386
250
Tuliambiwa kwamba awamu ya kwanza ya SGR Dar es Salaam kwenda Morogoro, kupitia Pugu, Soga, Ruvu, na Ngerengere ujenzi wake ungekamilika mwaka jana November 2019.

Mkasema ooh, kuna handaki karibu na Morogoro inabidi lichimbwe limechelewasha kazi (yaani kama vile hamkujua kuwa kutakuwa na hilo handaki kwenye SGR), kisha mkasema mvua kubwa zimenyesha zimeondoa madaraja. February mwaka huu 2020 mkaahidi kipande cha Dar - Moro kingekamilika April 2020, na majaribio kufanyika kwa miezi mitatu hadi July/August 2020, na kufikia October 2020 tungekuwa tunasafiri kwa treni ya SGR kati ya Morogoro na Dar es Salaam.

Sasa imekuwaje tena, au safari hii kiangazi kimekuwa kikali kimechelewasha SGR? Blah blah za kisiasa nyingi hadi kwenye SGR. Hebu semeni ukweli basi, lini awamu ya kwanza ya SGR itaanza kutumika? Haya mambo ya kukurupuka na miradi mikubwa mingi kwa wakati mmoja matokeo ndio haya.

Source: Tanzania’s standard gauge railway (SGR) to undergo formal testing
Ewe ndugu mpinzani leo imekuaje hata unaulizia maendeleo ya vitu?

Ooh nimekumbuka kumbe dawa imeshaanza kukuingia ndio maana unaanza kupata ufahamu, kwamba sio maendeleo ya vitu, bali ni maendeleo ambayo mchakato wake utamuinua na kumlinda kila mtu.

Chagua CCM, Chagua Magufuli
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom