mbingunikwetu
JF-Expert Member
- Feb 17, 2015
- 13,663
- 18,037
Jamii ya watanzania wanavyoelewa ni kwamba kazi ya ualimu ndiyo yenye mshahara mdogo kuliko kazi zingine zote. Hivyo hii imepelekea hadhi ya mwalimu kwenye jamii kushuka sana na mwalimu kuhesabika kuwa ni duni katika jamii. Lakini hii si kweli hata kidogo. Msichana akitaka kuchumbiwa na mwalimu anajisikia mnyonge, na mara nyingi hukataa labda akihisi kuwa umri unamtupa mkono au akiona hajapata chaguo la moyo wake.
Ukweli ni kwamba watumishi wote wa serikali (walimu na kada zingine) mishahara yao iko chini sana! Lakini ukiilinganisha hiyo mishahara yao midogo, mshahara wa mwalimu unakuwa juu kidogo kuliko kada zingine isipokuwa kwa kada ambazo wanasoma miaka mingi zaidi kama madaktari, wafamasia na wahandisi.
Ngoja niwaanikie hapa:
Mishahara ya walimu wanaoanza wenye digrii ya kwanza:
Hadi Juni 2022 walikuwa kwenye TGTS D1 = 716,000/=
Kuanzia Julai 2022 wanakuwa kwenye TGTS D1 = 771,000/=
Mishahara ya kada zingine wasio walimu wenye digrii ya kwanza:
Hadi June 2022 walikuwa kwenye TGS D1 = 710,000/=
Kuanzia Julai 2022 wanakuwa kwenye TGS D1 = 765,000/=
Kwa hiyo hadi Juni 2022 mshahara wa mwalimu ulikuwa unazidi mshahara wa kada nyingine kwa sh 6,000/=.
Kuanzia Julai 2022 mshahara waq mwalimu unazidi mshahara wa kada zingine kwa sh 6,000/= pia.
Kwa wastani mishahara ni midogo kwa wote japo jamii inaamini kuwa mwalimu ndiye mwenye mshahara mdogo wakati siyo kweli. Wahanga wa uongo huu wamekuwa ni wasichana kukataa kuolewa na walimu na kushobokea kada zingine kwa kigezo cha mshahara.
Mtumishi wa serikali akilalamika kuwa mshahara ni mdogo watu wanakimbilia kusema kuwa huyo lazima atakuwa ni mwalimu.
Nashauri tuwaheshimu sana walimu wetu, tusiwabeze bali tuwatie moyo maana kazi yao ni ngumu na ni muhimu sana. Kinachoendelea kwenye mitandao ya kijamii kwa sasa ni kukejeli walimu eti ndio wanaolalamikia nyongeza kiduchu ya mshahara mwaka huu kinyume na matarajio yao.