Mlioshuhudia vita mbalimbali njoeni mtupe uzoefu

Eng. Zezudu

JF-Expert Member
Aug 23, 2012
7,811
10,819
Mimi ni kijana wa Kitanzania nimezaliwa miaka ya 1990's.

Nimekulia maisha ya kawaida sana. Nyumbani tumeanza kumiliki TV miaka ya 2003 mwishoni. Habari ya vita halisi siijui zaidi ya kuangalia vita kwenye TV muvi ya Rambo, Warbus, Eastern condors na muvi za kivita za Frank Zagarino.

Mauaji ya kimbari Rwanda sijayaona mana nilikuwa mdogo na sikuelewa kitu zaidi ya kuangalia kwenye muvi tu

Marekani alipomvamia Iraq, tulikuwa hatuna TV kwa hiyo sikuona kitu.

Babu alikuwa askari lakini hakuniadithia show ilivyokuwa kwenye vita ya Kagera. Lakini naimani kuna watu humu mmeshuhudia na kuhadithiwa na ndugu zenu vita mbalimbali vilivyoikumba nchi yetu na dunia kwa ujumla.

Kuna watu wanashabikia vita hii ya tatu ipigwe bila kufikiri madhara yake, nchi yetu ni dependant country hao wanao pigana.

Wazoefu wa mambo ya vita tupeni hali inavyokuwa katika mapambano.
Ili sisi wazaliwa wa 1990's tujifunze kitu na tuache kushabikia vita.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Soma hii misemo ya wahenga mkuu, huenda ukang'amua chochote kuhusu vita!

1- Vita vya panzi, furaha kwa kunguru.

2-Wapiganapo mafahari (madume ya ngo'mbe), ziumiazo ni nyasi.

Kwahiyo hapo unaweza kuangalia vita kwa upande namba moja, mwingine akaangalia upande namba mbili.
 
Mimi nimeshuhudia vita mbili na moja wapo nilikuwemo
Vita isikie tu kwani inaharibu uchumi kufumba na kufumbua tu
Taharuki inaanza pale mashambulizi yanaanza na hujui uende wapi huku tumbo linaunguruma
Hapo ndio unajiongeza baada ya kuona wengine wakifa na wengine wakivamia mali ili mradi wapate cha kuingiza tumboni wao na watoto wao
Watu wanakimbia na hawajui wanakoelekea unapishana na watu kule unakokimbia wao ndio wanaenda sasa anaeenda kufa hujui ni wewe ama wao

Vita kadri inavyoendelea na chakula kinaanza kwisha na hapo ndio ule usemi wa survival of the Fittest inaingia
Na ndio mpaka leo nadunda ila sio kwa ujanja tu bali mda wangu haujafika tu

Sent from my iPhone using Tapatalk
 
aise, Sasa mpambano wa Marekani na Iran ungelipuka sisi Dunia ya Tatu tutaomba wapi misaada. Tukiomba msaada lazima tupewe mashariti ya kutuma wanajeshi wetu kwenye mpambano ndo tunapata msaada.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mfano mzuri wa vita cheki movie za akina maiko Didikofu, warbus ,choknoris na Rambo wameigiza uhalisia 90 asilimia Yale ndiyo maisha ya kivita yanavyokuwa achana hizi zenye 3rd effects
 
Umewahi adithiwa kuhusu Mabomu ya Mbagala na Gongo la Mboto jinsi yalivyoleta madhara. Nasikia watu walikimbia bila nguo mida ya ucku.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mfano hili hapa
IMG-20200109-WA0004.jpeg
 
Vita sio vizuri wee sikia tuu kwa majirani
Mimi ni kijana wa Kitanzania nimezaliwa miaka ya 1990's.

Nimekulia maisha ya kawaida sana. Nyumbani tumeanza kumiliki TV miaka ya 2003 mwishoni. Habari ya vita halisi siijui zaidi ya kuangalia vita kwenye TV muvi ya Rambo, Warbus, Eastern condors na muvi za kivita za Frank Zagarino.

Mauaji ya kimbari Rwanda sijayaona mana nilikuwa mdogo na sikuelewa kitu zaidi ya kuangalia kwenye muvi tu

Marekani alipomvamia Iraq, tulikuwa hatuna TV kwa hiyo sikuona kitu.

Babu alikuwa askari lakini hakuniadithia show ilivyokuwa kwenye vita ya Kagera. Lakini naimani kuna watu humu mmeshuhudia na kuhadithiwa na ndugu zenu vita mbalimbali vilivyoikumba nchi yetu na dunia kwa ujumla.

Kuna watu wanashabikia vita hii ya tatu ipigwe bila kufikiri madhara yake, nchi yetu ni dependant country hao wanao pigana.

Wazoefu wa mambo ya vita tupeni hali inavyokuwa katika mapambano.
Ili sisi wazaliwa wa 1990's tujifunze kitu na tuache kushabikia vita.

Sent using Jamii Forums mobile app
IMG-20200109-WA0000.jpeg
IMG-20200109-WA0002.jpeg
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom