Mlitega sungura mkanasa nyati, kwanini muhuzunike?

BUSARA ZANGU

JF-Expert Member
May 5, 2013
779
1,267
Wakuu Nawasalimu

Ninaomba niwape kisa cha wawindaji wawili waliokwenda kuwinda porini na kupata mnyama ambaye hawakutegemea kumnasa na hatimaye kwa haraka haraka wakakasirika kwa kudhani wamepoteza muda, nguvu na rasilimali zao. Sasa nianze:-

Kuna wawindaji wawili walikwenda porini kuwinda, mbinu waliyotumia kuwinda ilikuwa ni kutega mitego kadhaa lengo Lao likiwa kukamata kitoweo cha siku hiyo ambaye ni sungura

Wakati wanatega mitego yao, NYATI maarufu kwa jina la mbogo alikwenda pale mtegoni ili kuvuruga chochote kilichoachwa pale na wale viumbe wawili na hii ilitokana na Kiburi cha Asili alichonacho mbogo

Bila kufahamu kuwa ule ni mtego, tena usiochagua kiumbe cha kukamata, mbogo aliuvagaa ule mtego na ndipo aliponaswa.

Wawindaji wawili walipofika mtegoni walishikwa na mshangao ambao mshangao huo ulikuwa katika mfumo wa hasira, wakilalamika mbogo kuingilia kwenye mtego wao, yaani kwanini wamekama mbogo na si SUNGURA kama kusudi la mtego wao.

Kama bahati, akapita mzee mmoja akawakuta wawindaji hawa, vijana wawili wakiwa kwenye hali ya kuduwaa na kutofurahi hali iliyopo mbele yao. Baada ya mzee kuwauliza hawa vijana wawindaji, na kupata majibu ya nini kinaendelea..... Ndipo mzee alipowaweka chini wawindaji hawa na kuanza kuwapa somo

Kwanza aliwaambia hapa mmepata nyama kubwa kuliko mlivyotazamia kwani nyati/mbogo mmoja ni sawa na SUNGURA wengi tu ambao mngelazimika kuchukua hata siku 100 ili mpate SUNGURA wenye uzito/ujazo wa nyati

Pili, aliwaambia kwanini mlalamike wakati mmedhihirisha mbele ya wanyama wenzake na binadamu wote kwamba anachoonesha sivyo alivyo na mmedhihirisha yeye mnyama mkorofi, kiburi na pupa nyingi.

Tatu mzee aliwashauri, hii nyama ya NYATI mkiwa wajanja mnaweza kuitumia kuanzia sasa mpaka miaka mitatu ijayo kwenye kukidhi haja zenu

Mzee baada ya hapo akawa anaondoka huku anacheeeka, huku akisema kama ukipewa limao usichukie, embu ligeuze kuwa juice nzuri ya limao.

Ukiachilia mbali hao watu 3 (babu na vijana wawili wawindaji) , mimi nilikuwepo kwa mbaaali nafuatilia mtanange huu.

Sasa nasubiri nione kama hawa wawindaji wataufuata huo ushauri ama laa!!!
 
Heshima boss!

Ukisoma MAKUADI WA SOKO HURIA- Prof Chachage Seith L Chachage huwezi kushangaa ni kwanini Chinua Achebe aliikimbia Nchi baada ya kuandika A MAN OF THE PEOPLE (1966).

Alimaliza kitabu huku akionyesha Jeshi kupindua Nchi. Baada ya muda mfupi Jeshi likapindua Nchi. Alihojiwa sana baada ya kudhaniwa ni mhusika wa suala lile. Iweje uandike kitabu kama kile halafu muda mfupi ujao Jeshi lipindue Nchi?. Unahusika! na una la kujibu.

Chinua Achebe alijibu kuwa "Ni kule kuisoma tu Jamii. Mimi siyo mhusika".

Hongera kwa kuisoma Jamii, BUSARA ZANGU .

Hekima Ni Uhuru.
 
Uzuri wa aina hii ya uandishi unaweza piga ndege hata 10 kwa jiwe moja tu
 
Heshima boss!

Ukisoma MAKUADI WA SOKO HURIA- Prof Chachage Seith L Chachage huwezi kushangaa ni kwanini Chinua Achebe aliikimbia Nchi baada ya kuandika A MAN OF THE PEOPLE (1966).

Alimaliza kitabu huku akionyesha Jeshi kupindua Nchi. Baada ya muda mfupi Jeshi likapindua Nchi. Alihojiwa sana baada ya kudhaniwa ni mhusika wa suala lile. Iweje uandike kitabu kama kile halafu muda mfupi ujao Jeshi lipindue Nchi?. Unahusika! na una la kujibu.

Chinua Achebe alijibu kuwa "Ni kule kuisoma tu Jamii. Mimi siyo mhusika".

Hongera kwa kuisoma Jamii, BUSARA ZANGU .

Hekima Ni Uhuru.
Storu za vijiweni,
 
Acha tu nile hili limau na uchachu wake huku nikisubiria hii miaka mitatu mchungwa wangu uanze kutoa machungwa,sina sukari ya kuongeza ili iwe juice tamu
 
Nimejaribu kuwaza mbogo ni nani,wawindaji ni nani, sungura ni kina nani,huyu mzee alitoa ushauri halafu akachapa mwendo,kitoweo cha miaka mitatu nk....mkuu nimenasa,hebu ngoja nirudie tena kusoma!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom