Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 71,277
- 105,475
Hujajibu kwa nini Mungu mwenye ujuzi wote, uwezo wote na upendo wote kaumba ulimwengu ambao mabaya yanaweza kutokea.1. Sio wewe tu kunya, kila kiumbe amemuumbia hivyo, hasa sisi tunaoishi ulimwengu unaoonekana(Duniani). Kuanzia binadamu, wanyama, ndege na samaki woote tunakunya haja kubwa na ndogo. Huu ni mfumo alituumbia ili kutoa taka mwili. Chakula unachokula kikishameng'enywa kinachujwa kisichotakiwa mwilini kinatoka kama taka mwili. Kwa wanyama inasaidia kupatikana mbolea.
2. Baada ya Mungu kuiumba dunia na kutuumba binadamu, sisi viumbe binadamu kwa lifestyles n.k tukaiharibu dunia kwa namna tofauti na maradhi kutokea. Lakini Mungu akatufunulia binadamu akili ya kuunda madawa(Hospitalised Medicines) ambayo madawa haya hutokana na mimea ambayo aliyoiumba, pia kupitia mimea na matunda ni tiba kubwa ambayo ametuumbia. So kutufunulia uwezo wa kutengeneza madawa ni njia ya kutuwezesha sisi kutibu maradhi mbalimbali.
3. Hili limekaa kiimani zaidi na mimi sitaki kuingia kwenye mada hiyo. Hilo ni somo jingine. Lakini kwa faida yako hapo mwanzo Mungu alivyoumba dunia na viumbe wote, alituumba kwa kusudi zuri na hakukuwa na contents kama unazosema. Lakini uharibifu uliofanywa na kiumbe kisichoonekana(malaika aliehasi) kwa kuharibu utaratibu alioukusudia Mungu kwa kiumbe binadamu(Binadamu ambae aliumbwa ili kutawala vitu vyote alivyoviumba Mungu duniani) ndio chanzo cha uharibifu wote hapa duniani. So ni huruma ya Mungu bado anatuvumilia.
4. Mungu yupo na anavumilia uovu wote unaofanywa duniani na kiumbe binadamu aliyeharibiwa na kiumbe kisichoonekana(malaika aliehasi), LINI NA SAA NGAPI ATAKOMESHA UOVU WOTE ANAJUA YEYE PEKEE MUNGU ALIETUUMBA. Kuvumilia kwake kusikupotoshe hata kidogo kwamba hayupo na haoni.