Mlioijaribu Bia ya Arusha almaarufu "Banana", hebu tupeni feedback

Hahahhaa, hii kitu inaonekana ni shigida maana hakuna hata mmoja ambaye ameipatia.
 
Nakumbuka ushirika moshi....hiii kitu ilikua nikiweka tatu kichwani naweza kufanya maajabu kesho yake nasimuliwa siamn
 
du ! Jamaa muongo wewe..saa dola 170 unakunywa matapu tapu ya sh.200 ?
Why cant u use ur head just for once?
Wote wafanyao vitu vya bei rahisi does that mean hawana uwezo wa kufanya makubwa? Acha mazoea there is always the first time of everything!
Mi mwenyewe nilikunywa si kama sikuwa na afford cha gharama just that i wanted to feel the taste and rythim!
 
Jaribu tu mkuu utajutia maamuzi yako, tena zipo aina kama tatu hivi kama sijakosea kuna kibo, raha na kiboko embu anza na hio kibo kwanza afu uje ulete mrejesho hapa.kila kheri
Kuna nyingne inaitwa bhunubunduu inatengenezwaa kuleee ngalimii ukipiga mbilii ukasimama we kidumee
 
Wakuu hiyo kitu ni nuksi...

Wazee huku Chuga wamezibwa vibofu vya mkojo...

Ni mwendo wa kuchomekwa mpira tuu
 
Banana imeharibu vijana wengi sana wa mwanama, nina mtoto wa dada angu, akishakunywa bananan tu cku hiyo hakuna kulala, anakusanya mawe, anapiga bati huku analia mpaka kuna kucha, jamani sijui ni kitu gani kipo kwenye banana, mkimsogelea hamtabaki salama mvua ya mawe inahamia mwilini kwenu. Sijui kwa nini huwa anapiga bati>
 
Banana moja ni sawa na bia 5 kudadeki, niilikunywa 3, nikalala hadi kesho yake saa 10 . Safi sana.
nilianza kwa kunywa mbili, baadae tatu,,, saba..... Hadi mwisha naacha kuzinywa (sisemi sitazinywa tena) nilikuwa na uwezo wa kunya banana 10 ndani ya usiku mmoja tu. lakini tatizo ukiamka asubuhi mdomo unanuka ka umekula kinyesi cha binadamu. tena utahitaji maji menge sana ili kuuweka mwili sawa
 
Banana ni kiwanda cha pombe ya ndizi na wala si pombe kama ulivyotanabaisha.

Hizi ni bidhaa zinazozalishwa na kiwanda cha BANANA Inv co.

1. MERU WINE
2. MALKIA
3. RAHA POA
4. FIESTA GIN
5. MZALENDO WATER
 
ila mngejua hizo ndizi zinavyoandaliwa hat msingejaribu kuonja, yaani ndizi zinavundikwa kwenye mashimo kisha zinajazwa kwenye mapipa, zinaorojeka mpaka ziwe na wadudu ndo zinatengenezea hiyo pombe.
 
Aisee arif hilo zaga ni kwere babalai..nilikulaga ile Raha Poa tano nikalala mlangoni mpaka asubuhi. Enzi ile ikiwa kwenye chupa ya kioo unafungua kwa process kama kizibo cha rejeta iliyochemsha.
 
Nimekuwa nikikatiza maeneo na kukuta hii Bia ingawa binafsi sijawahi ijaribu...ila natamani nione what a local beer has to offer, especially from Arusha!

Mliowahi jaribu hii kitu, je ipo level za kina Serengeti na Kilimanjaro? Wengine walikuwa wanasema ati mataputapu, msemo huu una maana gani?

Mnaoiponda mna uwezo mdogo wa kustahimili pombe.. M nlizianza 2007 had 2010 ilkuwa bia yangu... Baadae nkaenda zenji nikaa huko nikasahau..
Ila had kesho naipenda banana..
 
Manina hiyo kitu sitak kusikia nilikunywa tatu mwaka2005 nikalewa chaka nikaanguka saa yangu ya mkononi ya dola 170 ikapasuka. Sitaisahau milele aisee.

Duc in Altum
Doh! Umekula taputapu na kidonda cha $170? hatari sana Mkuu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom