Mliotalikiana tunaomba uzoefu wenu

iMind

JF-Expert Member
Mar 27, 2011
2,873
4,273
Kama mnavyojua ndoa nyingi siku hizi zimekuwa ndoano. Kuna watu wengi ambao wanatamani watoke lakini pengine wanaogopa mambo mbalimbali kama jamii itawaonaje, maisha ya watoto, pengine mmoja wao ni tegemezi n.k.

Sasa wale ambao mmepata nguvu na uwezo wa kusema potelea mbali liwalo na liwe na mkaamua kuanua jamvi, tunaomba uzofu wenu.

1. Ilikuaje ukachukua uamuzi huu mgumu. Ulipata feelings gani na ulio overcome vipi uoga.

2. Maisha baada ya talaka, unajutia uamuzi au unaona uamuzi wako ulikuwa ni sahihi.

3. Uliwezaje ku move on.

4. Malezi ya watoto kama yapo yanaendeleaje je unahisi kuna kitu watoto wanakosa au wako ok.

5. Vipi inatokea una mmisi mwenzi wako na wakati mwingine mnajiiba kukumbushia game au ndo forever.

6. Ushauri wenu kwa wanandoa ambao wana migogoro na wanaishi bila raha na amani ni nini?

Tafadhali naombeni thread hii tuichukulie kwa uzito. Ili iweze kuelemisha. Kama hujawahi kuoa na kuachana ni vyema usichangie chochote, labda uulize au ku comment tu kwa wale watakaochangia.

Asante
 
Mmmh kama mahusiano ya kawaida tu watu wanavurugwa sembuse ndoa..ndoa haina mlango wa kutokea kaeni chini myasawazishe..
 
Kwa kweli ni maamuzi magumu sana kuyachukua unaweza kukaa mwaka mzima hujapata maamuzi?
Kama hujakurupuka kuvunja ndoa ni nadra sana kummiss mwenza wako.
Utata mkubwa ni jinsi ya kila mtu kurudi alipotoka kabla ya kuolewa.
Ushauri: Ndoa nyingi zinavunjika kutokana na nguvu kubwa ya shetani kutoka nje,Msiruhusu kinyago yeyote kujadili kuhusu Ndoa yenu zaidi ya nyie wanandoa wenyewe!
 
Maisha ya ndoa yana changamoto zake kubwa sana inahitaji hali ya uvumilivu ya hali ya juu ikiambatana na busara na hekima.Lakini ikitokea tu katika hali zote kuna mtu ameshindwa vumilia ni lazima ndoa ife na katika kuachana lazima kuna pande moja itapata nafuu na nyingine kuumia.Mnaweza kuachana na maisha yakaendelea na wote mkaridhika na maisha mapya .muhimu nikuachana kwa wema
 
Back
Top Bottom