Mlipuko mkubwa watokea kwenye Kanisa Katoliki Arusha, watu kadhaa wajeruhiwa

Status
Not open for further replies.
Tufafanulie ndugu, tafadhali sana. Je mlipuko wa nini? Umesabishwa na nini? Wakati gani (wakati wa misa, kabla au baada)? Nani anahusika? Hizi habari nyigine........
KWA USHAURI TU: ukitaka kuandika habari, andika ikamilike. Tambua ya kwamba wanaotumia Jamii Forums ni watu wenye akili timamu, na wengine wananyadhifa kubwa sana serikalini. Hivyo kuandika sawia itawapa mwanga.

acha ujinga wewe!
Mtu kaposti kadiri ya information aliyopata, halafu wewe unam-dril kiasi hicho eti atoe info kamili: aaaaaaaah nonn sense!

JF ni newz breaker! Sasa undani wa tukio au habari zaidi tutazidi kupata kadiri ya habari inavyozidi kuingia! Kumbuka mtoa habari hana obligation yeyote zaidi ya utashi na uelewa wake wa kutaka kutujuza

Mimi watu mnapewa news halafu mnaanza kumnanga au ku-demand upewe full mkoba; kama vp wewe nenda eneno la tukio kapata habari kamili.

Hope umenisoma, na ubadilike mkuu!
 
Waislamu walichokozwa lini? Walichokozwaje? Jamani, yamesemwa na Rais haya kweli?
...MTOTO wa kikristu aliyeshawishiwa na MTOTO wa kiislam alikojolea kurani - Hukusikia hotuba ya mwisho wa mwezi wa pili wewe.
 
Mimi binafsi sitafurahi kumsikia huyu mnafiki kikwete akitoa salam za pole kwa wale walioathiriwa na hili tukio,najua atafanya hivyo ili kujikosha ila ukweli ni kwamba huyu jamaa ni adui mkubwa wa wawakristo.simpendi kama nini!
 
Kamanda Lema anaingia, Radip Maria wana report kuwa watu ni Full Kutabasamu
 
Haya ndio watawala wetu wanayataka. Sijajua nani amehusika, ila ukweli ni kuwa uwezi tenganisha hili na choko choko za udini na ujinga unaendelea kwenye nchi yetu. Haya ndio matunda yake, sijui ifikie kiwango gani mpaka hawa watawala wetu dhaifu waone kuwa watanzania tunakwenda kuuana kuku muda si mrefu. Sasa tumefikia kiwango cha Nigeria, Iraq, Syria, n.k. Hakika sasa Tanzania sio kisiwa cha amani tena.
Walianza kukashifu na kutukana wenzao wakaona kimya hawajibiwi. Walipoona wanalalamikiwa na kudhibitiwa wakaona haitoshi sasa wameanza kupiga mabomu. Hao ndio alqaeda na al shaabab, wamekaribishwa wameingia sasa tutakiona.
 
Watanzania wenzangu, Kwanza niwape pole kwa yaliyotokea Arusha asubuhi hii, hili ni tukio la kusikitisha na linalostahili kulaaniwa na kila mpenda haki na muumini wa uhai duniani bila kujali dini yake. Kwa haraka haraka napeleka lawama zangu kwa waislamu wenye msimamo mkali. Lakini naomba nieleweke na mnielewe, hili ni kundi dogo tu la waislam na si sawa wala haki kuwalaumu waislamu wote hata itakapobainika ni waislamu wenye msimamo mkali ndio wamehusika. Watanzania wenzangu tukumbuke kwamba kabla ya kuwa waislamu, kabla ya kuwa wakristu, tulikuwa wapare, wamakua, wahaya, wasukuma nk. Dini zimekuja juzi tu na si sawa zitutenganishe na kutugombanisha. Sasa kuliko kipindi chochote tunahitaji umoja kama watanzania, tusianze kunyoosheana vidole kwa misingi ya dini, tuelewe kuwa hili ni kundi dogo la watu wasiowakilisha watu wote wa dini hiyo. Mwisho ni jukumu la serekali kutuhakikishia usalama wetu kama Watanzania. Ni wazi kuwa vyombo vyetu vya usalama havina uwezo wa kuchunguza na kupata ukweli kuhusu shambulio hili, tunataka vyombo vya nje vyenye uweledi katika uchunguzi wa matukio ya kigaidi kama haya vihusishwe tujue ukweli kuhusu tukio hili. Namaliza na rai yangu, NOW MORE THAN EVER WE NEED TO STAND TOGETHER AS TANZANIANS!
BAADA YA KUJA UISLAM NA UKRISTO -- SIKU HIZI HAKUNA : wapare, wamakua, wahaya, wasukuma nk. - - - NA VIPI UKIJA KUSIKIA KWAMBA CHANZO CHA MLIPUKO NI HITILAFU TU YA UMEME? ..... #MDINI - Ni yule anayeanza kuuzungumzia.... shame on You
 
Sijui Taifa linaelekea wapi na Watanzania tumeamua kupoteza ile hali ya Amani na Utulivu.
Why ni Makanisani tu hasa Kanisa Katoliki??

Kwa7bu ndilo lenye sauti kuliko watanzania wangine maana linalo sema linasikika, sawasawa na watoto wa baba mmoja ila anaepea kipao mbele ni mmoja tu....
 
Kama hivyo ndivyo maisha yetu yako hatarini. wote wanaotakiwa kutulinda muda wote wanahangaika na mambo ya vyama tu.
 
inna lilah wa inna illah rajiun. kama ni njama za m2 au kikundi na walaaniwe hakika makazi yao yawe jahnaum
 
Lema anangea kwa busara...
Anasema ni siasa zilizosababishwa na udini...Anasema polisi watumie jitihada kubwa kumtafuta mualifu kama walivyotumia kumkamata..
 
Mmoja wa ndugu kanijuza hii habari ila si kwa mapana zaidi.
Ila poleni sana watanzania wote walioguswa na tukio hili.
 
ayaah lema alitia togwa nchi kwa mara ya pili mtume siasa tupu kaharibu anadai wanasiasa mama yangu kainanika ccm kazuiwa he wamekata
 
Speech ya LEMA vs Mkuu wa mkoa

==hakuna jambazi anaweza akaja kutupa bomu kanisani
==polisi watafanya bidiii sana kumtafuta mhusika kwa nguvu ka walivyomkamata usikuuuu ule

hhaaaaaaa, wamemkatia maongezi
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom