Mliooa: Inaweekana mke wako akakuambia kila kitu cha kufanya

Jurrasic Park

JF-Expert Member
Sep 13, 2013
3,797
6,795
Habarini wana MMU

Siwezi kuiita shida ila naona nakosa confidence kwenye ndoa yangu maana sina usemi.

Nilikulia familia ya kishua sana (kitoto mayai) mpaka pale nilipokuja kuoa. huyu mke wangu tulijuana A level. Mapenzi yalianzia hapo mpaka tukaoana.

jambo ambalo nalileta hapa huyu mke wangu ndo ananipa akili zote za kuishi. ndiye anayeniambia nini cha kufanya na kipi siyo. tuanzishe biashara gani, miradi gani na nifanye nini.

japokuwa kila analoniambia huwa nafanya na nashukuru kila kitu kinaenda kama anavyonielekeza. sasa nimekosa usemi ndani ya nyumba siwezi kuleta wazo lazima anirekebishe mpaka naona chuki ndani kwa ndani.

nimejaribu kuwaza nami nitoe mawazo yangu kama mwanaume baada ya kuyachambua kwa akili yangu ila mke wangu akisikia ananikalisha chini na kuanza kunipa somo. mwisho wa siku nakuwa nishakubalia kila ushauri

sasa hapa nina chuki kubwa kwake kwanini kila kitu ananieleza kama mtoto. sina maamuzi japo tunaishi vizuri tu.

kwani hakuna matatizo yatakayo nipata mbeleni kwa kuata mawaz?
 
Kaa nae kwa upole ikiwezekana baada ya game, mweleze yote haya uliyotueleza na ni jinsi gani yanakufanya ukose confidance kama mwanaume. Hii iweke kama section A ya mtihani, kukiwa hakuna mabadiliko tafuta section B.
 
Mkuu mazoea huwa yanajenga tabia na Tabia hujenga mazoea

Ulikosea toka mwanzo na kum'badilisha au kutaka kubadilisha hiyo hali ni lazima utakumbana na changa moto nyingi

maana ulijingea kutokuwa na maamuzi na yeye aka amini hivyo sasa unapoanza kutafta uwe na maamuzi lazima utaleta sintofahamu ndani ya nyumba

na mwisho wa siku atakuja kukwambia kuna mwanamke anakuzuzua
 
kama hakuvunjii heshima, anakupenda , anakupa mawazo na unayaona yako vizuri unataka nini? naomba namba ya mkeo ya simu awe mshauri wangu wew Rudi kwenye ushua wako
 
hah hah hah unanichekesha sana mkuu...nadhani umesahau ule usemi usemao 'si vema kusafiria nyota ya mwenzako' there are so many fish in the river..you better get yours hah hahah
 
Wacha ushamba ww matatizo yako na mkeo usiyalete hapa malizana nae mwenyeo nyumbani hizo tabia za kipumbavu kabisa mambo ya kuduluhisha mwenyeo unatuambia sisi huoni kama tabia za kike hizo ndomana unapelekeshwa kwasababu huna msimamo kwenye maamuzi yako take care
 
Kosa kubwa ulishalifanya, hivyo hakuamini tena ndio maana anakupinga kila wazo utoalo.
Mfanye mkeo awe yo best friend, kaa nae mzungumze then take action na usiharibu ili ile imani uliyoivunja uirudishe kama mwanaume.
 
Sioni tatizo hapo, mke ni mshauri wako mkuu,
Kwani ukimpa wazo na yeye akaliboresha kuna tatizo gani? Au akitoa yeye na likafanikiwa kua shida yoyote? Au kwa kua ni mwanamke kasema.
Niamin mkuu mwenye mapenzi na uchungu wa kutaka maendeleo yako ni mkeo huko kuona utakuja kupata shida huko mbeleni ni uwoga wako tu.
Mwanaume ni mwanaume na atabak kuwa mume acha uwoga.
 
Walah wayasemayo wazee ni kweli kila ndoa ina cha utofauti adi mtu unawaza kama yote haya yanayotokea basi wanandoa wanamioyo ya uvumilivu sanaa
 
Umeandika pumba kabisa tena we ni kilaza wa kiwango cha lami acha kudhalilisha uanaume kwani huyo mke walikutongozea mpaka mambo ya msingi anayo kuelekeza umchukie wanaume hatuwachukii wanawake ila tunawaelekeza tu na wana tii
 
Habarini wana MMU

Siwezi kuiita shida ila naona nakosa confidence kwenye ndoa yangu maana sina usemi.

Nilikulia familia ya kishua sana (kitoto mayai) mpaka pale nilipokuja kuoa. huyu mke wangu tulijuana A level. Mapenzi yalianzia hapo mpaka tukaoana.

jambo ambalo nalileta hapa huyu mke wangu ndo ananipa akili zote za kuishi. ndiye anayeniambia nini cha kufanya na kipi siyo. tuanzishe biashara gani, miradi gani na nifanye nini.

japokuwa kila analoniambia huwa nafanya na nashukuru kila kitu kinaenda kama anavyonielekeza. sasa nimekosa usemi ndani ya nyumba siwezi kuleta wazo lazima anirekebishe mpaka naona chuki ndani kwa ndani.

nimejaribu kuwaza nami nitoe mawazo yangu kama mwanaume baada ya kuyachambua kwa akili yangu ila mke wangu akisikia ananikalisha chini na kuanza kunipa somo. mwisho wa siku nakuwa nishakubalia kila ushauri

sasa hapa nina chuki kubwa kwake kwanini kila kitu ananieleza kama mtoto. sina maamuzi japo tunaishi vizuri tu.

kwani hakuna matatizo yatakayo nipata mbeleni kwa kuata mawaz?
Kwanza ulipaswa kushukuru kupata mwenye akili ya maisha kama huyo maana wenzio wengi wana vimeo vinavyowaza kila siku mitoko na fashion za mjini tu, cha muhimu usimchukie wala kuleta kiburi maana yy ndio anasaidia mafanikio ya familia yenu. Mawazo yake mazuri yatumie as long as yanaleta mafanikio ila na ww jiongeze ukibuni kitu kitafakari kabla ya kujadiliana nae na uwe na msimamo
 
I wish ningekuwa na mke kama huyo. Yaani kuna ubaya gani mke kukushauri, na kama anakushauri vizuri na mambo yanaenda?

Kama angekuwa ana kushauri halafu mambo anayokushauri hayaendi vizuri lakini ana lazimisha hapo ndo ingekuwa vibaya.

Jiamini kaka. Ndo maana wanasema behind any successiful man there is a woman. Itakuwa ni kichekesho kumchukia mtu eti kwa sababu anakushauri.

Kama akikushinda naomba unipe huyo mke. Wengine wake zetu akili zao ziko likizo, yaani unafikiria each and everything mwenyewe. Hata pale unapo mpa mawazo atekelezi.
 
Back
Top Bottom