Mliowahi kupigana darasani leteni ushuhuda wenu hapa

kipindi nipo darasa la sita... kwenye kukaa tulikua tunapangwa ile wavulana wawili msichana katikati au wasichana na mvulana ili kuepusha kelele. Bhas bwana siku ya ijumaa kama kawaida vipind vichache na unakuta kila mtu karudi kukaa na shosti yake. .
nilipokua nakaa mimi wasichana walikua wawili na mvulana mmoja, sasa tulishajikusanya kupiga umbea mashosti ka ilivyo ada.. Eeee ghafla bin vuu jamaa katoka alipotoka kaja kukaa sasa dawati linabeba watatu yeye wanne kaja jiongeza Aaa tukaona mazinguz tukawa tunamsukuma,sasa si akaanguka na mimi ndio nilikua pembeni yake so alipoibuka na hasira akanivaa mimi tukanza ugomvi jamaa alinibutua mateke ya tumbo..
dah nikainama kusikilizia maumivu uku darasa zima linamwambia umeuaa!! umeuaaa!! aseh kuskia vile nilishikwa na hasira nilimuibukia jamaa na mangumi aliyoshindwa zuia adi tulipokuja amuliwa alishageuka nyanya maana alikua mweupe kukaa kidogo kengele nayo iyoo mda wa usafi...
haha iyo siku ndiyo ilikua mara yangu ya kwanza kupigana skuli
 
Balaa aisee.. tulikua tunacheza mchezo wa kupiga visoda darasani.. nlikua najifanya mjanja mjanja nkaficha visoda vingine.. alikuja dogo mmoja hivi mgupi alinipiga ngumi moja nzito.. nakumbuka nili shout “ kanipiga na jiweeee” ile kugeuka hivi tuanze kuzichapa nakuta dogo keshakimbia zamaniii...
 
Aisee darasa la 7 nakumbuka nilipigana na mwalimu, alikuwa kijana kijana halafu anapenda sifa sasa siku hiyo kaingia kakuta watu wanapiga kelele, mimi naye ndio naingia ndani nilikuwa nimepitiliza mapumziko maana kipindi hicho walimu hawafundishi tena, tunasubiria mtihani wa taifa.

Sasa mwalimu akaniwakia na kutaka kunichapa eti mimi ndio kilaza kabisa hata kufuata kengele siwezi, ile karusha fimbo anichape mkononi nikaidaka sijui ni ujinga gani ukaniingia nikaona huyu jamaa mbona namuweza nikaanza purukushani naye darasani nikamzidi nguvu sijui aliona aibu nikamgaragaza chini nikakimbia.

Ilikuwa katikati ya wiki sasa kurudi shule kesho yake aisee walimu walinikomesha nilipelekwa ofisini kuna wamama hao walinishikilia mikono wengine walikuwa wanachapa bakora nafikiri nilipigwa kwa muda zaidi ya saa 2 na walimu wa shule nzima, yaani wengine walikuwa wanachapa wanaenda kunywa chai wakirudi wanasema hili bado lipo wanachapa, nililia nikaachwa nikae kabisa katikati ya ofisi anayekuja anacharaza viboko anaondoka, nilikoma aisee
ni hatareeh sana.
 
Umenikumbusha kuna masela walikamatwa wanapigana na ticha darasani, akawaita mbele pale pale darasani wazipige nakozi kavu kavu halafu yeye ndio kama refa, ilikuwa kama dakika 5 msela alizidiwa akaanza kulia maana zilikuwa zinapigwa unasikia sauti kama muvi za wachina kila mtu yupo kimya hamna kupiga kelele unajua kabisa hiyo imengia vilivyo usoni, ticha akamwambia mshindi aende akakae halafu yule aliyepigwa akamcharaza viboko
 
Shule zetu za vidumu na mfagio mambo haya ya ngumi yalikuwa Kawaida sana kutokea.

Nimeshuhudia mechi nyingi sana za ngumi,mechi inaandaliwa mapema,njiani wakati wa kurudi ndio muda wenyewe.

Mimi nilikuwa si mtu wa vurugu japo nishawahi piga mtu katika harakati za kujinasua,,alinivamia anipige kwa chuki zake tu..
Nikamtandika.
ilikuaje.
 
Kuna dogo mmoja alikuwa anaitwa Hery barton mjuaji sana nakumbuka alizichapa na mchizi mmoja anaitwa Daniel Msuya! Sikuhio mapema sana kabla ya assembly saa 12 asubuhi.

Aisee zile ngumi zilikuwa level za kimataifa yani! Hamna kushikana hapo ni nako 2 nako yani ikipenya unaskia shavu limeitika fyo.toooh. Pale ndio tulipata taste ya kina Tyson kabisa huku hery barton akila nakoz za kwenda maana Daniel alikua na utulivu sana kwenye kuzipachika.
 
Mda huu tulikuwa tunauita “after bell rings” yani baada ya kengele ya mwisho ya kutoka shule wahuni wanajimwaga golf club kufundishana heshima na adabu!

Nakumbuka kuna mtoto mmoja wa kihindi anaitwa Huzeifa bonge hivi alijimix kwa mtoto wa kiluguru Ramadhani hussen amevimbia chini kama twaha kiduku! Asee alichofanywa yule ponjoro ilikuwa ni bad news aliondoka kaoteshwa vinundu kaiva kama jezi ya simba
 
Eti jezi ya Simba

Kuna muda mwalimu alikamata washangiliaji wote wa ngumi..
Kumbe alichelewa kutoka aiseeee...tuliruka kichura siyo Cha nchi hii..halafu mwalimu Mwenyewe ni bimkubwa .

Nilirudi nyumbani Sina hali,akasema kesho urudie tena kubaki kushabikia ngumi.
bi mkubwa alikunyoosha vilivyo.
 
Kuna jamaa nilikuwa namuonea sana ndio alikuwa fala wangu.

Siku hiyo akaamua kunitest hahahaha.
Maana nilikuwa maneno mengi mikwara kibao huku mweupe kabisa!!

Jamaa aliniotea roba moja halafu madenti wengine wakawa wanashangilia kwamba asiniachie hadi nikojoe!

Kiukweli siku hiyo nilimuona ziraili kbs..
Ilibidi nikojoe tuu maana sio kabali ile.
Hata angetaka ninye ningekunya!!

Hapo heshima ikawepo..
Akaletwa chalii mwingine tena alikuwa na kaumbo kadogo halafu mi bonge la mtu.

Nikaanza bullying kama kawaida.
Yule dogo akatonywa na wambea kwamba mi mweupe mikwara tuu..

Dogo akaniamulia siku hiyo akanishika mapumbuu acha maneno kabisaaa!!
Yaani kumpiga nilishindwa nikabaki nimetulia tuu.mkono mmoja kanibana mapumbuu mwingine ananipiga ngumi na makofi!!
Kalikuwa kafupi yaani kunipiga kofi hadi karuke juu km masai ndo kanipate.hahahaha
Jaman nacheka km chizi khaaah.
 
Usiombe upigane na kijana muoga! Siku zote huwa shabiki ila ikafika siku namie nikapambanishwa na mnyonge wangu kijana wa mwenye mabasi ya BM Coach yale dogo anaitwa Blasius Makundi!

Hii ilinitokea mzee nilikula gumi la pua nikaanza kuvuja damu nikaamua nitoke dima tu nilikuwaga namjambisha tu mikwara mingi ila ngumi sijui aisee nilisepa kesho ikawa gumzo wahuni wote class walinivua vyeo maana nilikuwa cheerleader!
 
Nakumbuka kuna chalii mmoja alikuwa mbabe sana kwangu siku hiyo ujasiri ukanijaa amenila hela kwenye kamali ya kichwa mwenge halafu ananicheka c'se ananiweza

Nilisimama kama dk 5 natafakari hela nimeiba home halafu mtu ananila anacheka nikirudi home naenda kuchezea nikasema isiwe kesi nikampa roba ya nikijikologa nimekunya hadi nikasikia anaanza kukoroma nikatuma mkono mfukon nikazoa salary zote nikatimua mbio home wiki bila kwenda shule nazuga naumwa

Kuja kwenda nikabeba maziwa mgando kwenda kumpoza na dharau zikaisha
 
Hahahahah kipigo cha mbwa kachoka
Dah Mkuu maisha ya shule kw zamani kam unakua mlaini lain unaacha shule maan nlipew bakor nying Sana na adhabu y kuchimba mashimo 90 wakt shule yenyew eneo eka 3 tu hazifiki kwa hasir nlichimb mashimo ad jumapili nkaacha shule nzima mashimo ya kutosh ad assemble nkapigwa ten adhab ya kufukia Dadek
 
Aseh nilipigana na demu ana mapepo anaitwa ashura primary kudaadeki nakumbuka utani wa kawaida tu akaanza kuntukana hapo darasa limejaa hatari. Alikuwa kasimama mbele ya darasa na njia ilikuwepo ila kuonesha umwamba wangu nkapanda juu ya madawati kumfata alipo tukaanza kupigana. Daadeki kilichonipata Najua mwenyewe wana ndo walikuja kuniokoa. Dem alinichakaza huku mapepo yako juu nilipigwa ile siku sisahau
 
Aseh nilipigana na demu ana mapepo anaitwa ashura primary kudaadeki nakumbuka utani wa kawaida tu akaanza kuntukana hapo darasa limejaa hatari. Alikuwa kasimama mbele ya darasa na njia ilikuwepo ila kuonesha umwamba wangu nkapanda juu ya madawati kumfata alipo tukaanza kupigana. Daadeki kilichonipata Najua mwenyewe wana ndo walikuja kuniokoa. Dem alinichakaza huku mapepo yako juu nilipigwa ile siku sisahau
Hio inaitwa mwana ukome
 
Nakumbuka Ilikua Ijumaa mida ya kutoka mapema Waislam wanaenda masjid, Darasa letu E ndo lilikua na watu vilaza na ndio wa mwisho kuhusiwa.

Kuna katoto Cha kiarabu nikakaandikia ujumbe wa kukapiga sound wakati Nampa kumbe jamaa wengine nje wananichora nao walikua wanafukuzia, bwana wee muda wa kutoka jamaa wakanibana Kona.

Zilipigwa ngumi mpaka nikawa naona Malaika wanapepea angani, ngumi moja ilitua puani mpaka PUTO la Kamasi likatokea..nikaona Cha kufia nn nikapata upenyo nikaokota mawe.

Nilirusha moja nikatoa mtu tochi ya maana wengine wakasepa, nikajipigia zangu saaafi...J3 kaleta mzazi nikala Viboko vya Haja.

Nyingine nilipigana na Dem nikampandisha sketi wadau wapate kuona Mema
 
Inakuwaje wanangu wa Jamiiforums

Binafsi mimi nilikuwa mpenzi mtazamaji, na Hakuna kitu kilikuwa kinaniuzi kama kuona watu wakizichapa atokee mtu aje kugombolezea

Kwa wale mliowahi kuzichapa class mutuelezee sababu ilikuwa ni ipi, je bifu liliendelea, kama ulichapwa vp kisasi kilitokea

Kwa wale wapenzi watazamaji wenzangu ulikuwa unaenjoy nini wana wakizichapa class?View attachment 1947737
Dah😂 umenikumbusha nipo darasa la 4 shule zetu izi za kidumu na mfagio huku kuna kupishana kukaa kwenye madawati...
Sasa mi nlikua nmekaa chini.. kuna bidada akapita akanikanyaga nkavumilia. Nlikua type hii ya wanafunzi wapole sana class na wanaofanya vizuri, bas bhana ... akaja kupita tena akanikanyaga mara ya pili, nkamshika nkamwambia umenikanyaga mara ya pili sasa ila hakujali.. ani alikua ni wale micharuko ya darasa...


