Mliowahi kupitia hali kama hii ninayopitia hapa India njooni mnishauri

ufumawicha

JF-Expert Member
Mar 16, 2014
504
209
Mimi ni mtanzania, ninayesomea hapa India kwa ufadhili wa ICCR!
SIFICHI huu ufadhili ni mzuri. Tatizo chuo nilichopo hapa na hasa idra niliyopo haina walimu kabisa kiasi kwamba wanafunzi waliomaliza masters wamepewa mikataba ya muda ili watufundishe!

Walimu wanakosea mno kiasi kwamba tumeshaathiriwa na sisi hasa kwenye mitihani!!!Ukikata rufaa na kueleza kuwa ulichojibu ndicho ulichofundishwa unaambiwa, hata kama ni hivyo kwa nini na wewe ukubali kuandika uongo?? Ubaguzi haukuwepo ila umeanza! Kama una shida na mwalimu hata kama umetangulia akija mwanafunzi wa Kihindi inabidi asikilizwe yeye halafu ufuate wewe!!

Wadau mliopitia hali hizi njooni mnipe ushauri maana ninafikiria kusitisha ufadhili nirudi Tz!!!
 
Mkuu energy inaflow sehemu ambayo attention yako ipo kwa ushauri wangu soma achana Na ayo mambo mengine

Umepata ufadhili Basi hakikisha unaitumia iyo nafasi ipasavyo

Uwe Na masomo mema kiongozi
 
Mkuu energy inaflow sehemu ambayo attention yako ipo kwa ushauri wangu soma achana Na ayo mambo mengine

Umepata ufadhili Basi hakikisha unaitumia iyo nafasi ipasavyo

Uwe Na masomo mema kiongozi
Tatizo walimu wanatufundisha uongo na inapokuja mitihani matokeo si mazuri.Mara nyingi wamekuwa wakiomba msamaha kuwa walikosea!Tatizo kwa kuwa hawana sifa hawaruhusiwi kutunga mtihani wala kusahihisha!Mitihani tunatungiwa na profesa wa chuo jirani!Kumbuka mimi ninasomea masters na hao jamaa wa part time nao elimu yao ni masters!
 
Hata mimi+(sisi) tulifubdishwa na tutorial mzee makalayi ni kufikia so komaa tu hakuna namna!
 
Mkuu jiongeze, ushajua kwamba wanafundisha uongo sasa wewe jibiidishe kuupata ukweli. Yaani wanachofundisha kichukue kwa ajili ya mitihani yao lakin inapofika mitihani ya huyo professor basi andika ukweli.. japo ni ngumu ila komaa.. vumbi la bongo sio zuri, pambana urudi na hiyo masters tena una bahat una hadi ufadhili
 
Mimi ni mtanzania, ninayesomea hapa India kwa ufadhili wa ICCR!
SIFICHI huu ufadhili ni mzuri. Tatizo chuo nilichopo hapa na hasa idra niliyopo haina walimu kabisa kiasi kwamba wanafunzi waliomaliza masters wamepewa mikataba ya muda ili watufundishe!

Walimu wanakosea mno kiasi kwamba tumeshaathiriwa na sisi hasa kwenye mitihani!!!Ukikata rufaa na kueleza kuwa ulichojibu ndicho ulichofundishwa unaambiwa, hata kama ni hivyo kwa nini na wewe ukubali kuandika uongo?? Ubaguzi haukuwepo ila umeanza! Kama una shida na mwalimu hata kama umetangulia akija mwanafunzi wa Kihindi inabidi asikilizwe yeye halafu ufuate wewe!!

Wadau mliopitia hali hizi njooni mnipe ushauri maana ninafikiria kusitisha ufadhili nirudi Tz!!!
Hujasema unasoma level gani-Diploma, Bachelor au Masters? Mtu aliemaliza masters anaweza kufundisha hata masters level kutegemea na chuo. Kuna Chuo kule UK hiyo ilikuwa kawaida tu. Kwa Tanzania kuna vyuo vingi vinaruhusu lakini kusimamia research ya Masters vyuo vingi haviruhusu. Hivyo hiyo isiwe shida labda kama hata research wanasimamia.

Kuhusu kuandika uwongo kwenye mitihani, naona unatatizo la kutegemea kile unachopata darasani tu. Siku hizi kuna library, bookshop na internet ni rahisi kujiongeza na kugundua cha mwalimu kinapishana wapi na hizi sources nyingine. Na hili ukiona mpishano ni mkubwa unadiscuss na ticha. Hivyo ni juu yako kujiongeza.

La ubaguzi sina ushauri kwani inategemea policy za chuo zikoje-unaweza ukamezea kama una wasiwasi wa kushughulikiwa au ukapiga kelele bora uwe na ushahidi na uwe tayari kwa lolote lile.
 
Mkuu energy inaflow sehemu ambayo attention yako ipo kwa ushauri wangu soma achana Na ayo mambo mengine

Umepata ufadhili Basi hakikisha unaitumia iyo nafasi ipasavyo

Uwe Na masomo mema kiongozi
Huna haja ya kusema wewe ni msomi,andiko lako linajidhihirisha hongera mnoo mkuu#jf yenye nguvu
 
Mkuu upo chuo gani? au mji upi? maana mie nimesoma Bangalore huko tulikuwa na changamoto kama hiyo ila usipokuwa mwelewa ndo utajuta. Mfano kila somo huwa kuna kitabu chake na mwaka wake ( Topic zote, maswali na majibu ) na huwa hawatungi nje ya hicho kitabu. kama humwelewi lecturer si usome hicho kitabu ambacho chuo kinakuwa kimepitisha juu ya hilo somo au course.
 
Back
Top Bottom