Mliosoma Magazeti ya leo

Job K

JF-Expert Member
Oct 4, 2010
9,278
2,000
Wakuu kwa wale mliosoma magazeti ya leo kuna habari nilisikia kwenye redio wakati nawahi kanisani misa ya kwanza. Habari yenyewe ilikuwa ikimhusu Mkuu wa mkoa wa Darisalama, nilisikia kama anatukana watu kwamba ni wajinga na wapumbavu kwa kuhoji anakopata pesa ya kusaidia makundi mbali mbalia. Sasa sikuifuatailia kwa vile nilikuwa nawahi kanisani! Sasa kwa wae wa Darisalama kama mmeiona hiyo habari hebu tupeni kwa undani ilikuwaje?

Na hii kasumba ya kutukana watu sijui imeanzia wapi? Hawa jamaa kupata madaraka wanajiona miungu watu!! Mara tuambiwe marofa na wapumba.vv, mara tuitwe vilaza almradi kila mmoja anaropoka kadri alivyojaliwa!!
 

slim b

JF-Expert Member
Nov 6, 2016
322
225
Kwani na nyinyi mnaetukana vipi nanyi mnatoka upande Wa wazee waliosema malofa ama!?
 

TUJITEGEMEE

JF-Expert Member
Nov 6, 2010
15,865
2,000
Mimi nimesoma Mzalendo (18/12/2016). Ukurasa wa Tano, kulikuwa na habari ya Mh. Ridhiwan akishauri nini cha kufanya ilikuboresha elimu. Amesema yeye alipomaliza shule ya sheria, alikuwa hajui kitu, kazi yake ilikuwa kubeba mabegi ya wanasheria mahakamani na alitumia furusa hiyo kutetea uwezo wake mpaka akakubalika. Ameongeza kusema kuwa hakuna jibu sahihi la tatizo la ajira bila kuwa na mfumo bora wa elimu wenye kuwandaa vijana kujitegemea. Habari hiyo imeandikwa na Mariam Mziwanda.
 

Ikwanja

JF-Expert Member
Jul 12, 2011
2,083
1,500
Mara Mashetani, na huo ni mwak mmoja , sasa ngoja uanze mwaka wa pili, tutajujua
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom