Mlioielewa Kauli hii ya Kimafumbo ya huyu Mzee niliyepanda nae Daladala leo asubuhi nisaidieni Kunielewesha

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,054
107,538
" Mjuukuu Wangu asikuambie Mtu Siasa za Afrika ni za Kimafia sana na yakutaka uwe na Uwezo mkubwa wa Kuyaona ya mbali. Yaliyotokea jana Mwanza hayakuwa matakwa ama Binafsi au ya Taasisi husika ya Kisiasa bali Watu wameshachungulia na Kuona Kesi zao Lukuki zilizopo Mahakamani kuna Moja hiyo hawawezi Kutoka na Hukumu ikitoka wanaenda Kuozea Jela hivyo ulichokiona jana ni sehemu ya Mtoto Kumuomba Msamaha Baba ili hata Watoa Maamuzi Mahakamani nao walegeze Kamba na Watu wasiende Kuozea Segerea. Leo hutonielewa ila ipo Siku utanielewa Mimi Babu yako na hizi Kesi zote zitaisha na watakuwa Huru tu "

Najua JamiiForums ni Uwanja / Jukwaa la Watu ' Werevu ' sana ( Ukimuondoa tu GENTAMYCINE pekee ambaye ni Popoma Aliyetukuka ) hivyo ni imani yangu ' Werevu ' mliopo hapa mtanisaidia Kunielewesha vyema hizi Kauli za huyu Babu ambaye nilibahatika Kukaa nae leo katika Siti tukitokea Mbagala Kizuiani kuelekea Mbagala Charambe ambako nafanya Kazi zangu za Kuuza Mkaa na Nyasi za Ng'ombe kwa Bei nafuu kama siyo ya Kutupwa.

Karibuni.
 
Kama umeona maneno ya huyo babu ni fumbo basi una uwezo mdogo sana wa kuelewa mambo. Yeye hapo ameeleza mambo waziwazi, sasa wewe unaloona hapo kuwa fumbo ni nini? Nini hapo kinachohitaji kufafanuliwa kwa mtu mwenye akili?

Na ndiyo maana kwa ' Upopoma ' wangu ' Ulionitukuka ' nimeona niwaulizeni nyie ' Werevu ' Mkuu na hata Wewe ukiwemo je, hapo tatizo liko wapi? Kwani Sisi ' Mapopoma ' hatutakiwi Kupewa Ufafanuzi na Watu ' Werevu ' kama Wewe? Kinachonisikitisha tu ni kwamba pamoja na Uelewa wako ( Uwerevu wako ) lakini ndani ya hizo Kauli za huyo Mzee umeshindwa Kung'amua / Kuelewa Fumbo hapo na unanishangaa tena na Mimi.
 
Kwa uwezo wako wa kuchambua mambo ambao umeshathibitika ndani ya post zako GENTAMYCINE ulipaswa kuiripoti hii kama habari ilivyo, sio kama fumbo. UKisema ni fumbo unafanya watu tunaokufahamu tusikuelewe.
 
Mawazo mgando ya huyo mzee kesi nini mbona Mbowe alikaa mahabusu Siku 104 lakini hakuomba msamaha? Unapokuwa mpinzani dhidi ya chama tawala kufungwa ni sehemu ya maisha na kama unaogopa kufungwa kama Lowassa na wasaliti wengine utajitoa upinzani.
 
Na ndiyo maana kwa ' Upopoma ' wangu ' Ulionitukuka ' nimeona niwaulizeni nyie ' Werevu ' Mkuu na hata Wewe ukiwemo je, hapo tatizo liko wapi? Kwani Sisi ' Mapopoma ' hatutakiwi Kupewa Ufafanuzi na Watu ' Werevu ' kama Wewe? Kinachonisikitisha tu ni kwamba pamoja na Uelewa wako ( Uwerevu wako ) lakini ndani ya hizo Kauli za huyo Mzee umeshindwa Kung'amua / Kuelewa Fumbo hapo na unanishangaa tena na Mimi.
Mkuu GENTAMYCINE, tatizo kubwa la watu wanaofikiri mbali kama wewe ni kwamba hata mkiambiwa kitu rahisi sana, mnakwenda mbali kuliko kile alichokusudia yule anaekuambia hicho kitu. Wakati nikiwa shule tunachambua vitabu vya kina Shaaban Robert, Kezilahabi, Chinua Achebe, nk, nilikuwa najiuliza, hivi hawa jamaa walioandika hivi vitabu waliandika kwa maana ya haya mawazo tunayochambua au wao walikuwa wanaandika stori rahisi tu ila sisi ndio tunachambua kuliko hata mawazo yao yalikofika? Kuna wakati hata nilihisi tukiwapa uchambuzi tuliofanya hata wao wanaweza wasielewe!

Huyu babu katoa very simple statements. Usiende mbali na kuwa too academic na alichosema. Zielewe kama zinavyosema.

Mwanzoni hata nilikuwa nafanya hivyo kwa kauli za kina Magufuli, Bashiru, Ndugai nk. Then nikaja elewa kuwa sihitaji ku-crack kichwa changu ku-synthesize wanachotamka ili kuelewa wanachosema. Huwa hawaendi mbali kiasi hicho, wanachotamka ndicho wanachosema ndio maana sometimes wanachotamka haki-make sense kwa wengi wetu kwwa sababu tunaenda mbali zaidi yao! We basically give them more credit in what they say than they deserve!

Mtu kama Nyerere atatamka maneno kama ""Small nations are like indecently dressed women. They tempt the evil-minded." Sasa hii ni class ya statement ambayo siwezi kuwaweka watu kama hao kutamka maneno kwa upeo wa level hii ya Nyerere! So I just take what they say to be what they mean.
 
Kama umeona maneno ya huyo babu ni fumbo basi una uwezo mdogo sana wa kuelewa mambo. Yeye hapo ameeleza mambo waziwazi, sasa wewe unaloona hapo kuwa fumbo ni nini? Nini hapo kinachohitaji kufafanuliwa kwa mtu mwenye akili?
Actually everything is so obvious, doesn't need a genius to understand!!
 
Nimewahi kufanya kazi na Mbowe na najua anavyoona mbali, lakini pia anapenda sana upatanishi na kelegeza kamba anapoona maslahi yake binafsi yako hatarini. Au yuko radhi kukosana na yeyote anapoona mahusiano fulani yana maslahi makubwa kwake binafsi. Kwa vyovyote vile iwavyo (pengine hata kwa unafiki), kukaa pamoja watu wa taifa moja kunapendeza sana na kunapunguza mno misuguano isiyo na tija. Zaburi 133:3
 
Nadhani huyo mzee alikuwa anabashiri tu! Kama ingekuwa kwamba wanaogopa kuozea jela,huenda wengi wao wangekuwa wameshajiunga na CCM kuunga juhudi kama akina Waitara! Maana ukishaunga juhudi hata kama ulikuwa na kesi ya mauaji inafutwa.
 
9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom