Mlipuko mkubwa watokea mji mkuu wa Lebanon, Beirut. Watu zaidi ya 78 wafariki na zaidi ya 4,000 kujeruhiwa

Ni kama mlipuko wa kemikali..amonia. inawezekana pia ni kuficha ushahidi maana mlipuko umetokea kwenye ghala linalotumika kuhifadhi vitu vilivyotaifishwa au kuzuiwa hapo bandarini. Labda kuna mzigo ulishikiliwa huko sasa wahuni wakafuta ushahidi kwa kulipua.

Israel imekana kuhusika hadi sasa...ila naona mfaransa na iran wamekomalia hiyo show sijui kuna nini hapo kati.

Beirut ni kitovu cha ujasusi na uzandiki duniani. Pale ndio makutano ya combination za michezo yote ya east, west na middle East. Hivyo ngoma mbichi kabisa hiyo. Tuipatie muda itajulikana tu.
Mi naomba Israel awe hajahusika,maana hao hezibullah kwa hiyo michezo ni hatari sana,halafu walipuaji wa vikundi vidogo hawawezi kuwa na bomu la tani kubwa kiasi hicho,hapa labda ni nchi fulani imefadhili...
 
Hahahaha mwenye Mbwa Iran mpaka leo hii haijajibu kitu sembue huyo
IRAN ajibu nini kuna siku umesikia ISRAEL kaigusa IRAN akijitia ujinga wakuigusa mchana usiku mtaitafta nahamtakaa muione ilipo

Israel adil na hamas nakwambia nanakuhakikishia akijulikana kahusika hatakwapunje yamtama atateseka mnoooo.....
 
Ukiangalia kwa mbali nawaza Yale mkazi ya Mzee Nyerere,pia makazi ya Mzee Mkapa pale butiama na lupaso !!sasa linganisha msoga na chato tukianza kupigana hapa bongo nitalipua bagamoyo yote halafu mwanza yote nateketezaaaa yaani hatuwezi kupakwa unafiki matokeo ndio hayooo watu tumenyamaza huku tukiangalia mchezo

Unalipua ukiwa kitandani au wp
 
Unaweza kutuwekea ushahidi?
Naamini ni utunzaji mbovu wa silaha kwenye ghala. Anayesema ni Hezbollah, hawa hawana makazi eneo hili la Beirut wao wako field za nje ya miji uko na juzi hapa Israel imedai wana roketi zimeelekezwa kwao.
Ajari itakuwa ni kutokana na depot ya milipuko maana tumeona rangi za mafataki kwanza kisha mlipuko mkubwa. Kuwepo kwa mushroom cloud na shockwave kunafanya iwepo imani ya some sort of nuclear warhead ndogo sana.

Hata hivyo kuna uwezekano Israel anahusika kwa kujishikiza kwenye uzembe wao. Maana bandari hupokea baadhi ya silaha kutoka Iran kwenda Hezbollah lakini mara nyingi wanatumia mpaka wa Syria ambao hushambukiwa sana na Israel.

Taarifa za awali za serikali zinaonesha ni ajari, ingekuwa shambulizi Hezbollah wangeshajiapiza muda mrefu. Israel hapendi vita hata wiki iliyopita wapiganaji wanne wa Hezbollah waliingia mipakani lakini command ya jeshi ikaomba ruhusa ya kushambulia kwa Netanyahu akakataa ikabidi wawaache watoke. Ukishambulia Hezbollah wanajibu, hii sio Gaza ambako hawana technology ya kujitutumua. Mwaka 2006 kulitokea upinzani mkali dhidi ya Hezb, mwaka 2013 wakati Israel anashambulia Gaza strip walikuwa wanajibu na viroketi vichache. Hezb ina mkono wa Iran, ina engineers, technicians, commando unit, na roketi za masafa ya kati. Ni jeshi lisilo na mamlaka kamili na lisilo rasmi lakini lenye nguvu kuliko jeshi la nchi. Ni kama Iran (walimu wao) ilivyo na IRGC na jeshi la nchi.
Wale watu manne walioingia mipakani Israel iliwafyeka hawajaachwa
 
Ni kama mlipuko wa kemikali..amonia. inawezekana pia ni kuficha ushahidi maana mlipuko umetokea kwenye ghala linalotumika kuhifadhi vitu vilivyotaifishwa au kuzuiwa hapo bandarini. Labda kuna mzigo ulishikiliwa huko sasa wahuni wakafuta ushahidi kwa kulipua.

