Mlioko Bagamoyo haya ndo Mavitu tunayoyafanya muda huu.

Bill Lugano

JF-Expert Member
Aug 20, 2018
1,130
2,000
Nipo na Marafiki wengi baada ya kazi tulikubaliana tukutane wote Mlimani City Tule then tuanze safari ya kuja Bwagamoyo.

Leo nimetumia GMC.... Kwenye Gari yangu nipo na Jamaa yangu mmoja then marafiki zangu wengine nao wamechukua gari zao Jumla ni msafara wa magari 7.

Safari ilianza vizuri jamaa wengine wamebeba Mabint mimi na jamaa mwingine hatukupata bahati ya kuwa na warembo wa kutoka nao. Sijawahi kiukweli nadhani sababu ya woga naposikia habari za mabinti wengi wa TZ.

Tumefika sehemu moja wanaita tegeta tulipark gari pembeni na kushuka kuwapa tu Traffic waliokuwa barabarani Wekundu wekundu. Tulikubaliana hivyo kuwa kila tunapokuta kuna traffic barabarani tunashuka kuwapa pesa za pongezi wanafanya kazi katika mazingira magumu sana.

Nlishuka na 60,000 nikagawa kwao walikuwa 3 na jamaa zangu nao wakashuka kugawa kwa wote. Ni kama kuwatuza hivi. Kiukweli wanafanya kazi ngumu na mazingira magumu.tukawaaga tukafika mbele tena nikashuka na 100,000 walikuwa watano nikagawa. Na wenzangu pia.

Kufika sehemu tukakuta wauza mahindi hawa nao tuliwapa 10,000 kila mtu. Tunafurahi na watu hatuna roho mbaya.

Bwagamoyo nako tuliendelea kufanya uungwana nlikuwa nmeweka kama 400,000 kwenye kile kijikabati cha gari.nadhani zimeisha maana baadaye nikawa nachota tu.sijui maybe kuna mabaki.

Tumefika Camp Site. Jamaa yetu alishaandaa mazingira hiyo sehemu. Baada ya harakati nyingi. Maana kuna mabinti waliletwa wamekunywa Hennesy ,Jack Daniels ,John Walker, Heineken n.k wamepagawa sana.

Hapa kuna kila something choma... Yaani Kuku Choma, Nyama Choma, Samaki Choma. Vipo. Watu wana enjoy tu hawana maneno.

Zoezi ambalo nmelipenda... Sisi wenye magari tupo watatu na wenye Toyota wapo pia na mmoja ana Subaru. Ikafika wakati kuna mabinti watukutu wanataka kucheza juu ya Bonnet ya Gari au Usafiri wa mtu.

Hapa ilileta hali ya sintofahamu kidogo. Jamaa wa Subaru na Toyota Mark X na mwingine Harrier. Hawa wamegoma. Kuwa wao hawataruhusu mtu apande juu ya bonnets za Toyota na Subaru yake.

Mi nikaona siyo shida. Nikaleta GMC karibu na nikamwambia Jamaa yangu ambaye aliomba nimwazime FORD RANGER naye asogeze mabinti waweze (ku twerk). Huwezi amin wale mabinti kuna wenye kilo above 80 mpaka 90+ wamesimama wanacheza bila shida. Bonnet zimetulia tu.

Jamaa wengi wameshangaa wanasema ingekuwa usafiri wa Mjapani basi wale wadada wangeweza kudumbukia ndani.yaani ile kusimama pale juu miguu ingetoboa bonnet au bonnet ingeenda gusana na injini kwa kubonyea. Wakasema labda mkonga ndo ungehimili.sasa hapo nikawaambia mtu mwenye akili timamu atakujaje na mkonga ku party badala ya kwenda nao porini?

Bagamoyo tutakuwepo mpaka kesho mchana. Then tutaanzisha msafara wa kurudi town kwa ajili ya mapumziko siku ya nyerere. Hapo sijajua maana kuna wanaosema twende white sands hotel kuna wanaotaka twende Hotels zilizopo Ukanda wa Mbezi huku. Yaani tupitie moja baada ya nyingine tutakayoona inafaa tutulie hapo.

Nyerere day tutakuwa na msafara wa gari 12. Na zote tumekubaliana ziwe SUV za ukweli. Kuwa asitokee mtu akaja na gari ambayo bei yake ni chini ya Mil 80. Pia isiwe imewahi gongwa au pakwa rangi. Isiwe imepitisha miaka 3 toka itengenezwe.

Masharti yetu yana lengo la kuwa motivate watu kununua gari na siyo vipando au vyombo vya usafiri.mimi ntatumia Range Rover Sport. Kama kawaida sina gari ambayo imepitisha 3 years toka itengenezwe. Na sina gari yenye kms zaidi ya 100,000.

So wadau kama unataka kujumuika nasi tuwasiliane. Safari yetu itaanzia Hotel moja iliyopo katikati ya Jiji then ndo tutakuwa na msafara huo. Karibuni sana.

Mapovu yenu bakini nayo mi natumia washing machine. Hayo mapovu ya sabuni ya kipande hayatanisaidia kitu.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom