mlipuko soweto

fred mswelo

New Member
Jun 13, 2013
1
0
mlipuko wa bomu la kutupwa kwa mkono umetokea mara baada ya kumalizika kwa hotuba ya mh freeman mbowe viwanja vya soweto
 
mrushaji atakuwa alikosea timing atakuwa alikuwa anamtaka mbowe sasa kachelewa gd blss tz!! hali sasa inatisha sana kwa kweli kama mambo yapo ivi tuna hali ngumu na hayo mabomu yatoka wapi???inabidi polisi waulizwe, na nina mashaka na uchaguzi ujao nahisi mengi yamehifadhiwa kusubiri uchaguzi
 
Huko arusha kuna matatizo makubwa sana. Usalam wa taifa inabidi wapaangalie sana. Hii ni mara ya pili mabomu yanalipuka, je kuna nini huko arush?. Ina maana haya mabomu yanasambazwa na kikundi fulani, ambacho lengo lao sio jema kwa tanzania. Tukumbuke, moto mkubwa mno, huanza kwa cheche ndogo sana.
 
Serikali imekuwa ikifunika kikombe ili mwanaharamu apite kwa mambo mengi yaliyopita na sasa basi yatosha niwakati wa jeshi la police sasa kukubali wameshindwa kazi yao ili taifa na serikali kwa ujumla wajue la kufanya na uwajibikaji wa police wa Arusha sasa wanatakiwa kuwajibika
 
mara baada ya mlipuko mshukiwa alipandishwa kwenye gari la polisi na aliokolewa kwa kutumia mabomu ya machozi.
Polisi wasije na taarifa ya kutokamata mtuhumiwa ,wakifanya hivyo watathibitisha ushiriki wao katika mauaji haya.
 
Mie mwenyewe nimefuatilia hii kitu hadi nimeogopa..!!
Nasikia wananchi walikuwa wanamfukuza alierusha bomu maana walimwona... kuona hivyo polisi wakaanza kuwapiga wananchi mabomu ya machozi...!!

Hapa kuna jambo, tena baya sana....!!
 
Alafu mama aliye onyesha mtu aliye rusha bomu walimtandika risasi ya kifua polisi hao.
 
mara baada ya mlipuko mshukiwa alipandishwa kwenye gari la polisi na aliokolewa kwa kutumia mabomu ya machozi.
Polisi wasije na taarifa ya kutokamata mtuhumiwa ,wakifanya hivyo watathibitisha ushiriki wao katika mauaji haya.
Najua una hasira ndo maana unaongea point na pumba humo humo. Police imempa hifadhi mtuhumiwa kwa maana hiyo ni kweli watakuja na taarifa ya kutokumkamata mtuhumiwa..!
 
Atakuwa Ni AMBROSE tena huyo,hawa polccm kwa kazi mimi nawakubali sana,subiri utasikia majibu yao ya kisiasa as usual
 
Back
Top Bottom