Mara ya tatu alivopita akanikanyaga afu akasimamia apo apo weeeeh!! Kichaa changu cha kipemba kikaamka😂 nkamsukuma huku namwambia umenikanyaga nakuambia huniskii..

Akainuka tukashikana.. nlimshushia migumi ya mgongo mpaka wanadarasa wakafurahi, akaingia ticha watu kimya.. sa alivoona ticha na ile kuwa kaaibishwa maana alikua celebrity wa darasa akaanza kulia..

Ticha kuuliza kulikoni nkamuelezea, nkaambiwa nmekosea kwa hiyo nkachapwa fimbo 6 ila dada ndo aliaminika ndo mchokozi maana kwa hali ya kawaida mimi mpole siwezi kuchokoza mtu.



Tukio jingine hili ndo nliloapa stakuja kuzichapa tena mimi!

Ilikua kipindi nipo form 3.. enzi za ujana ujana na balehe.. as usual nlikua tu mpole na mkimya.. kuna mdada akaanza kunletea pigo za ki se nge .. yani ujinga ujinga tu.. anansema ovyo ovyo kwa watu... yan mpaka watu wanashangaa mi nawezaje kuwa na izo tabia afu nlikua prefect enzi izo..

Kumbe bhana boyfriend nliekuwa nae bi mdada alikua anamtaka na hana njia ya kumpata ... apo npo nae since form 1... akaona njia rahisi ni kunichafua asee nlikonda kwa kuvumilia kejeli za kijinga jinga...

Siku tumetoka skuli nkaona huu u se nge utaisha lini unaniathiri mkimya mimi.. nkasema hapana.. alikua na rafiki ake nkamdaka nkamwambia nna maswali nataka kukuuliza.. tuongee yaishe..


Kheeeh akawa ananijibu vibaya, alipokosea ni pale aliponitukana🤕 nlimchapa kofi la uso.. alivoona npo serious akataka tupigane nkajisemea kudadadeki nmevumilia sana ngoja tuheshimiane kidogo...

Mwenzie yupo mbele uko katangulia .. aliponitibua ni aliponkatia vifungo vya shati.. nlimpiga ngumi izo..(wakati nakua nmeishi na kaka zangu kwa hiyo michezo ya ngumi walinifundisha sana na karate na nlikua nafanya mazoezi sana ya mwili... ila msniogope mi mrembo tu 😂😂)
Bas nlikua natembea na vile vijiwembe vya surgery nlikitoa nlimchana chana.. mpaka tunakuja kuamuliwa nlikua nmemuumiza sana.. apo wadada walikua waogopa kunishka ilibidi wakaka ndo wanithibiti...
Baada ya kuona ule msala nkabadili njia nduki😂 hawakuniona .. bahati nzuri nlikua na sweta nkavaa nkaenda kupanda gar.. na skwenda shule wiki nzima..

Nlikuja tu kuambiwa mdada kachukua RB polisi na kesi ikaenda shule.. staff nzima haikuamini nlichofanya maana nlikua mpole mno wala sio muongeaji..

Kwa ustaarabu mkuu wa shule akamsihi ile kesi akafuta polisi ikamalizwa kishule.. nkapigwa suspension wiki 3.. na kazi za nje ya darasa wiki 1 nkavuliwa na uongozi na nliondoka na viboko vyangu 8 vya makalio!!!


Mpaka leo nmesema siji kupigana tena mimi hasa na mdada japokuwa juzi kati tu nmekoswa koswa na kupiga mtu😂😂😂
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom