GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 56,518
- 108,793
" Mjuukuu Wangu asikuambie Mtu Siasa za Afrika ni za Kimafia sana na yakutaka uwe na Uwezo mkubwa wa Kuyaona ya mbali. Yaliyotokea jana Mwanza hayakuwa matakwa ama Binafsi au ya Taasisi husika ya Kisiasa bali Watu wameshachungulia na Kuona Kesi zao Lukuki zilizopo Mahakamani kuna Moja hiyo hawawezi Kutoka na Hukumu ikitoka wanaenda Kuozea Jela hivyo ulichokiona jana ni sehemu ya Mtoto Kumuomba Msamaha Baba ili hata Watoa Maamuzi Mahakamani nao walegeze Kamba na Watu wasiende Kuozea Segerea. Leo hutonielewa ila ipo Siku utanielewa Mimi Babu yako na hizi Kesi zote zitaisha na watakuwa Huru tu "
Najua JamiiForums ni Uwanja / Jukwaa la Watu ' Werevu ' sana ( Ukimuondoa tu GENTAMYCINE pekee ambaye ni Popoma Aliyetukuka ) hivyo ni imani yangu ' Werevu ' mliopo hapa mtanisaidia Kunielewesha vyema hizi Kauli za huyu Babu ambaye nilibahatika Kukaa nae leo katika Siti tukitokea Mbagala Kizuiani kuelekea Mbagala Charambe ambako nafanya Kazi zangu za Kuuza Mkaa na Nyasi za Ng'ombe kwa Bei nafuu kama siyo ya Kutupwa.
Karibuni.