Mliowahi kuomba kazi mashirika ya Umoja wa Mataifa (UN) mpitie hapa

Kingsmann

JF-Expert Member
Oct 4, 2018
3,061
2,000
Naombeni ushauri wa namna nzuri ya kuandika CV ya kuomba kazi kwenye hayo mashirika tajwa hapo juu hasa hasa UN.

Namna ya kuapply mara nyingi wanakuambia utume CV yako kwenye email. Sasa kimbembe ni kujua muundo wa hiyo CV unatakiwa uweje ili angalau kidogo wakupe attention.

Najua CV ya kutuma kwa hawa mabwana haiwi kama zile za kwetu ambazo mwishoni unaweka referee watatu. Hivyo kwa ambaye anajua naombeni msaada wa format yake ikiwezekana kama nitapata sample nitashukuru sana.

Cc: Nyani Ngabu Sky Eclat Zitto

Manners Maketh Man
 
Consultant

JF-Expert Member
Jun 15, 2008
10,416
2,000
CV isizidi page nne.

Pitia job description vizuri na some of the duties kwenye hiyo JD zicopy na uzidistribute kwenye maeneo mbalimbali uliyofanya kazi ndani ya CV yako.

Huna haja ya kuweka referees kwenye CV. Wakiwahitaji huko mbele ya safari watakuomba uwape

Kama wametaka cover letter, make sure ni one page only. Kwenye barua andika how skills na experience yako inakufanya wewe upewe kipaumbele. Unaweza kutoa mfano wa nini ilifanya huko nyuma kuthibitisha hilo.
 
Asante kiongozi.

Mfano kama wameomba CV tuu, then kwenye CV umeainisha skills zako kulingana na job descriptions zao, je kuna haja ya kuambatanisha na certificates za training mbalimbali ulizofanya?
Unforgetable

Manners Maketh Man
 
Manjagata

JF-Expert Member
Mar 7, 2012
7,524

Umeeleza vizuri consultant ila hapo kwenye ku-distribute hizo responsibilities awe mwangalifu maana kuna mashirika huwa yana kazi zake specific ambazo inawezekana hata hazijui, kwa hiyo achague zile tu anazifahamu.

Pia issue ya referees, kwenye online application yao huwa kuna window ya kuweka referees kwa hiyo hata kama atakuwa hajawaonesha kwenye CV kwenye application watamwomba.

Kwa mkuu mleta mada unaposema UN maanake hayo mashirika yote ukiyoyataja hapo juu yote hayo ni UN na yana mfumo mmoja wa kufanya application ya kazi!
 
Kingsmann

JF-Expert Member
Oct 4, 2018
3,061
2,000
Umeeleza vizuri consultant ila hapo kwenye ku-distribute hizo responsibilities awe mwangalifu maana kuna mashirika huwa yana kazi zake specific ambazo inawezekana hata hazijui, kwa hiyo achague zile tu anazifahamu. Pia issue ya referees, kwenye online application yao huwa kuna window ya kuweka referees kwa hiyo hata kama atakuwa hajawaonesha kwenye CV kwenye application watamwomba. Kwa mkuu mleta mada unaposema UN maanake hayo mashirika yote ukiyoyataja hapo juu yote hayo ni UN na yana mfumo mmoja wa kufanya application ya kazi!
Asante sana mkuu, mode of application ni kupitia email hivyo hiyo application window haitumiki.
Unforgetable

Manners Maketh Man
 
kawoli

JF-Expert Member
Feb 20, 2014
6,016
2,000
Kutumia email address?? Cross my fingers usije ukaingizwa mjini.
Anyway, nimewahi kufanya interview kadhaa kwenye UN agencies lkn mode of job application haikuwa kutuma emails.

Nachojua kazi una-apply kwa kujaza online links ambazo wanakuwekea kwenye kila tangazo la kazi. Mara nyingi attached document wanayoitaka ni cover letter. Maelezo mengine kuhusu elimu yako, skills, job experience, referies na blahblah nyingine kuna segment unazijaza kwenye hiyo online application form.

If you qualify for further steps they will ask for copies if academic certificates and other legal documents such as birth certificate or work permit kwa nchi husika depending na nature ya kazi yenyewe. Then wanna stages mbalimbali zisizopungua mbili mpk tatu.

Kama huja - qualify for further process huwa wanatunza kumbukumbu zako for future job alerts endapo zitamatch your skill. Bado sijafanikiwa kupata job kwenye hizi UN agencies ila I hope my day will come.
 
Redpanther

JF-Expert Member
Feb 23, 2019
1,648
2,000
Nimewahi kufanya interview kadhaa kwenye UN agencies lkn mode of job application haikuwa kutuma emails.

Nachojua kazi una-apply kwa kujaza online links ambazo wanakuwekea kwenye kila tangazo la kazi. Mara nyingi attached document wanayoitaka ni cover letter. Maelezo mengine kuhusu elimu, skills na job experience Kuna segment unazijaza kwenye hiyo online application form.

Then wanatunza kumbukumbu zako for future job alerts endapo zitamatch your skill. Bado sijafanikiwa kupata job kwenye hizi UN agencies ila I hope my day will come.

Amen

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kingsmann

JF-Expert Member
Oct 4, 2018
3,061
2,000
Kutumia email address?? Cross my fingers usije ukaingizwa mjini. Anyway, nimewahi kufanya interview kadhaa kwenye UN agencies lkn mode of job application haikuwa kutuma emails.

Nachojua kazi una-apply kwa kujaza online links ambazo wanakuwekea kwenye kila tangazo la kazi. Mara nyingi attached document wanayoitaka ni cover letter. Maelezo mengine kuhusu elimu yako, skills, job experience, referies na blahblah nyingine kuna segment unazijaza kwenye hiyo online application form.

If you qualify for further steps they will ask for copies if academic certificates and other legal documents such as birth certificate or work permit kwa nchi husika depending na nature ya kazi yenyewe. Then wanna stages mbalimbali zisizopungua mbili mpk tatu.

Kama huja - qualify for further process huwa wanatunza kumbukumbu zako for future job alerts endapo zitamatch your skill. Bado sijafanikiwa kupata job kwenye hizi UN agencies ila I hope my day will come.

Ndio, unatuma resume/cv through email yao waliyoitoa.
Unforgetable
 
Consultant

JF-Expert Member
Jun 15, 2008
10,416
2,000
Asante kiongozi.

Mfano kama wameomba CV tuu, then kwenye CV umeainisha skills zako kulingana na job descriptions zao, je kuna haja ya kuambatanisha na certificates za training mbalimbali ulizofanya?
Kama wameomba CV tu, wape CV tu. Hiyo ndo inaitwa kufuata masharti. Vyeti watakuomba huko mbele baada ya kukutest na kujiridhisha.

Kuna watu wanaamini kwanza kwenye uwezo wa mtu wa kufanya kazi na kudeliver results kabla ya kuja kwenye vyeti.

Kwenye application ukisema una level flani ya elimu hawana haja ya kutia shaka kwani watakuja kuthibitisha baadae kama wanataka kuendelea mbele na application yako

Kila la kheri!
 
Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
49,901
2,000
Kingsmann
Pitia CV tamp lets google pia kuna majarida kama The Economic huwa ya a CV za viongozi wa vitengo. Unaangalia mifano hiyo na kazi unayoomba unaangalia wapi utakuwa na ushawishi kwa elimu na uzoefu wako.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom