Mliokaririshwa uongo kuwa mishahara ya walimu ni midogo kuliko watumishi wengine wa serikali, nawaanikia hapa

mbingunikwetu

JF-Expert Member
Feb 17, 2015
13,661
18,035
Jamii ya watanzania wanavyoelewa ni kwamba kazi ya ualimu ndiyo yenye mshahara mdogo kuliko kazi zingine zote. Hivyo hii imepelekea hadhi ya mwalimu kwenye jamii kushuka sana na mwalimu kuhesabika kuwa ni duni katika jamii. Lakini hii si kweli hata kidogo. Msichana akitaka kuchumbiwa na mwalimu anajisikia mnyonge, na mara nyingi hukataa labda akihisi kuwa umri unamtupa mkono au akiona hajapata chaguo la moyo wake.

Ukweli ni kwamba watumishi wote wa serikali (walimu na kada zingine) mishahara yao iko chini sana! Lakini ukiilinganisha hiyo mishahara yao midogo, mshahara wa mwalimu unakuwa juu kidogo kuliko kada zingine isipokuwa kwa kada ambazo wanasoma miaka mingi zaidi kama madaktari, wafamasia na wahandisi.

Ngoja niwaanikie hapa:

Mishahara ya walimu wanaoanza wenye digrii ya kwanza:
Hadi Juni 2022 walikuwa kwenye TGTS D1 = 716,000/=
Kuanzia Julai 2022 wanakuwa kwenye TGTS D1 = 771,000/=

Mishahara ya kada zingine wasio walimu wenye digrii ya kwanza:
Hadi June 2022 walikuwa kwenye TGS D1 = 710,000/=
Kuanzia Julai 2022 wanakuwa kwenye TGS D1 = 765,000/=

Kwa hiyo hadi Juni 2022 mshahara wa mwalimu ulikuwa unazidi mshahara wa kada nyingine kwa sh 6,000/=.
Kuanzia Julai 2022 mshahara waq mwalimu unazidi mshahara wa kada zingine kwa sh 6,000/= pia.

Kwa wastani mishahara ni midogo kwa wote japo jamii inaamini kuwa mwalimu ndiye mwenye mshahara mdogo wakati siyo kweli. Wahanga wa uongo huu wamekuwa ni wasichana kukataa kuolewa na walimu na kushobokea kada zingine kwa kigezo cha mshahara.

Mtumishi wa serikali akilalamika kuwa mshahara ni mdogo watu wanakimbilia kusema kuwa huyo lazima atakuwa ni mwalimu.

Nashauri tuwaheshimu sana walimu wetu, tusiwabeze bali tuwatie moyo maana kazi yao ni ngumu na ni muhimu sana. Kinachoendelea kwenye mitandao ya kijamii kwa sasa ni kukejeli walimu eti ndio wanaolalamikia nyongeza kiduchu ya mshahara mwaka huu kinyume na matarajio yao.
 
Walimu Hawana dili Wala marupurupu ya ziada Kama kada nyingine, hiki Ndo kinawafanya kua maskini Sana

1. Dreva wa halmashaur ana mshahara mdg kuliko mwalimu ila atapiga dili za vifusi,mchanga,kokoto n.k night za misafara n.k

2. Afisa biashara au ardhi wa halmashaur ana mshahara mdg kuliko mwalimu,
Ila atapiga rushwa za leseni za kufa mtu.

3. Afisa mifugo au kilimo atapiga elfu tano tano za sindano mifugo ya watu au atalima mashamba yake uko uchochoroni kwa kutumia dawa au pembejeo za ruzuku za serikali.

4. Mfamasia atakula laki tano tano kila mwezi for free za cheti chake tu kutumika kwny maduka ya dawa ya watu uko mitaani uku katulia tu..

5. Daktar au nesi wa halmashaur,
Hawa dili za semina,mafunzo n.k Ni nyingi mno(covid 19, chanjo, ukoma, malelia n.k). Hapo bado hawajaiba vifaa Tiba na kuviingiza mtaani kwenye hospital binafs.
Kuna na mabwana afya kaam matrafiki TU, wanatupiga Sana elfu hamsin hamsi Za faini uku mitaani

6. Wahasibu na maafisa manunuzi wa halmashaur wanapiga Sana dili za kimahesabu na 10% wakishirikiana na maboss wao (wakurugenz) ili Kupiga Cha juu kwenye tenda na matumiz mbalimbali ya fedha kwny halmashaur.