Israel imekana kuhusika hadi sasa...ila naona mfaransa na iran wamekomalia hiyo show sijui kuna nini hapo kati.

Beirut ni kitovu cha ujasusi na uzandiki duniani. Pale ndio makutano ya combination za michezo yote ya east, west na middle East. Hivyo ngoma mbichi kabisa hiyo. Tuipatie muda itajulikana tu.
Iran lazima akomalie hiyo show maana hizbolah ni derivative yao, na mfaransa ni muuza bidhaa za nyuklia wa siri mashariki ya kati.
 
Israel was ruled out. Tangu mwanzo Israel huwa haina bifu na Lebanon bali ina bifu na Hezbollah. Hezb yenyewe iliomba kuwepo umoja katika tukio hili, hawajajiapiza kama wanavyofanyaga mara zote. Maana yake mpaka wao wanaamini ni ajari, ingawa najua wanachunguza kivyao.

Mkuu wa Usalama na Waziri Mkuu wamesema kulikuwa na ammonium nitrate tani 2750 zimehifadhiwa kwenye ghala kwa kipindi cha miaka 4-6. Hizi hutumika kutengeneza mabomu na mbolea, nyingi serikali ilikuwa inazikamata kama magendo. Kuna uzembe wa mamlaka za bandari. Mafataki pia yalikuwepo, moto ulianza kwa namna nyingine ndipo ammonium nitrate ikalipuka. Chanzo cha huo moto wa mwanzo ambao ulikuwa unatoa flash nyeupe za mwanzoni ndo bado kujulikana. Kuna mchanganyiko wa explosive substances maana ni kama warehouse ya milipuko ya aina yote. Ndo maana kuna moshi mweupe, yellow, na rangi gani sijui.

Naamini nchi nyingi zitatoa msaada maana Lebanon ni ndogo. Israel yenyewe imesema ina mazungumzo kupitia third party kutoa msaada. Qatar inatuma vitanda vya dharula kwa majeruhi, Saudi Arabia inakuja, Turkey, Iraq na wengine.
Trump kama kawaida yake anatoa taarifa bila uhakika, alidai inaonekana ni shambulizi. Kauli yake itapuuzwa.
 
mi naomba israel awe hajahusika,maana hao hezibullah kwa hiyo michezo ni hatari sana,halafu walipuaji wa vikundi vidogo hawawezi kuwa na bomu la tani kubwa kiasi hicho,hapa labda ni nchi fulani imefadhili...
Iran anaemfadhili Hezibullah kila siku analipuliwa sehemu zake nyeti na hajalipia mpaka sasa.
 
Wale watu manne walioingia mipakani Israel iliwafyeka hawajaachwa
Taarifa za Israel zinasema zimewaacha, intelligence ya Iran inasema wameachwa, wewe unasema hawajaachwa.

Israel nowadays haiui members wa Hezbollah, kwakuwa wanalipiza. Kwa kipindi hiki Netanyahu ana maandamano, serikali bado haijatengamaa, alikuwa na annexation plan, kuna US election na uchumi mbovu. Ikitokea mapigano yoyote raia watalaumu sana. Hezbollah wanajua hili, Iran wanajua na Israel inajua kuwa wanajua. Ndiyo maana Iran na Syria siku hizi zinawachukua wapiganaji wa Hezbollah kisha zinaifanya Israel ijue, Israel wenyewe wanaita hii mbinu "new antiaircraft weapon".

Hao jamaa wanne waliingia kisa shambulizi moja lililoua member wao, walipoonekana vikosi vikaomba ruhusa ya engagement ambayo ilifika mpaka kwa Waziri Mkuu, hii haitokei siku za nyuma kanali tu alikuwa anaruhusu kushambulia mtu yeyote mwenye silaha akivuka mpaka. Polisi wanaua Wapalestina wanaoandamana lakini jeshi linajitahidi kukwepa kuua Hezbollah mpaka PM mwenyewe hataki mzozo.

Hata Hezb yenyewe inajua kuna uchumi mbovu wakianza mapigano wataamsha hasira za raia.
 
Kuna mlipuko mkubwa sana umetokea Lebanon muda si mrefu, inasemekana silaha na milipuko ya Hezbolah ndio imeharibiwa na intelijensia ya Israel..

Picha linaendelea..
====
Mlipuko mkubwa umepiga mji mkuu wa Lebanon, Beirut, huku kukiwa hakuna uthibitisho kuhusu mlipuko wa pili

Mlipuko mkubwa umetokea mjini Beirut wakati kukitarajiwa uamuzi kuhusu kesi ya mauaji ya Waziri Mkuu wa zamani Rafik Hariri mwaka 2005.

Ripoti zinasema kuwa mlipuko mkubwa umetokea kwenye eneo la bandari la mji huo, huku kukiwa hakuna ripoti za kutokea kwa mlipuko wa pili. Mamlaka zinahofu kutokea kwa madhara makubwa.

Video iliyowekwa mtandaoni imeonesha uharibifu mkubwa uliotokana na mlipuko huo.

Mahakama ya Umoja wa Mataifa inatarajiwa kutoa uamuzi kuhusu kesi ya washukiwa wanne wanaoshukiwa kuhusika na mauaji ya bwana Hariri.

Wafuasi wote wanne wa kundi la Hezbollah, wamekuwa wakikana kuhusika na kifo cha Hariri. Uamuzi wa mahakama utatolewa siku ya Ijumaa
Ripoti kuhusu uwezekano wa kutokea mlipuko wa pili katika makazi ya bwana Hariri imetolewa.

Waziri wa afya wa Lebanon Hamad Hasan amezungumzia kuhusu majeruhi wengi na uharibifu mkubwa uliojitokeza.

Shirika la habari la Reuters limenukuu vyanzo vya habari vikisema miili kumi imetolewa kutoka kweny kifusi.

Vyombo vya habari nchini humo vieonesha watu wakiwa wamenasa kwenye vifusi. Shuhuda akieleza jinsi mlipuko huo wa kwanza ulivyokuwa wa kishindo na sauti kubwa.

Sababu ya mlipuko huo bado haijafahamika.

Ripoti hii imekuja wakati kukiwa na mvutano wa kisiasa nchiniLebanon, huku maandamano yakitokea mitaani dhidi ya serikali kuhusu namna wanavyoshughulikia changamoto za kiuchumi tangu vita vya wenyewe kwa wenyewe vya mwaka 1975-1990.

UPDATES
WATU ZAIDI YA 25 WAFARIKI DUNIA KATIKA MLIPUKO WA BEIRUT, LEBANON

Takriban watu 25 wamefariki dunia na wengine zaidi ya 2,500 wamejeruhiwa katika mlipuko huo ambao chanzo hakijafahamika

Mlipuko huo umetokea katika eneo la bandari la Beirut

UPDATES
Waziri wa Afya, Hamad Hassan amesema Watu zaidi ya 50 wamepoteza maisha na wengine zaidi ya 2,750 wamejeruhiwa kufuatia mlipuko uliotokea eneo la bandari ya mji huo

Mlipuko huo pia umetuma mawimbi yaliyosababisha majengo mengi mbali na eneo la mlipuko, kutikisika, kuvunjika madirisha na milango
Ukiutazama mlipuko huo video yake ina viashiria kuwa ni ya kutengenezwa:
Mosi: moshi unaoanza kufuka unaashiria kuwa ni mlipuko wa bomu la atomic, sidhani kama ni rahisi kwasasa (ethically) kwa jeshi kutumia bomu la ainahii.

Pili: mlipuko wa chini unaonesha kama ni bomu la kawaida tena la kutegwa na si la kutupwa. Combination hizi mbili zinashiria kuwa video ni ya kutengenezwa. Period.
 
Back
Top Bottom