Mlipuko Arusha na nadharia Pasua Kichwa!

2. NADHARIA KWAMBA WAHUSIKA NI CHADEMA WENYEWE.

Wanaokuja na fikra hii wanadhani kwamba CHADEMA wameamua kujifanyia Ugaidi wenyewe Ili waisingizie CCM, na CCM waonekane kwamba ni magaidi na na hivyo ni watu wasiofaa.

Vielelezo vya hoja hii (kutokana na maelezo ya wale wanaoitoa) ni kuwa;

(a) Kuna mifano mingi duniani ya Serikali au vyama kujihujumu vyenyewe na kuwasingizia wenzake ili waonekane wabaya.

(b)Ni mkakati wa kumaliza mjadala juu ya ishu ya Lwakatare.

KWA HOJA HIZI KUNA UDHAFU UFUATAO (JAPO HAUZIFANYI KUWA ZA UONGO 100%)

(A) Udhaifu wa kwanza ni kwamba; CHADEMA wasingekuwa na sababu ya kufanyia hivyo Arusha ambako wao ndio wamepashikilia.

(B)Kwa kujihusisha wao na tukio kama hilo isingekuwa rahisi wakati huu ambao wanakazana kujisafisha kutokana na kashfa ya Rwakatare.

(c)Kwa CHADEMA si jambo rahisi kupata mabomu na kuyatunza hadi kufikia kuyatumia bila kukamatwa

(d)Kwa mazingira yale; Milipuko ingeweza kwenda na Mwenyekiti wa chama na viongozi wengine waandamizi. Hivyo ni jambo lisiloingia akilini kusema viongozi wa chama walipanga kujitoa muhanga.
 
how i wish through serial numbers za vitu kama silaa za hatari kama hizi zingekuwa zinaambatana na taarifa za mnunuzi ambazo zingeambatanishwa kwenye records za serial number yenyewe.. sijui wataalam labda mtuambie more abt this as its not a local made
 
Mkuu sisi hapa tunajadili tu general logic lakini details za ndani kabisa hatuwezi kuzijua kwa kuwa hatuko kwenye field moja kwa moja na hatuna vifaa. Kupatikana kwa taarifa za ndani kabisa kama unavyosema, hilo ni suala la vyombo rasmi vya usalama kwa kuwa wako field, wana vifaa na ujuzi. Suala tu linakuja kama nao hawataingiliwa na wanasiasa.Tumuombeni mungu huku tukifuatilia.
 
kwa mtazamo usiokwepeka huachi kumfikiria mwigulu na kofia yake kama ndiye mnunuzi wa hizo bidhaa.. nikiitazama hiyo kofia naona kama ni bonus baada ya kununua bidhaa mfano wa mnunuzi wa sim anapopewa na pochi ama cover kama bonus.. zaidi mtu waweza pata wazo kuwa ni mwaka huu huu ambao mwigulu ametoka china tena very recently kiasi ambacho wasambazaji na wauzaji wa bidhaa hizo hapa kwetu wasingeweza kuzipata na kuziingiza nchini this soon. Zingetoka uingereza ama ujerumani haraka ningeanza kufikiria na uwezekano wa nadharia ya kuihusisha CHADEMA otherwise not tht simple
 
Mkuu sisi hapa tunajadili tu general logic lakini details za ndani kabisa hatuwezi kuzijua kwa kuwa hatuko kwenye field moja kwa moja na hatuna vifaa. Kupatikana kwa taarifa za ndani kabisa kama unavyosema, hilo ni suala la vyombo rasmi vya usalama kwa kuwa wako field, wana vifaa na ujuzi. Suala tu linakuja kama nao hawataingiliwa na wanasiasa.Tumuombeni mungu huku tukifuatilia.
ni sawa mkuu nalielewa hilo but as long as serial number zimeweza kupatikana, kwa mtizamo wa kawaida ni kuwa mnunuzi pia aweza kupatikana kutokana na kuwa si bidhaa inayoweza kuuzwa kiholela sembuse gari tu waweza jua mmiliki through registration number so kwa kuwa wachunguzi wamefikia kusema wamezifahamu serial number then tutegemee mshangao wa wao kusema hawawezi kumjua mnunuzi?
 
3;NADHARIA YA KWAMBA NI HUJUMA KUTOKA MAKUNDI YA KISIASA NJE YA NCHI;

Hii kimsingi ni nadharia isiyofaa kupuuzwa hata kidogo.Tukumbuke kwamba ni mwezi mmoja na nusu tu umepita toka Waasi wa M-23 watutishie baada ya serikali yetu kuidhinisha kupeleka majeshi ya kulinda amani Congo DRC.

Inawezekana kwamba kinachotokea hapa kuna makundi kutoka nje yanataka kutuharibia "concetration" ya kuangalia mambo mengine ya kimataifa, na kinyume chake turudi kuzozana wenyewe kwa wenyewe.Pia ikumbukwe kuwa Obama anatarajiwa kuja nchini siku za karibu.Inawezekana ni hila za watu wa nje kutuvuruga (pengine wivu) ili Obama aogope asije tena.Lakini Pia Rais kikwete juzi juzi kashauri kutatua mgogoro wa Congo kwa Mazungumzo. Nadhani mmeona "Reaction " iliyokuja .Kwa hiyo hapa napo panahitaji uchunguzi wa kina.

Hata hivyo kwa mtu wa kawaida kwenye eneo hili ni vigumu kujua chochote kwa kuwa kunahitaji uchunguzi wa kina kwanza.Hapa tu ni kuachia vyombo vya usalama na kujiaminisha kwamba vitafanya kazi yake ipasavyo.
 
deduction nzuri sana kaka..nimekugongea LIKE!!

mwigulu nchemba ana roho ya ajabu sana...roho nhumu sanaa.....

ni kweli hapa kutokana na hypothesis yako research question kadhaa zinajitokeza na pengine majibu ni kama ifuatavyo....

RQ1. je kinana na kundi lake walekwenda kuwatisha wachina kuwa chadema wakichukua nchi interest zao zitapotelea magharibi? kwamba interest zao kama za gesi bandari na nyinginezo zitakuwepo tu ikiwa CCM watakuwa madarakani!

RQ2. je ni kwamba China inapaswa kuisaidia ccm ili mambo yaende shwari....

RQ3. je kwamba ujumbe wa kofia ya mwigulu ni kwamba CCM ni tawi la chama cha kikomunisti cha china?

THE FACT KWAMBA BOMU LILIOPIGWA, BUNDUKI NA SILAHA ZA MOTO VILITOKEA KWENYE KIWANDA CHA SEREKALI YA CHINA TENA TOLE AMBALO HATA MAJESHI YETU BADO HAYAJAWA NAYO NALIFANYA TUKIO SIO HILI TU, HATA LILE LA OLASITI KUWA NI MTANDAO NDANI YA CCM UNAORATIBIWA NA MWIGULU NCHEMBA ......

PROBLEM YA NCHEMBA NI KUWA IQ YAKE NI NDOGO SANA...MAANA HATA KAMA NI MUONGO BASI NI BORA UCHEKI KONSISTENCY YA MATENDO YAKO NA MANENO YAKO.....

KWANGU MIMI SASA TUKIO LA OLASITI KANISANI LILIKUWA NI TUKIO LA KUWAANDA WATU WA ARUSHA KUOGOPA MIKUTANO NA KUJUA ADHA YA MABOMU...ILI WALIVYOKUJA KUPIGA HILI LA JUZI WATU WAWE WAOGA KABISA.....POOR NCHEMBA
 
3;NADHARIA YA KWAMBA NI HUJUMA KUTOKA MAKUNDI YA KISIASA NJE YA NCHI;

Hii kimsingi ni nadharia isiyofaa kupuuzwa hata kidogo.Tukumbuke kwamba ni mwezi mmoja na nusu tu umepita toka Waasi wa M-23 watutishie baada ya serikali yetu kuidhinisha kupeleka majeshi ya kulinda amani Congo DRC.

Inawezekana kwamba kinachotokea hapa kuna makundi kutoka nje yanataka kutuharibia "concetration" ya kuangalia mambo mengine ya kimataifa, na kinyume chake turudi kuzozana wenyewe kwa wenyewe.Pia ikumbukwe kuwa Obama anatarajiwa kuja nchini siku za karibu.Inawezekana ni hila za watu wa nje kutuvuruga (pengine wivu) ili Obama aogope asije tena.Lakini Pia Rais kikwete juzi juzi kashauri kutatua mgogoro wa Congo kwa Mazungumzo. Nadhani mmeona "Reaction " iliyokuja .Kwa hiyo hapa napo panahitaji uchunguzi wa kina.

Hata hivyo kwa mtu wa kawaida kwenye eneo hili ni vigumu kujua chochote kwa kuwa kunahitaji uchunguzi wa kina kwanza.Hapa tu ni kuachia vyombo vya usalama na kujiaminisha kwamba vitafanya kazi yake ipasavyo.
mkuu kwa nadharia ya nmna hiyo sidhani kama wangei target upinzani, nadhani wangewalenga ccm kama serikali
 
Mkuu sisi hapa tunajadili tu general logic lakini details za ndani kabisa hatuwezi kuzijua kwa kuwa hatuko kwenye field moja kwa moja na hatuna vifaa. Kupatikana kwa taarifa za ndani kabisa kama unavyosema, hilo ni suala la vyombo rasmi vya usalama kwa kuwa wako field, wana vifaa na ujuzi. Suala tu linakuja kama nao hawataingiliwa na wanasiasa.Tumuombeni mungu huku tukifuatilia.

Usitufanye mbumbumbu hakuna cha logic hapa mwenyewe umeshaiondoa Chadema kenye hoja yako ya pili unaaka tujadili nini. Endelea na story yako wewe unajua zaidi
 
3;nadharia ya kwamba ni hujuma kutoka makundi ya kisiasa nje ya nchi;

hii kimsingi ni nadharia isiyofaa kupuuzwa hata kidogo.tukumbuke kwamba ni mwezi mmoja na nusu tu umepita toka waasi wa m-23 watutishie baada ya serikali yetu kuidhinisha kupeleka majeshi ya kulinda amani congo drc.

Inawezekana kwamba kinachotokea hapa kuna makundi kutoka nje yanataka kutuharibia "concetration" ya kuangalia mambo mengine ya kimataifa, na kinyume chake turudi kuzozana wenyewe kwa wenyewe.pia ikumbukwe kuwa obama anatarajiwa kuja nchini siku za karibu.inawezekana ni hila za watu wa nje kutuvuruga (pengine wivu) ili obama aogope asije tena.lakini pia rais kikwete juzi juzi kashauri kutatua mgogoro wa congo kwa mazungumzo. Nadhani mmeona "reaction " iliyokuja .kwa hiyo hapa napo panahitaji uchunguzi wa kina.

Hata hivyo kwa mtu wa kawaida kwenye eneo hili ni vigumu kujua chochote kwa kuwa kunahitaji uchunguzi wa kina kwanza.hapa tu ni kuachia vyombo vya usalama na kujiaminisha kwamba vitafanya kazi yake ipasavyo.

haraka haraka nilitaka kumsingizia masikini wa watu paul kagame...... Sio yeye...ni humu humu ndani....kwa hili i reject the alternative hypothesis and i agree with null h0: - - - bomu hili sio hujuma kutoka nje ya nchi!
 
Yaani wewe unauliza na kujijibu mwenyewe! Kwa nini unataka ku-manage mawazo ya watu? Hiyo nadharia ya CCM umeipamba wakati ya CHADEMA yenye ushahidi mwingi umeifinya na kukanusha hapo hapo!

Ndio maana nchi hii ni masikini kwa sababu wajinga wanadhani wana akili!
 