7. Maengineer wa halmashaur Ndo kabsaa wezi wakubwa, wao kila mradi wa serikali wakipewa kusimamia Lazima umalizike na yeye tayar ana kijumba keshakijenga kwa material zile zile za mradi.

8. Maafisa masjala wao Ni Kama matrafiki au madalali wa viunga vya halmashaur, una faili lako pale kwa mkurugenz au mkuu wa wilaya,ili likimbie chap chap Lazima utamwachia elfu 2 au elfu 5 ya maji.

9. Afisa maliasili wa halmashaur Hawa Ni wazee wa madili na rushwa za misitu,mikaa,mbao na magendo mbalimbali ya serikali.

10. Afisa utumiishi Hawa ndio wazee wa madili ya watumishi hewa.
Mtu anafariki, ripoti haiendi hazina kusitisha mshahara. Inatolewa ripoti ya mwajiriwa kubadili account yake, mshahara wa marahemu wanaula hata miaka 10 mfulurizo bila yeyote kujua.
mtu anamakosa ya kinidhamu,kasimamishiwa mshahara. Ripoti haiendi hazina, inabadilishwa tu account. Wanaupiga kimya kimya. Ukisamehewa ukarudishiwa mshahara, ule wa nyuma hata uulizii.
mtu anaripoti Ila haendi kituo Cha KAZI, au anaacha kazi anaenda zake private kwa muda.
wanakula dili na afisa utumishi, wanaugawana nusu nusu huku yeye Yuko zake private sector anapiga Ela nyingine.

Kama Kuna mtumish mwngne wa halmashaur nmemsahau nikumbushe.

Ila kiuhaisia mwalimu nje ya mshahara sijui atapiga dili gani atoboe,

ukiachilia mbali suala la twisheni ambalo bado kipato chenyewe Ni kidg mno na jasho linalomtoka Ni jingi mno

Sijui atapiga dili gan jingine maana vitabu vyote vya serikali vimeandikwa "HAKIUZWI", boksi lenyewe la chaki Mtaani halizidi hata elfu 2.
 
Walimu Hawana dili Wala marupurupu ya ziada Kama kada nyingine, hiki Ndo kinawafanya kua maskini Sana

Dreva wa halmashaur ana mshahara mdg kuliko mwalimu ila atapiga dili za vifusi,mchanga,kokoto n.k night za misafara n.k

Afisa biashara au ardhi wa halmashaur ana mshahara mdg kuliko mwalimu,
Ila atapiga rushwa za leseni za kufa mtu.

Afisa mifugo au kilimo atapiga elfu tano tano za sindano mifugo ya watu au atalima mashamba yake uko uchochoroni kwa kutumia dawa au pembejeo za ruzuku za serikali.
Sasa huo ni wizi!! Ni mtu mjinga peke yake anayeweza kufurahia kipato cha wizi na cha udanganyifu kisicho halali!! Fikiria msichana anayemkubali mtu anayeonekana ana kipato kikubwa lakini kumbe chanzo chake ni wizi, halafu ni kweli mtupu kuwa siku za mwizi ni arobaini! Kuna siku atakamatwa na kufukuzwa kazi na kifungo juu!! Walimu wana maisha mazuri, wanajua kulea watoto wao vizuri na wana maadili sana!! Inasikitisha watanzania kujivunia kazi kwa kuwa ina "fursa" za wizi na udanganyifu!!
 
Walimu wakitaka wathaminiwe na selikari ijali maslahi yao, just simple, walimu wote wasiombe kazi za muda uchaguzi mkuu 2025.

Selikari haiwezi kuwabana majobless eti waibe kura fisiemu iibuke kidedea.

Walimu wote kuacha kuomba kazi za muda uchaguzi mkuu 2025 Hilo haliwezekani kila mtu anajua.
 
Wanabakia na laki na nusu kwa mwezi baada ya mikopo, pili hawana kamba za kuvuta
Mikopo wanayo watumishi wote! Kama ni mikopo ya bodi ya elimu ya juu wanayo watumishi wa kada zote, kama ni mikopo ya benki na sakosi wanayo pia watumishi wote! Hayo ndiyo mambo waliyokaririshwa kuwa eti ni walimu tu wenye mikopo wakati siyo!
 
Wanabakia na laki na nusu kwa mwezi baada ya mikopo, pili hawana kamba za kuvuta
Hilo pia siyo kweli! Mtumishi lazima abaki na theluthi moja ya mshahara wake katika mazingira yoyote yale! Nimetoa mfano wa mwalimu graduate ambaya kwa sasa atakuwa anapata 771,000/=. Huyo akikopa sana lazima abakize sh 257,000/= kwenye mshahara wake. Lakini pia wengi wanakopa siku hizi kwa ajili ya kuendesha miradi mbalimbali kama kuku wa mayai au nyama, ng'ombe wa maziwa, shamba nk. Kwa hiyo japo anabakiza mshahara kidogo lakini ana kipato kingine cha pembeni na cha halali kuliko wale wanaojisifia wizi!!

Walimu wana maisha mazuri sana kwa kutumia akili yao kwa halali. Nenda shule yoyote iwe ya msingi au ya sekondari uangalie magari ya walimu waliyopaki hapo. Walimu wengi wamejenga nyumba zao za kisasa na wana miradi mbali mbali na watoto wao wanasoma vizuri kwenye shule nzuri. Tatizo mmekaririshwa matango pori!
 
Kwenye kata yetu sijaona mtu wa kada nyingine alieomba hizi kazi za muda za sensa ni walimu tu tena ni wengi.

Shule ambayo mkuu wake ndo anafanya usaili ndo wameenda kama walimu shule nzima. Sasa hapo kweli utasema hawa jamaa huko kuna maslahi waanze kugombania hizi kazi ambazo naamini tu ni za shurba na kuzurula kwiingi wakati muda huo ungeutumia kupumzika na familia ama kufanya ishu zako nyingine.
 
Sasa huo ni wizi!! Ni mtu mjinga peke yake anayeweza kufurahia kipato cha wizi na cha udanganyifu kisicho halali!! Fikiria msichana anayemkubali mtu anayeonekana ana kipato kikubwa lakini kumbe chanzo chake ni wizi, halafu ni kweli mtupu kuwa siku za mwizi ni arobaini! Kuna siku atakamatwa na kufukuzwa kazi na kifungo juu!! Walimu wana maisha mazuri, wanajua kulea watoto wao vizuri na wana maadili sana!! Inasikitisha watanzania kujivunia kazi kwa kuwa ina "fursa" za wizi na udanganyifu!!
Hakuna kada isiyo na wizi,
Wizi upo kuanzia kwnyw ngazi ya uraisi,bungeni,mawizarani mpk kushuka chini kabisa kwny mahalmashaur.

Ufisadi umewaneemesha mwengi sana,
Hata uku mitaani kwny vibanda vyetu, watumishi wanafanya biashara for leisure, mzigo ukikata, anapiga ufisadi wake anajaza mzigo TU.
Wao suala la kushusha Sana Bei kukimbizana na ushindani hata sio kazi yao. Una hela nunua, huna Ela tembea mbele.

Kingine,
Kwa zama tulizopo,
Hakuna mwanamke ana ubavu /kifua cha kumkatalia mwanaume fisadi hata siku moja, Habar za umezitoa wapi pesa hiyo hata haimuhusu.
mwanamke anachotaka Ni huduma zake zitimizwe TU TU. Full stop
 
Kwenye kata yetu sijaona mtu wa kada nyingine alieomba hizi kazi za muda za sensa ni walimu tu tena ni wengi.

Shule ambayo mkuu wake ndo anafanya usaili ndo wameenda kama walimu shule nzima. Sasa hapo kweli utasema hawa jamaa huko kuna maslahi waanze kugombania hizi kazi ambazo naamini tu ni za shurba na kuzurula kwiingi wakati muda huo ungeutumia kupumzika na familia ama kufanya ishu zako nyingine.
Sahii kabisa
 
Hilo pia siyo kweli! Mtumishi lazima abaki na theluthi moja ya mshahara wake katika mazingira yoyote yale! Nimetoa mfano wa mwalimu graduate ambaya kwa sasa atakuwa anapata 771,000/=. Huyo akikopa sana lazima abakize sh 257,000/= kwenye mshahara wake. Lakini pia wengi wanakopa siku hizi kwa ajili ya kuendesha miradi mbalimbali kama kuku wa mayai au nyama, ng'ombe wa maziwa, shamba nk. Kwa hiyo japo anabakiza mshahara kidogo lakini ana kipato kingine cha pembeni na cha halali kuliko wale wanaojisifia wizi!!

Walimu wana maisha mazuri sana kwa kutumia akili yao kwa halali. Nenda shule yoyote iwe ya msingi au ya sekondari uangalie magari ya walimu waliyopaki hapo. Walimu wengi wamejenga nyumba zao za kisasa na wana miradi mbali mbali na watoto wao wanasoma vizuri kwenye shule nzuri. Tatizo mmekaririshwa matango pori!
Hayo magari mengi ni ya wanawake wamenunuliwa na waume zao.
Maendeleo ni akili sio kipato,kama akili ipo popote penye watu pana pesa ukiona mtu ni pesa ni akili yako tu umuuzie huduma au bidhaa Ili uchukue pesa yake.
 
Kwenye kata yetu sijaona mtu wa kada nyingine alieomba hizi kazi za muda za sensa ni walimu tu tena ni wengi.

Shule ambayo mkuu wake ndo anafanya usaili ndo wameenda kama walimu shule nzima. Sasa hapo kweli utasema hawa jamaa huko kuna maslahi waanze kugombania hizi kazi ambazo naamini tu ni za shurba na kuzurula kwiingi wakati muda huo ungeutumia kupumzika na familia ama kufanya ishu zako nyingine.
Hicho ni kipato cha ziada na hana sababu ya kutokukihitaji! Hiyo ni akili kubwa! Nimekuambia kuwa kimsingi watumishi wa serikali walio wengi mishahara yao ni kidogo sana. Huyo ambaye hajaomba si kwamba yeye ndiyo mwenye mshahara mkubwa. Halafu taaluma ya ualimu imewafanya wawe na ufahamu wa mambo mengi na wanajiamini kuwa kwenye usaili watafanya vizuri!! Wengine yawezekana wanapenda pia kuomba nafasi hizi lakini hawajiamini kama watafailu kwenye usaili maana huko watapambana na walimu pia ambao ubongo wao una chaji muda wote!!
 
halafu ni kweli mtupu kuwa siku za mwizi ni arobaini! Kuna siku atakamatwa na kufukuzwa kazi na kifungo juu!! Walimu wana maisha mazuri, wanajua kulea watoto wao vizuri na wana maadili sana!! Inasikitisha watanzania kujivunia kazi kwa kuwa ina "fursa" za wizi na udanganyifu!!

Mkuu,
Hebu achana na hekaya za
"za mwizi arobaini"

Za mwizi zinafika kwa yule anaepiga hela za kipumbavu, ila yule anaepiga ufisadi wa kueleweka hata jela haendi.

Mf: unapiga dili la billion moja ,
afu ukipelekwa mahakamani unahonga Kama mil.200 kwa waendesha mashtaka,mawaliki wa serikali na majaji,
Mchongo ni unakiri kosa HARAKA ili usisote Sana jela ili kusubir uchunguzi.
afu jaji anakuhukumu kulipa faini ya mil.10 au kifungo Cha miaka 5 kwa kuisababishia serikali hasara ya bil.10.
unalipa faini unatoka, unatembe zako na bakshishi ya mil. 710 kibindoni
 
Hayo magari mengi ni ya wanawake wamenunuliwa na waume zao.
Maendeleo ni akili sio kipato,kama akili ipo popote penye watu pana pesa ukiona mtu ni pesa ni akili yako tu umuuzie huduma au bidhaa Ili uchukue pesa yake.
Huo pia ni uongo wa kukaririshwa!! Fanya utafiti kidogo utajua kuwa umeamini uongo. Mimi hapa nina majirani walimu kibao, wanaishi kwenye nyumba zao za maana na wana vyombo vizuri (magari) vya usafiri.
 
Hakuna kada isiyo na wizi,
Wizi upo kuanzia kwnyw ngazi ya uraisi,bungeni,mawizarani mpk kushuka chini kabisa kwny mahalmashaur.

Ufisadi umewaneemesha mwengi sana,
Hata uku mitaani kwny vibanda vyetu, watumishi wanafanya biashara for leisure, mzigo ukikata, anapiga ufisadi wake anajaza mzigo TU.
Wao suala la kushusha Sana Bei kukimbizana na ushindani hata sio kazi yao. Una hela nunua, huna Ela tembea mbele.

Kingine,
Kwa zama tulizopo,
Hakuna mwanamke ana ubavu /kifua cha kumkatalia mwanaume fisadi hata siku moja, Habar za umezitoa wapi pesa hiyo hata haimuhusu.
mwanamke anachotaka Ni huduma zake zitimizwe TU TU. Full stop
Mwalimu, mwanajeshi,askari jela,anakula wapi kwa mfano.

Hizo biashara zote za watumishi huwa zinastaafu pindi mtumishi akistaafu au fukuzwa Kazi au hamishwa maana zinaendeshwa kwa nguvu ya ofisi na sio nguvu ya biashara
 
Back
Top Bottom