Mlipuko wa Virusi vya Corona, Shauku ya Ajira kwa Vijana Tanzania na maandaliizi ya maandalizi ya Mwaka wa Fedha 2020/21

Freddie Matuja

JF-Expert Member
Jul 21, 2018
1,462
2,855
Magazeti ya leo yamekuwa na story ya Trilioni zaidi ya 30 kwa mwaka ujao wa fedha.

Suala la kusambaa kwa virusi vya Corona (COVID 19)duniani kote nalo limenifikirisha kwenye angle nyingine. Maana dunia haikujua kama ambavyo sisi Watazania pia hatukujua athari yake upande mmoja wa China sasa limesambaa Ulaya hususan Italia.

Hatua imefikia viwanja vya michezo, migahawa ya huduma ya chakula kwa sasa imefungwa. Hakuna biashara hakuna mzunguko wa fedha, na huenda kuna fedha zitatakiwa kurejeshwa kama huduma haikutumika kwa muda.

Sasa hivi hata Viongozi wanagonga miguu au hi 10 bila kugusana kwa uwoga wa kusambaza maambukizi.

Mathalani, kama ni ticket ya ndege mtu alikata kwenda kwenye mkutano au mafunzo ndani ya muda fulani, kwa kuvunjwa safari za ndege, hotels zitakosa wateja, vyakula vitashindwa kuuzwa kama ni perishable foods kama matunda na mbogamboga. Harasa juu ya hasara.

Kwa upande wa bidhaa za viwandani kuna mahali zimeanza kupungua ikiwemo baadhi ya nchi za Afrika Mashariki kwa kuwa China ilikuwa ndiyo soko la jumla (wholesale) na nchi zetu zimekuwa soko la rejereja (retail) kwa ajili ya mlaji/mtuamiaji wa mwisho wa bidhaa au huduma.

Nije kwenye mada ya msingi; Ajira kwa vijana wa kizazi cha sasa na kizazi kijacho. Kwa mtazamo wangu kiuchumi na kijamii mifumo ya ajira rasmi ina faida kubwa kwenye nchi au jamii ya Tanzania kuliko mifumo ya ajira zisizo rasmi. Nitoe mfano hai.

Kutokana na mfumo wa ajira rasmi, waajiri na waajiriwa wanachangia 20% ya mshahara na ndipo mashirika ya pensheni (NSSF na PSSSF) Ikumbukwe PSSSF amezaliwa kutokana na PPF, PSPF, LAPF, GEPF.

Then, shirika la bima ya Afya NHIF lilianza wakati wa Rais Mkapa kwa wafanyakazi hasa wa serikali kuu wakati huo, kuchangia 3% ya mshahara na muajiri 3% ya mshahara. Kwa sasa kuna WCF ambayo ni fidia ya mfanyakazi kama atapatwa na majanga. Th

Then kuna income tax au PAYE anayokatwa mfanyakazi baada ya kutoa michango ya mfuko wa pensheni.

Kwa lugha nyingine, uki-reverse ajira zisiwepo watu wafanya kazi mmoja mmoja ni isolation bila organized system; ina maana baada ya hapo uhakika wa makusanyo ya mifuko ya pesheni italegea. Mifuko ya pesheni kama haina wateja (wafanyakazi) wanaochangia itapunguza staff au kufuta kabisa operations, kodi ambayo serikali inge-project kwa kuwa na tax base ya staff hawa ntapata hiki, nayo itapotea

Ni ngumu sana kujenga stable economy kwa watu kujiajiri kama wamachinga wa wachuuzi wa biashara ndogondogo. Inawezekana kujenga mfumo kama una wakulima wachache wanaolima kwa mfumo wa umwagiliaji na kuna projection ya mavuno kwa ajili ya soko fulani.

Mathalani, inawezekana kuwekeza kwa kuwa na mkulima mmoja au wawili wenye ng’ombe 9,000 wa maziwa kwa ajili ya kumuuzia say bakheresa ili asindike badala ya kuendelea kunua maziwa India ambapo yakija Tz Anaya-reconstitute.

Shamba la ng’ombe 9,000 litakuwa na staff wa malisho ya ng’ommbe, staff wa afya ya wanyama, staff wa logistics za maziwa kufika kiwandani, staff wa maslahi ya wafanyakazi, staff wa legal kwa ajili ya wafanyakazi na kiwanda, staff wa masoko kama soko moja la kiwanda litajaa, staff wa accounts kufuatilia malipo, staff wa storage ili ku-monitor flow in and flow out ya maziwa.

Either, shamba hili laweza kulazimisha uwepo wa kufungua kiwanda cha madawa ya mifugo kwa ajili ya hawa ng’ombe 9,000 walio katika organized farm.

Tukirejea kwenye msingi wa mada, taasisi zetu kama TRA, NHIF, mifuko ya pesheni, mabenki yanayoishi kwa mikopo ya wafanyakazi na huduma zingine za kifedha kwenye corporates ambazo zinazalishwa kwa kuwa kuna staff,

Je, zina mkakati gani wa kuzalisha ajira katika mfumo rasmi ili kuwa na uhakika wa kodi zaidi (kama ni TRA. Kodi PAYE, kodi ya manunuzi ya huduma na bidhaa); Uhakika wa michango zaidi wa wanachama kwenye oragazed institutions (kama ni NHIF au NSSF au PSSSF)

Strategy begins before the bolicies. Na kuna wakati kwa kuwa tuko vitani strategy huwa inafichwa ila inakuwa na maandalizi ya kina nyuma ya pazia ili kukidhi uhutaji wa soko lililopo.

Wakati Wizara ya fedha inakwenda kwenye maandalizi ya bajeti ya 2020/21; kuna mkakati walau wa kushirikiana na private sector ili mwisho wa mwaka wa bajeti walau makampuni 50 yazaliwe. Kila kampuni liwe na uwezo wa kuzalisha kwa mahitaji ya soko la ndani nan je na kila kampuni litoe ajira walau 200. Maana yake mwisho wa mwaka tuna hakika ya kazi 1000 (white collar jobs)

Kazi zikizalishwa huwa zinazaa athari kama virusi wa corona; Hela yake inasambaa. Watu anaoa na kuolewa na kuzaa watoto, watoto wanasoma shule zenye hadhi kwa kuwa “wallet” zinamudu huduma. Wenye nyumba wapangisha, wenye biashara wanatangaza kwa radio/tv other media outlets. Mzunguko wake kwa ndani ni mkubwa sana kuliko tunavyodhania. Kama athari ya corona.

Kuna mifumo ya kutengeneza organized industrial production projects ambazo fedha zake zinasambaa. Ukifika Mafinga (Iringa) mbao na chai zina athari chanya hasa mafinga na Iringa kwa ujuma. Fika Kahama, athari ya migodi ya Kahama (in term of purchasing power na cashflow)sio sawa na migodi isiyo organized kama Nyarugusu.

Wale wa zamani kidogo Mwatex enzi zile effect yake kwa Mwanza was superb, Polytex Moro, Urafiki na Sungura Tex, Mutex kuliko miaka hii tupouza pamba raw. The list goes on. Corona (COVID 19) ni ugonjwa, falasafa yake naiona kwa angle tofauti. Enzi zile soko la mafuta ya kula yatokanayo na mbegu za pamba yalikuwa yanalika sana Tanzania.

Kulikuwa na Tanbond kama siagi itakonayo na mafuta ya pamba. Leo Kenya wanauza Prestige na Blueband na fedha tunayonunua inakwenda Kenya kwenye mifumo ya viwanda kuajiri Wakenya wakati tungetengeneza ndani, hizo fedha zingebaki humu kwa wingi.

Wizara ya fedha, viwanda na uwekezaji, wizara ya vijana na ajira je wanaona kwa jicho hili ??

Kama tunaandaaga bajeti kwa mazoea pasipo mikakati na fikra mbadala na fikra za kimkakati na jumuishi kwenye kutengeneza uwekezaji ambao soko lake lipo kwa kupunguza imports, kila mwaka kuna watu watakuwa wanashangaa shangaa tu bila kuelewa kwanini bajeti inaandaliwa na ina athari gani kwenye maisha yao ya leo na kesho yao na Taifa kwa ujumla.

Tusiache suala la kutotengeneza nafasi za kazi kama jambo la kawaida. Watanzania tupo tuofikiria mbadala kwa kutumia vyanzo hivi hivi vya ndani ili kuwa na kile Tanzania vision 2025 inasema "A competitive economy capable of producing sustainable growth and shared benefits"

Wasalaam
 
Nimeshindwa kukuelewa; unamaanisha watu wakiajiriwa wanaongeza risk ya kupata COVID-19, kwanini iwe hivyo, kwani CORONA ipo maofisini pekee?

Then again, hizo kampuni 200 unazozungumzia haitakuwa rahisi kuanzishwa na sekta binafsi, kwasababu kwanza serikali ingeongeza ufanisi kwa sekta binafsi, ikiwa ni pamoja na kuwapa tenda mbalimbali za serikali ili waanze kujimudu kwa kipato, hii itawezesha sekta binafsi kuanza kuwa na nguvu ya kuajiri.

But as we are talking, tenda nyingi za serikali bado zinapewa taasisi za serikali, mfano, Suma JKT na nyingine, kazi nyingi siku hizi wanapewa hao, hii ni kwasababu aliyepo madarakani anaonekana kuwaamini zaidi, hivyo kuzidi kuiminya sekta binafsi, kama wanataka sekta binafsi ijimudu waanze na hili.

Mwisho, mara nyingi budget ya serikali kwa kiasi fulani hutegemea wahisani, hii husababisha project zilizokuwa intended kunufaishwa na budget husika kupata kiasi kidogo endapo wahisani hawatasaidia, hasa ukizingatia kipindi hiki tunavyonyooshewa vidole huko nje, hii itasababisha lengo lililodhamiriwa kutofikiwa, bado hatujawa na uwezo wa kujimudu 100% kwenye budget yetu.

All in all sidhani kama your wishes kwenye thread yako zitafanikiwa, bado kuna vikwazo vya ndani na nje kama nilivyokuonesha hapo juu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimeshindwa kukuelewa; unamaanisha watu wakiajiriwa wanaongeza risk ya kupata COVID-19, kwanini iwe hivyo, kwani CORONA ipo maofisini pekee?

Then again, hizo kampuni 200 unazozungumzia haitakuwa rahisi kuanzishwa na sekta binafsi, kwasababu kwanza serikali ingeongeza ufanisi kwa sekta binafsi, ikiwa ni pamoja na kuwapa tenda mbalimbali za serikali ili waanze kujimudu kwa kipato, hii itawezesha sekta binafsi kuanza kuwa na nguvu ya kuajiri.

But as we are talking, tenda nyingi za serikali bado zinapewa taasisi za serikali, mfano, Suma JKT na nyingine, kazi nyingi siku hizi wanapewa hao, hii ni kwasababu aliyepo madarakani anaonekana kuwaamini zaidi, hivyo kuzidi kuiminya sekta binafsi, kama wanataka sekta binafsi ijimudu waanze na hili.

Mwisho, mara nyingi budget ya serikali kwa kiasi fulani hutegemea wahisani, hii husababisha project zilizokuwa intended kunufaishwa na budget husika kupata kiasi kidogo endapo wahisani hawatasaidia, hasa ukizingatia kipindi hiki tunavyonyooshewa vidole huko nje, hii itasababisha lengo lililodhamiriwa kutofikiwa, bado hatujawa na uwezo wa kujimudu 100% kwenye budget yetu.

All in all sidhani kama your wishes kwenye thread yako zitafanikiwa, bado kuna vikwazo vya ndani na nje kama nilivyokuonesha hapo juu.

Hakuna mhisani taanzisha mradi wa uwekezaji unaokuwa na conflicting interest na fursa za kule kwao hamna.

Say, kampuni kama YARA wanatengeneza mbolea toka Nordic countries na kuuza duniani kote. Sio rahisi wa-Nordic wakawekeza hapa kwenye kiwanda cha mbolea ili ki-comprete na YARA kupunguza ajira za wazungu wenzao, never.



Sent using Jamii Forums mobile app
Kama SUMA JKT anafanya kile ambacho kinaweza kupunguza imports na kuwa chanzo cha ajira wa Watanzania hilo ni jema kwa maana watakaofanya kazi ni Watanzania, kama wafanyakazi 1000 watatokana na initiative ya SUMA JKT basi, kuna ripple effect (ambayo kwa muktaadha wa wangu) nimeifanyanisha na kusambaa kama virusi.

Na nimetoa mifano ya miji na jamii zinavyokuwa kwa uwepo wa organized white collar jobs vs kujiajiri kwa kuchuuza mitumba au toothpick au chochote kile ambacho kingekuwa imported ambacho kuna nafasi ya kukitengeneza humukumu ndani.

Mtanzamo wangu sio miradi ya barabara na reli ambayo ripple effect yake sio quick. Kuna vitu vya haraka tu.
Mfano hata kama ni SUMA akiwekeza kwenye ku-process ngozi na kuzalisha products za ngozi kama mikoba, mikanda, viatu, wallet na tukapunguza imports based on uhakika wa ngozi ghafi mbona hiyo ni deal.

Anyway, kama wakubwa wasiponunua fikra mbadala sina na hatuna cha kuwafanya. Maana ushauri unapotolewa, mshauriwa halazimiki kufuata nini mshauri anafikiri au kudhania.
 
Unataka kumkasirisha jiwe...
Sidhani kama atakasirika leo ukimhakikishia (kama akitia mkono wake inawezekana hata sio pesa) unatengeneza ajira say 200, unapunguza imports anapata uhakika wa income tax (PAYE) walau, then its obvious anapata indirect tax based on spending power ya hawa watu, 200, kwenye kila corporate purchase ya umeme, maji, other consumables kuna other deductions za VAT, REA, EWURA; huyu mzee bila shaka ata-buy in.
 
Back
Top Bottom