Hivi vielelezo vyako vimenistua sana mkuu.

Tuna rekodi za Mawaziri kama Karamagi kuwa walikuwa wajasiriamali na kuamua kuingia katika siasa ili kulinda maslahi yao na kupata opportunities mpya za biashara, baada ya kuona mambo yametibuka kwa nia njema tu wakaamua kujiuzuru na kukubali matokeo.

Sasa swali langu, huyu Mwigulu anataka nini hasa!!????

Inawezekanaje milolongo ya matukio yote haya ya kikatili namna hii yatokee kwa kiwango hiki na asisikie hata uchungu! (Japo swali la pili ni juu ya mtandao anaoshirikiana nao maana siamini wanaccm kama Mzee Salim, Butiku, Diallo, Malecela au vijana kama Ngeleja au Masha wanakubaliana na ukatili huu!
)
 
4.NADHARIA YA MWISHO INAYOWEZEKANA NI KWAMBA INAWEZEKANA NI WATU WENYE UFUNGAMANO NA AL-QAEDA.

Ifahamike kwamba hawa jamaa wa AL-Qaeda kwa ujumla wake hawaungi mkono Democrasia wala Mataifa yanayoamini juu ya mfumo wa Kisecular. Kwa hiyo kwao wao; yeyote anayepigania democrasia ya vyama vingi, anaseyeunga mkono mataifa na mfumo wa kisecular, kwa ujumla wake wanamtafsiri kama adui na wakimpatia target wanaweza kumdhuru. Hawa jamaa wao wana mambo mengi ambapo wakati fulani hata ni vigumu kuelewa vizuri kwamba ni nini wanachotaka.

Kwa sasa hawa jamaa wanaweza kuingia nchini na hata kuingiza silaha kinyemela Kutoka mogadishu (Waliko Al-shabaab) ambapo pia kuna wasiwasi kwamba wakati fulani kuna muingiliano wa watu wa somalia, Kenya na Tanzania kupitia mpaka wa Namanga.

Kwa hiyo nadharia hii nayo inaweza kutupa muongozo wa kuelekea.

N.B;
kATIKA NADHARIA ZOTE; Inawezekana alietupa bomu ni mtu tu wa mtaani ambaye ametumiwa na genge mojawapo.Hata hivyo si lazma tukio la sasa liwe na uhusiano wa moja kwa moja na la lile La Olasiti Arusha.
 
Yaani wewe unauliza na kujijibu mwenyewe! Kwa nini unataka ku-manage mawazo ya watu? Hiyo nadharia ya CCM umeipamba wakati ya CHADEMA yenye ushahidi mwingi umeifinya na kukanusha hapo hapo!

Ndio maana nchi hii ni masikini kwa sababu wajinga wanadhani wana akili!
Mkuu; na wewe ungesaidia kuongezea kwenye nadharia moja wapo hapo; kwa namna yeyote ile (hata kama ni dialogue) ungeweza kusaidia mawazo pengine..
 
ccm ndio wausika......na wamesaidiwa na polis hilo halipingiki....mwigulu ni hatari sana wana JF
 
Mtoa mada ameonesha udhaifu mkubwa sana ktk kudadabua hoja yake. 1. Anasema mlipuko Arusha ni nadharia pasua kichwa. Ninavyofahamu mimi kitu kinakuwa pasua kichwa kama kinakosa majibu au majibu yanatatanisha. Kwa maelezo yake utata uko wapi? wakati anaonesha dhahiri kuwa ccm wanahusika (kwa ushahidi wa mazingira). 2. Mtoa mada anaonekana ushabiki wa kisiasa unamtawala kuliko ukweli (reality). Mfano, kachambua vizuri mazingira yanayoweza kudhaniwa ccm na cdm wanahusika, lakini cha ajabu ametoa udhafu wa kuihusisha cdm TU na mlipuko kana kwamba hoja za kuihusisha ccm hazina udhaifu. Hapa ndipo umakini na ueledi wa mtoa hoja unapokuwa mashakani.
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom