Mlipuko mpya wa virusi vya Corona waibuka jijini Beijing, China kutoka kwa samaki kwenye soko la vyakula la Xianfadi

pingli-nywee

JF-Expert Member
Sep 16, 2015
11,923
13,344
Wakazi wa Beijing wamerudi kwenye hali ya taharuki ya hapo awali janga la Corona lilipoibuka baada ya serikali yao kuweka sehemu za jiji lao kwenye total lockdown na kuwashurutisha maelfu ya watu kupimwa. Hii inafatia mkurupuko mpya wa COVID-19 ulioibuka kutoka kwa samaki aina ya 'Salmon' ndani ya soko la vyakula vya Xianfadi.

Hadi sasa hivi walioambukizwa kwenye mkurupuko huo mpya ni watu 106. Wataalamu wa afya walifanya uchunguzi baada ya watu 27 kupatikana wana virusi vya Corona hapo awali na kupata sampuli +ve kutoka kwa mbao ya kukatia samaki ndani ya soko hilo. Kabla ya hapo siku 56 zilikuwa zimepita kabla ya jiji la Beijing kupata hata kesi moja tu ya maambukizi ya ndani kwa ndani ya virusi vya COVID-19.

Beijing yaripoti visa vipya 31 vya Corona, Mamlaka zatangaza masharti zaidi ili kudhibiti mlipuko
 
MBAO YA KUKATIA SAMAKI INA CORONA?
ndo maana mimi nasema kwenye corona nipo na magufuli
Boss, mkurupuko wa hapo awali wa virusi hivyo, ambao umeua maelfu ya watu kote duniani hadi sasa hivi ulianza hivyo hivyo. Kutoka kwa soko la vyakula kama samaki, nyoka, popo n.k. ila ilikuwa kwenye mji wa Wuhan sio Beijing.
 
Nazungumzia hyo mbao ya kukatia samaki.
Boss, mkurupuko wa hapo awali wa virusi hivyo, ambao umeua maelfu ya watu hadi sasa hivi ulianza hivyo hivyo. Kutoka kwa soko la vyakula kama samaki, nyoka n.k. ila ilikuwa kwenye mji wa Wuhan sio Beijing.
 
Hyo na ile ya Magufuli Ina tofauti?
Wataalamu wamefanya tracing ya virusi hivyo kwenye soko hilo hadi wakapata virusi kwenye 'chopping board'. Kumaanisha kuna nyama ya kiumbe flani ilikatiwa kwenye mbao hiyo na ilikuwa na virusi hivyo, sio mbao yenyewe. Umeelewa sasa?
 
Wanasayansi kimia saivi wa chanjo ya corona, huu ugonjwa pasua kichwa sana.

Huu tutaishi nao kama HIV ilivyo sanda kuisha na dawa kukosekana.
 
Wakazi wa Beijing wamerudi kwenye hali ya taharuki ya hapo awali janga la Corona lilipoibuka baada ya serikali yao kuweka sehemu za jiji lao kwenye total lockdown na kuwashurutisha maelfu ya watu kupimwa. Hii inafatia mkurupuko mpya wa COVID-19 ulioibuka kutoka kwa samaki aina ya 'Salmon' ndani ya soko la vyakula vya Xianfadi. Hadi sasa hivi walioambukizwa kwenye mkurupuko huo mpya ni watu 106.

Wataalamu wa afya walifanya uchunguzi baada ya watu 27 kupatikana wana virusi vya Corona hapo awali na kupata sampuli +ve kutoka kwa mbao ya kukatia samaki ndani ya soko hilo. Kabla ya hapo siku 56 zilikuwa zimepita kabla ya jiji la Beijing kupata hata kesi moja tu ya maambukizi ya ndani kwa ndani ya virusi vya COVID-19.

New Coronavirus Outbreak in Chinese Capital
Corona inakuzwa sana lakini haipo
 
Daudi Mchambuzi,

Eleza tofauti usijifiche kwenye kichaka unachojaribu kutengeneza. Zote zilikuwa na aim moja; kutambua uwepo wa DNA ya kirusi kwenye hivyo vitu. Sasa utofauti upo wapi?
 
pingli-nywee,

Habari ya chini ya kapeti zinasema uchina imeanza kuulizia kuhusu korona tz na kuuliza ambassador wake kama ni kweli tz watu wanaishi maisha ya kawaida bila kusumbuliwa na korona baada ya barozi kuthibitisha kuwa ni kweli serikali ya China imeona isiwe tabu imetuma watu wake kushirikiana na tz kuhusu njia za tiba tunazo tumia pamoja na kujifukiza na mitishamba
 
Habari ya chini ya kapeti zinasema uchina imeanza kuulizia kuhusu korona tz na kuuliza ambassador wake kama ni kweli tz watu wanaishi maisha ya kawaida bila kusumbuliwa na korona baada ya barozi kuthibitisha kuwa ni kweli serikali ya China imeona isiwe tabu imetuma watu wake kushirikiana na tz kuhusu njia za tiba tunazo tumia pamoja na kujifukiza na mitishamba

Waje tuwape tiba
 
Back
Top Bottom