Nzige The Bless
JF-Expert Member
- Aug 20, 2018
- 990
- 738
Asante. Hapo kwenye hiyo post nimekujibu ninajua kwamba Mungu ndiye alieumba vitu hivyo kwa maana hakuna kiumbe yoyote anayeweza kuumba ulimwengu usioonekana (malaika n.k) na ulimwengu huu unaoonekana(sayari zote na vyote vilivyomo). Pia nilikujibu kwenye post #153 kutokuweza kwa kiumbe yeyote kuumba ulimwengu usioonekana na unaoonekana kunathibitisha kwamba yupo Mungu pekee ambaye alieumba uumbaji wote(usioonekana na unaoonekana). Majibu haya nimeyarudia tena kwa faida ya akili zako. Asante.Post #150 umeandika hivi.
"Nimekupa uthibitisho wa uumbaji wake nikakutajia mpaka vitu alivyoumba , ninajua kwamba Mungu ndiye alieumba vitu hivyo kwa maana hakuna kiumbe yoyote anayeweza kuumba ulimwengu usioonekana (malaika n.k) na ulimwengu huu unaoonekana(sayari zote na vyote vilivyomo), najua kwamba Mungu yupo kwa ushahidi wa uumbaji wake, hakuna kitu kinaweza kutokea bila muumbaji"
Nakuuliza hivi.
Unajuaje kwamba huo unaouita uumbaji wake ni uumbaji wake kweli, na kwamba, hiyo habari ya "uumbaji wake" si hadithi za watu tu wanaosema huu ni uumbaji wake kwa sababu hawajui uumbaji huu umetokea vipi?
Kujua kwamba hakuna kiumbe anayeweza kuumba uumbaji huo hakuthibitishi Mungu yupo wala kaumba.
Hujajibu swali hili.
Nakupa mfano mdogo mmoja, hakuna kiumbe yeyote anaweza kuumba bahari na vyote vilivyomo ndani ya bahari(samaki n.k). bali ni Mungu pekee ndiye alieumba uumbaji huo.