Uchaguzi 2020 Mliosoma na kuiva vyema kabisa katika 'Political Science', kauli ya kidhaifu kama hii ifuatayo inaruhisiwa kutamkwa na aliyeshikilia Mpini?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
39,312
2,000
"Nichagueni Mimi GENTAMYCINE si mmeona kabisa Maendeleo niliyowafanyia? Kamwe msiwachague hao Wahuni, wanaotumiwa na akina Trump na Johnson. Nichagueni tu Mimi GENTAMYCINE ambaye kiukweli ndiyo nayajua matatizo yenu makubwa na msiwachague kabisa hao wengine kwani ni Mafisadi, Waongo na hawana Uchungu na nchi yetu hii ya Malawi ya Kaskazini kabisa. Nichagueni Mimi GENTAMYCINE kwani ndiyo Masikini mwenzenu na kamwe msiwachague hawa Mawakala wa Mabeberu ambao wengi Wao huwa hawaishi Malawi ya Kaskazini na wala hawana nia njema nayo kabisa "

Sasa kama tu Mgombea 'Mshika Mpini' anazuia Wananchi wa Malawi ya Kaskazini wasiwachague 'Washindani' wake je, na Wao wasemeje labda?
 

Graph Theory

JF-Expert Member
Jul 2, 2011
4,638
2,000
Nimesomea kuchunga mbuzi, nawapisha wataalamu wa politiko sayansi waje wadadavue.

Kama wewe GENTAMYCINE ni mzalendo na maskini mwenzangu, acha kugombea, njoo tuchunge mbuzi.

Bai ze wei, si ulikuwa una'ropoka' kuwa kuongoza nchi Ni kugumu hadi unalala na mafaili, mbona tena umeamua kuendelea kushika mpini?

Au kulima umekuzoea, na Sasa hutaki tena kuacha kushika mpini?
 

Chief Kabikula

JF-Expert Member
Jan 1, 2019
6,608
2,000
Ujuaji ukizidi matokeo yake ndio haya sasa .Kufanya Mambo bila busara impact yake ndio hii , Kuna maamuzi na Mambo aliyafanya ndani ya miaka mitano bila kuangalia matokeo yake , Sasa ndio muda unampa majibu na bado hasa plan b ya Lissu hatoamini.
 

MPIGA ZEZE

JF-Expert Member
May 16, 2011
2,520
2,000
Hapo ndipo utajua mlozi aliyeiroga Malawi ya Kaskazini aliishatangulia mbele ya haki na tunguri zake!! Baada ya kuambiwa hayo Wamalawi wanashangilia na kucheza mdundiko.

Sasa hawa watoto wa wanyonge siwangewaacha tu wakafurahia utoto wao, wakacheza huko mitaani (hata kama hakuna bustani za kuchezea), wakafurahia shule zao badala ya kuwalisha bangi za siasa kabla ya wakati wao.

Na hao wazazi wa Malawi ya Kaskazini wanaowaruhusu watoto wao kushiriki kwenye siasa, kweli wanazo akili timamu? Mimi mtoto wangu ama anakwenda shuleni au anabakia nyumbani.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom