Mlipuko mkubwa watokea kwenye Kanisa Katoliki Arusha, watu kadhaa wajeruhiwa

Status
Not open for further replies.
Mlipuko mkubwa umetokea maeneo ya Olasiti kanisa la Roman Catholic -Arusha, watu wa wengi wamejeruhiwa,chanzo cha mlipuko bado hakijulikana,habari zaid zinafuatia
Chanzo cha Habari Redio Maria
 
habari haijakamilika haieleweki wapi saa ngapi nini ilikuwaje kwa nini

Habari hii ni ya kweli tatizo lako wewe unaamini hisia zako zaidi,nimeshapokea simu kwa marafiki zangu kutoka Arusha kuhusu hilo tukio ns ni la kweli.
 
Tafadhali picha mliopo
pia Mods unganisheni thread hizi mbili
Tufuatilie kwa urahisi.


Nchi hii inakwenda wapi jamani
ndiyo hatuna amani tena hivi
tutafika 2015 kwa hali kama hii ilivyomnaya
sana.


Tuseme Ndovu nao issue yao Bungeni
inafutwa na Mlipuko wa Bomu Kanisani

Lema aliona mbali sana aliposema udini
pale Bungeni.

Ukishaona picha ndio utafanya nini?
 
Tuwe makini tusinyosheane vidole,jazba haitakiwi ukweli unatakiwa,tunahitaji habari kamilkamili,mungu ibariki Tanzania.
 
sasa ninaanza kuamini kuwa nchi inashidwa kutawalika kweli ni nchi gani kila mtu ni msemaji wa serikali? na RAISI yupo anashindwa kutoa msimamo wa serikali? sina uhakika kama kura yangu inakwenda tena mlengo wa kulia sasa ni kabla ya kipiga kura fikiri sana kwenye chumba cha kupigia kura na tafakari na chukua hatua ngumu. bila hatua ngumu hali hii itaendelea na Tembo wetu wataisha na sasa wataamua kuchingwa watu na kuchuna ngozi na kupeleka china.
 
sikilizeni radio maria, mi nasikiliza online hapa via itune app.....ni kanisa katoliki - olasiti arusha walikuwa katika misa.Padri anadai kuna mtu alikuja amevaa kanzu akarusha kitu na ndipo mlipuko ukatokea.
 
UGAIDI umeingia rasmi nchini ukilenga makundi fulani ya kijamii. It has now been proved beyond reasonable doubt.
 
Sijui Taifa linaelekea wapi na Watanzania tumeamua kupoteza ile hali ya Amani na Utulivu.
Why ni Makanisani tu hasa Kanisa Katoliki??

Naisikitikia sana nchi yangu Tanzania, kuna kila dalili ya kutofika 2015 kabla machafuko makubwa hayajatokea. Lakini ni vyema ikafahamika kwa viongozi wetu kuwa gharama ya machafuko ni kubwa kuliko maslahi ya kisiasa. Gharama ya machafuko ni kubwa kuliko gharama ya kuyaepuka kwa ku compromise na maslahi ya baadhi ya watu. Tunaomba viongozi wa nchi yetu nzuri Tanzania kamwe wasiyatabasamulie haya mambo, ni matukio yanayo hitaji seriousness ya hali ya juu, kwa kuchukua maamuzi thabiti na stahiki kwa wahusika wote. Serikali kamwe haiwezi kufurahisha makundi ya watu tofauti kwa wakati mmoja, serikali inatakiwa ilinde maslahi ya Taifa kwa ujumla ili kuondoa huo mkanganyiko wa kimaslahi, lakini kama mtu anataka kufanya mambo ili luepuka kuonekana mbaya kwa makundi kinzani, huku akiweka rehani mustakabali wa taifa kwa ujumla ni jambo lilisilokuwa sahihi hata kidogo. Niko Rwanda hapa, kuna watanzania wenzangu wako hapa wamepata hii taarifa na wamenipigia simu kuonesha masikitiko yao na hofu yao ya ni wapi Tanzania inaelekea. MUNGU IEPUSHE TANZANIA NA JANGA HILI INALOKABILIANA NALO!
 
Ni kweli mlipuko mkubwa umetokea kanisa catholic, muda huu naona magari ya uokozi pamoja na magari field force yanapita kuelekea olasiti eneo lilipo parokia ya urafiki
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom