Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 48,684
- 149,887
Wanaojidai kutumbua majipu leo hii ni wanasiasa tena kutoka chama kile kile ambacho wanasiasa wake hawakuchukua hatua kuzuia haya yote na baadhi yao walikuwa mawaziri katika serikali iliyopita ambayo ilijitia upofu huku nchi ikiibiwa.
Ukweli ni kwamba uchafu wote huu walikuwa wanaujua ila waliamua kukaa kimya kwasababu zao binafsi ila sasa wanajidai kugeuka na kuwa wakali ili hali baadhi yao wanatuhumiwa kuandika hata "vimemo" kwa watendaji wakuu wa Mashirika na Taasisi hizi za umma wakiwaagiza watendaji hawa wafanye yale wanayoyataka. Habari hii ya kuandika vimemo iliwahi kuripotiwa na gazeti la Mtanzania na haikuwahi kukanushwa popote pale.
Ushauri:
Ma-CEO semeni ukweli hadharani huku mkitoa vimemo hivyo mbele ya camera na mbele ya wanasiasa wanaosema wanawatumbua majibu huku mkiwataja kwa majina na wadhifa vigogo waliokuwa wanawapa maelekezo alafu muone kama kuna kitakachoendelea.Kukaa kwenu kimya hakutawasaidi bali kutawafanya mtumike kuwajenga watu kisiasa.
Jiulizeni mbona TANESCO mpaka leo hii hawaendi?TANESCO itagusa wanasiasa wangapi?